Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi atashinda uchaguzi, Maalim Seif atashinda kura

TWisheshagi

Member
May 2, 2020
10
100
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimehitimisha mchakato wa kupata mgombea wake wa urais kwa upande wa Zanzibar.
Ni Hussen Ali Hassan Mwinyi. Mwanasiasa mtulivu, mkimya na asiyependa kujikweza.

Zipo tetesi kuwa ukimya wa Hussein Mwinyi, unavuka mipaka ya kawaida. Hata kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri hakuwa mzungumzaji mzuri.

Kuna nyakati hata alipoombwa kutoa maoni yake aliishi kusema:"Naunga mkono yote yaliokwisha kusemwa na wenzangu" na kisha aliketi.

Tetesi hizi ni vigumu sana kutoziamini kwa sababu zinaeleza tabia halisi ya Hussein Mwinyi. Ukimya wake unaacha maswali mengi kuliko majibu.

Wapo wanaoamini kuwa ukimya wa Hussein siyo Udhaifu wake. Utii wake kwa viongozi wake si Ujuha! Mawazo haya yanaweza kumshawishi yeyote.

Lakini ukweli wa MUNGU, ni hatari sana kumkabidhi madaraka makubwa mtu ambaye misimamo yake haijulikani bayana.

Nimesema ni hatari kumkabidhi "madaraka" si kwa bahati mbaya. Ukweli ni kwamba kwa siasa za Zanzibar, na ukiritimba wa CCM ulivyo, inawezekana kabisa, Hussein Mwinyi ndiye Rais ajaye wa Zanzibar.

Ni ukweli mwingine kuwa, hana ushawishi mkubwa Zanzibar, hana umahiri mkubwa wa siasa za Zanzibar, hajawahi kujipambanua kama mtetezi halisi wa maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano.

Hulka za ukimya wake, zimetunyima fursa wengi ya kujua na kumfuatilia kama mtetezi wa maslahi ya Zanzibar.

Katika hili ninaweza kusema kwa wazi na kujiamini kabisa kuwa, kwa Mara nyingine tena historia imeandikwa kutokea Tanganyika. Nina maana kwamba, Rais wa Zanzibar amechaguliwa kutoka bara(Tanganyika)

Wapo Wan zanzibar wanaoupenda sana Muungano, lakini daima huchukizwa sana na tabia ya dola la Tanganyika kuwachagulia Rais wao.

Watu wenye hisia kama hizi bado wapo zanzibar! Wanaupenda Muungano wetu, lakini hawapendi namna tunavyoishi nao ndani ya Muungano. Hawa wamekubali kuishi katika hali wasiyoweza kuibadili.

Hulka ya Wan zanzibar wengi ni kupenda kwanza Zanzibar kabla ya kupenda Muungano! Kwao mtu mwenye kutetea Zanzibar kwanza ni bora zaidi kuliko yule anayetetea Muungano kwanza.

Sifa hii haipo kwa Hussein Mwinyi. Sifa hii anayo Maalim Seif Sharrif. Maalim Seif amekuwa kipenzi cha Wan zanzibar kwa muda wote kwa sababu ameweza kusoma hisia zao.

Seif Sharrif, anajua Wan zanzibar wa napenda kusikia kitu gani. Kama kuna jambo linalowaunganisha Wanzibar wote popote walipo Duniani ni Uhuru wao na maslahi ya Zanzibar. Maalim Seif amekuwa wazi mno katika hili, ndio maana hachuji katika siasa za Zanzibar.

Wapo wana-CCM wanakubaliana na hilo. Tofauti pekee ni kuwa wao hawasemi hadharani. Wengi hutumia majina bandia kwenye mitandao ya kijamii kutapika nyongo zao ili wapate usingizi.

Hulka hiyo haipo kwa Hussein Mwinyi. Sioni kwa namna gani anaweza kuwaaminisha Wazanzibari kuwa anaweza kutetea maslahi yao japo kwa bahati mbaya.

Ninaona turufu ya wazi kwa Maalim Seif Sharrif Hamad. Hussen Mwinyi, atashinda Uchaguzi, Maalim Seif Hamad, atashinda kura na Mzee Jecha, atazihesabu kura tena.

