JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Jamani wazazi tunalia na michango ya Shule ngazi ya kidato cha tano, Serikali imetangaza kufuta ada kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita kwa shule za Serikali lakini tunachokutana nacho huku kwenye uhalisia ni tofauti.
Tunaambiwa ada imefutwa lakini katika masharti au form za Watoto kujiunga na masomo katika ngazi ya Kidato cha tano tunaambiwa kila Mwanafunzi anatakiwa kulipa Tsh 65,000 ikiwa ni “Mchango wa Uendeshaji wa Shule”, malipo ambayo yanatakiwa kufanyika katika akaunti ya Shule husika
Kiango hicho ni mbali na malipo mengine madogomadogo kama nilivyoambatanisha kwenye hizo form.
Tunaomba Serikali imulike Shule ya Sekondari Longido Mkoani Arusha au iwekwe wazi ili Serikali nayo itoe msimamo wake kuwa ada zimefutwa au la? Au zimefutwa lakini zinarejeshwa kwa njia nyingine?
UPDATES...
Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa, anafafanua:
Tumeshatoa waraka kuandikia wote, michango ni hiyari, hivyo unatakiwa kuuliza shule husika, ukifuatilia kama kuna michango ya ziada inamaanisha Shule imekaa na wazazi wakakubaliana na suala la mchango husika.
Kama mzazi anaweza kuacha kuchangia kwa kuwa sio lazima na akiwa hana anaweza kuzungumza na shule husika wakaelewana.
Taarifa ya Mwalimu Mkuu wa Longido, inafafanuzi:
“Hicho kiwango (Tsh. 65,000) kipo lakini kiwango hicho kimepitishwa na TAMISEMI na wanakifahamu, kuna maelekezo rasmi kuwa kuna kiwango fulani hakitakiwi kuvukwa.
“Kama kuna mzazi ambaye anaona kuna jambo halipo sawa, anaruhusiwa kuuliza kwa kuwa form ya kujiunga na Kidato cha Tano ina namba zote za Walimu wanaohusika.
“Hakuna nafasi ya kumuelekeza mzazi mmojammoja kwa kuwa tayari form zipo kwenye tovuti ya shule na maelekzo hayo.
Kwa ufupi hatujaongeza kitu kutoka katika utaratibu au muongozo uliotolewa na TAMISEMI, tulichobadilisha pale labda ni jina la Shule na sare.”