Husein Yahaya: Hakuna uchaguzi mwaka huu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Husein Yahaya: Hakuna uchaguzi mwaka huu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muheza2007, Mar 25, 2010.

 1. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Watabiri wengine mnasemaje? Mwenzetu kwa kutabiri ujinga ujinga, anapata kila aina ya misaada toka kwa viongozi wetu.
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Source pls!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Anaongea na waandishi wa habari.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  nimemsikia hata Kibonde kwenye Jahazi akisema mh haya ngoja tuone safari hii kama utabiri wake utatimia maana Kakobe ye alisema umeme utakaopitishwa kwenye zile nyaya zilizosababisha mabango yake yakatolewa hautowaka. Yangu macho
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyu si ndo ametabiriwa kufa mwaka huu, labda ameshaanza kuota ndogo za kufakufa na kuzimu. mchawi huyu hana lolote, pamoja na kwamba ni tegemeo kubwa kwa viongozi wetu. siku atakapotunguliwa na Mungu mwenyewe ndipo wale waliokuwa wanamtegemea watakapotunguka vilevile. your days are coming,,,coming and its gonna be soon.
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Huyu mganga wa kienyeji anamatatizo sana, anabahatisha bahatisha mambo meengi ili moja likikubali aje ajisifu kuwa yeye ni rafiki wa Shetani na huwa anampa siri za mbinguni!
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sisi watanzania hasa tunapenda kukuza mambo!....mzee mmoja anakaa kuganga njaa sie tunampublish Tanzania nzima! as if he can make a difference
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Mwenzenu ana link na Ofisi kuu, labda kesha ambiwa mwaka huu tutasimamisha uchaguzi mkuu hivyo anza kutangaza maana ile ya kufa mtu wameona watu haiwatishi.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  “Enyi Mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi za shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa”
  (Q 5: 90).

  Msile nyama yo yote yenye damu ndani yake, Msifanye uaguzi wala uchawi.
  Walawi 19:26
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kisha tunaambiwa Sheikh Yahya kabobea kwenye Uislam! kumbe dini yake inamkataza....agggr
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Na ule utabiri wa kuwa Wanaompinga JK watakufa ulifutika? Hivi ugonjwa wa Alzheimer ulimuanza lini huyu mnajimu?

  Au amesha anza kupagawa na mental disorder characterized by abnormalities in the perception or expression of reality inayoitwa Schizophrenia, imeshaanza kumpata huyu.

  Sasa anakuwa na auditory hallucinations, paranoid or bizarre... AU ndio delusions zilizo na occupational dysfunction?
   
 12. O

  OkSIR Senior Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona ajawahi kutabiri kumegewa mkewe kale cheupe chake!!!
  ama mpaka wamwage radhi watu hadharan ndio atatabiri
  tushamchoka na yeye!!!!Asubiri kwenda kusali kwa GWAJIMA UFUFUO NA UZIMA
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nadhani siku zake sasa zinarudi zile za utoto wake.
   
 14. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Zachary Kakobe amelalamikia uzushi mzito uliozushwa kuwa alisema kuwa umeme huo hautawaka utakapokamilika.

  Akizungumza na mwandishi wetu juzi Jumapili Askofu Kakobe alisema waliozua uzushi huo wanashangaza kwa kuwa hakusema maneno hayo na kwamba kama wangekuwa wana uwezo huo basi waumini wa Kanisa analoliongoza wasingekuwa na sababu ya kukaa nje ya Kanisa usiku na mchana kulinda.

  “ Ukweli ni kwamba watu wanavumisha kitu ambacho sikukisema, ni maneno ya kishetani, kama tungekuwa na uwezo wa kufanya umeme usiwake kulikuwa na sababu gani ya waumini kukesha hapa huku wakipigwa jua na mvua usiku na mchana?” alihoji Askofu Kakobe.

  Alipoulizwa anadhani kwanini watu hao wanamvumishia kitu ambacho hakukisema, kiongozi huyo wa kiroho alisema anachojua ni kwamba wavumishaji wana shetani mbaya na kwa watu kama hao dawa pekee ni kuwaombea tu waondokane naye.