Ndimi Mkulima wa Miwa, Bonde la Mto Simiyu- Magu-Mwanza
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,050
2,000
Zanzibar safari hii wakikubali utawala wa "KIFALME", ule wa mtoto kamrithi baba, wameumia milele daima. Shauri yao.

Baba Rais Karume, akapokea kijiti Mtoto Rais Karume. Baba Rais Mwinyi, sasa anapewa kijiti Mtoto Mwinyi.
 

SeliSelina

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
209
500
Haikuwahi kutokea CCM ikashinda uchaguzi Zanzibar, labda kidogo yule kijana (ayoub) watu walimpenda wote, huenda angepata angalau asilimia kidogo, lakini wote walobakia hamna hata mmoja angeambulia kitu, kwa hivyo kwa kupiga kura tuu, CCM haina lake jambo zanzibar, kama kawaida watu watapiga kura, kisha hawatojali maamuzi ya watu, watafanya wanavyotaka ndio walivyozoea.

Mtihani mkubwa sana waliokuwa nao Wazanzibar.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
31,115
2,000
Maalimu Seif toka aanze kugombea Zanzibar hadi leo wameshapita marais wangapi.
 

Bruno Toto

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
397
500
Mimi nawashangaa Sana nyinyi mnaosema eti utawala wa kifalme, kwani Kama Baba yako aliwahi kuwa Rais huko nyuma we mtoto unakosa vigezo? Katiba inasemaje? Kina George Bush senior na junior mliwaita wafalme? Huyu waziri mkuu wa sasa wa Canada mbona hamumuiti mfalme? Baba yake si alikua waziri mkuu na yeye?
Zanzibar safari hii wakikubali utawala wa "KIFALME", ule wa mtoto kamrithi baba, wameumia milele daima. Shauri yao.

Baba Rais Karume, akapokea kijiti Mtoto Rais Karume. Baba Rais Mwinyi, sasa anapewa kijiti Mtoto Mwinyi.
 

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
6,834
2,000
Haikuwahi kutokea CCM ikashinda uchaguzi Zanzibar, labda kidogo yule kijana (ayoub) watu walimpenda wote, huenda angepata angalau asilimia kidogo, lakini wote walobakia hamna hata mmoja angeambulia kitu, kwa hivyo kwa kupiga kura tuu, CCM haina lake jambo zanzibar, kama kawaida watu watapiga kura, kisha hawatojali maamuzi ya watu, watafanya wanavyotaka ndio walivyozoea.

Mtihani mkubwa sana waliokuwa nao Wazanzibar.
Akae Ayoub au yoyote yule CCM, Seif hapotezi kura hata moja. Wazanzibari huwajui bado
 

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
6,834
2,000
Mapendekezo ya CCM Zanzibar yalijaa walafi na wizi tu. Wacha Mwinyi aogoze miaka yake 10. Wakiacha upumbavu wao labda chaguo lao litakubalika 2030
 

Jimbi

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
2,416
2,000
Mapendekezo ya CCM zanzibar yalijaa walafi na wizi tu.... Wacha Mwinyi aogoze miaka yake 10. Wakiacha upumbavu wao labda chaguo lao litakubalika 2030
Kulikua na SHINIKIZO Mkuu, yale majina 5 hayakuwa chaguo HALISI la Wazanzibari wenyewe.
 

Bungua

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
580
500
Mimi nawashangaa Sana nyinyi mnaosema eti utawala wa kifalme, kwani Kama Baba yako aliwahi kuwa Rais huko nyuma we mtoto unakosa vigezo? Katiba inasemaje? Kina George Bush senior na junior mliwaita wafalme? Huyu waziri mkuu wa sasa wa Canada mbona hamumuiti mfalme? Baba yake si alikua waziri mkuu na yeye?
Wewe toto kweli. Jiulize kwa nini asemwe Putin lakini Angela Merkel hasemwe!
 

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,511
2,000
TWisheshagi,
Nimeshasema mara kadhaa na ninarudia tena, wazanzibari wana haki ya kuwa huru na kujitawala wenyewe. Zanzibar ingekuwa mbali sana kimaendeleo/kiuchumi kama ingekuwa ni taifa huru. Huu ujinga unaondelea kuna siku wazanzibari watasema enough is enough na the unthinkable will happen.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom