Hussein Pambakali kizimbani kwa utapeli wa 75ml

Hussein Pambakali kizimbani kwa utapeli wa 75ml

wang'ambo

Senior Member
Joined
Nov 29, 2015
Posts
105
Reaction score
27
MMILIKI wa maduka ya nguo Jijini Dar es Salaam,Hussein Mkangala (38) maarufu 'Hussein Pamba Kali' amefunguliwa mashtaka ya kesi ya madai baada ya kushindwa kulipa Sh.Milioni 75 alizokopa kutoka kwa Anna Kiabi.

Shauri hilo lilitajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo upande wa mdai ulikuwa unasimamiwa na Wakili Jonas Nkya, wakati ule wa mdaiwa ukiongozwa na Ernest Swai.

Mbele ya Hakimu Is -Haq Kuppa, Upande wa mdai ulisema kwamba Novemba 20 mwaka jana mfanyabiashara huyo alikopeshwa kiasi cha sh. Miloni 80 kwa makubaliano atamlipa kwa kipindi walichokubaliana kitu ambacho amevunja makubaliano.

Wakili Nkya alidai Mei 22 mwaka huu mdaiwa Husseni alimtuma mdogo wake aitwaye Hassan Mkangala, apeleke fedha kiasi cha sh. Milioni 5 kwa Anna na kiasi kilichobakia hakulipa tena.

Kwa upande wa utetezi wao waliomba mahakama hiyo iwape muda wa siku 6 ili waweze kujibu madai hayo.

Hivyo Hakimu Kuppa aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena lakini Mdaiwa hakufika mahakamani.

Chanzo: Michuzi blog
 
Sasa Pambakali angezipata wapi wakati shule kaogopa umande na kazi hapendi kutoka jasho! utaalamu wake upo mdomoni! Leo kashikwa utapeli, subiri kesho ni ugoni. Mdomo wake mwepesi kutongoza!
Hahaa Share bwana
 
Sasa Pambakali angezipata wapi wakati shule kaogopa umande na kazi hapendi kutoka jasho! utaalamu wake upo mdomoni! Leo kashikwa utapeli, subiri kesho ni ugoni. Mdomo wake mwepesi kutongoza!

Alikua bwanako nini akakutosa? Acha wivu wa kike na kushupalia ujinga.. Waongea Kama umemeza betri kutoa ushahidi hewa hapa.
 
Sasa Pambakali angezipata wapi wakati shule kaogopa umande na kazi hapendi kutoka jasho! utaalamu wake upo mdomoni! Leo kashikwa utapeli, subiri kesho ni ugoni. Mdomo wake mwepesi kutongoza!
Umemmaliza...Ngoja asote huko lupango labda ndo panamfaa
 
Hilo ni deni dogo?

Mbona anadaiwa sasa...si alilipe kama ni dogo.

Pamba zenyewe feki feki feki.

Sijajua kwa upande wako mkuu, Ila 80m ni ndogo kwa mfanyabiashara Kama Husein...

Kuhusu ufeki wa nguo anazouza hayo ni majungu binafsi.. Nakupa id yake soon mmalizane
 
Sijajua kwa upande wako mkuu, Ila 80m ni ndogo kwa mfanyabiashara Kama Husein...

Kuhusu ufeki wa nguo anazouza hayo ni majungu binafsi.. Nakupa id yake soon mmalizane
Ingekuwa ni ndogo angeshitakiwa?

Si angekuwa keshailipa zamani za kale...

Acha kurahisisha mambo bana.

Mtu kashitakiwa kwa kushindwa kulipa halafu we unasema hicho ni kiasi kidogo?
 
Umemmaliza...Ngoja asote huko lupango labda ndo panamfaa

Tatizo kubwa la vijana ni wivu wa maendeleo.. Yaani hampendi kuona mtu anafanikiwa. Sasa aliekuambia ataenda lupango kwa ajili ya 75m ni nani?

Pili, umeambiwa kesi imeenda mahakamani Leo, Hata Husein mwenyewe hakuepo, huenda hata madai yenyewe ni fake,lengo kuchafuana tu. Subiri mahakama iamue Ndo uzungumze kitu
 
Ingekuwa ni ndogo angeshitakiwa?

Si angekuwa keshailipa zamani za kale...

Acha kurahisisha mambo bana.

Mimi huwa nadhani Una uelewa mkubwa kumbe bure kabisa, kesi imefunguliwa Leo na hujui kama anadaiwa Kweli au lah, ushanza kushabikia na kuponda bidhaa zake.. Natamani sheria nchi Hii wangeanza kufundisha toka la kwanza.
 
hii dar ina mengi, huyu si nilisikia anajenga mall
 
Mimi huwa nadhani Una uelewa mkubwa kumbe bure kabisa, kesi imefunguliwa Leo na hujui kama anadaiwa Kweli au lah, ushanza kushabikia na kuponda bidhaa zake.. Natamani sheria nchi Hii wangeanza kufundisha toka la kwanza.

Sasa kama hadaiwi mashitaka yamefunguliwa kwa ajili gani?

Wanaigiza bongo muvi?

Wahshi kabisa wewe na huyo muuza pamba feki feki feki.
 
Sasa kama hadaiwi mashitaka yamefunguliwa kwa ajili gani?

Wanaigiza bongo muvi?

Wahshi kabisa wewe na huyo muuza pamba feki feki feki.

Wangapi washafunguliwa mashtaka mahakamani na hata kwenda mahabusu miaka kadhaa lakini hukumu inatoka wanakutwa hawana hatia?

Fanya kazi, kua mbunifu ili na wewe upate mafanikio, wivu wa namna hii utazidi kuumiza Moyo wako tu.

Mcpoangalia mtaendelea kulishia wazungu mbwa wao Milele mwishowe mrudi nchini mmezeeka na mifuko mitupu Kama Lemutuz
 
Back
Top Bottom