  “Watu wenye mapenzi mema na Kanisa wapuuze maneno hayo ambayo hata ukiyapima kwa akili ya kawaida utagundua kuwa yamezushwa na watu wenye maslahi nayo na kuwa na chuki na Kanisa,” alisema Askofu Kakobe.

  Hivi karibuni Askofu huyo aliruhusu nyaya za Tanesco kupita nje ya Kanisa analoliongoza na chombo kimoja cha habari kikaandika kuwa amesema umeme huo hautawaka utakapokamilika, hata hivyo, waandishi walioandika hawakufafanua maneno hayo aliyasemea wapi.
  SOURCE: GPL
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mzee Max hapa siyo siri imebidi kusogeza dictionary yangu
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaha, ndo ameshaanza kuchanganyikiwa huyo, si muda ataenda kuokoka pale kwa gwajima, tena sasahivi anahamishia kanisa lake kule kawe, patakuwa patamu, atakaribishwa kwa furaha kubwa siku hiyo ya kuja kuokoka na kuacha uchawi. kama hatafanya hivyo, mwaka huu pengine ni mbaya kwake....mapigo ya moyo yameshaanza kwenda mbio...pressure inapanda, pressure inashuka!
   
 17. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyu si alitabiri Kikwete atakuwa rais mwaka huu au ni mwingine

  "Natabiri kuwa Kikwete ndiye Rais mpya wa mwaka 2010 na atakayempinga katika chama chake atakufa ghafla. Natabiri ushindi wa Rais Kikwete mwakani utaleta serikali ya mseto Tanzania Bara na Tanzania Visiwani," alisema Shekhe Yahya.
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Waandishi wa habari,
  Siku ya Jumatatu Tarehe 27/12/2009 niliitisha kikao kama hichi cha Waandishi wa Habari kuwapa utabiri wa mwaka wa 2010 na nilitabiri mambo mengi ambayo mengine mpaka leo bado yanazungumzwa kwa sababu aidha watu hawakunielewa au wengine hawakukubaliana na utabiri huo kwa maslahi yao.
  Kuna wengine walifikiri nimewalenga wao, kuna wengine walisema nimetumwa niseme niliyoyasema, na kuna wengine watu binafsi na viongozi wa dini waliyakejeli maneno yangu kila mtu kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe.

  Kwanza napenda kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu natoa utabiri kwa manufaa ya jamii kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu aidha kukubali au kukataa haya ambayo niliyoyasema. Katika mkutano huo nilitabiri kutokea kifo cha kiongozi wa wa zamani wa kitaifa na baada ya siku chache alifariki Mhe Rashidi Mfaume Kawawa.
  Nilitabiri atakayempinga Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndani ya CCM kufa ghafla, kauli hiyo ilileta utata mkubwa lakini hilo bado lipo kwa sababu muda wake bado, na kwa ufafanuzi sikusema viongozi wa upinzani nilisema ndani ya CCM.
  Nilitabiri upinzani ndani na nje ya CCM
  Nilitabiri kutokea kwa serikali ya Serikali ya Mseto

  Nilitabiri kwamba hali Hali ya uchumi Tanzania itaboreka

  Nilitabiri kwamba Waziri Mkuu ajaye atatokea upinzani

  Nilitabiri kwamba kutatokea Maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi hasa katika uchaguziwa wabunge
  Na Nilitabiri kwamba kutatokea Kutokea ajali nyingi kwa vyombo vya usafiri na vyombo vya angani
  Katika hayo kuna mengi yameshatokea kimataifa na hapa nchini, na muda wake ukifika hayo niliyoyasema mtayaona.
  Niliwaahidi kwamba kipindi hiki nitawaita tena ili kutoa tena utabiri kwa sababu mwaka wa kinyota unaanzia tarehe tarehe 21/ Machi kwa hivyo kinyota leo ni siku ya tano tangu mwaka wa kinyota kuanza.

  Vile vile mnamo tarehe 15/1/2010 jua lilipatwa na hiyo kinyota ni ishara ya kwamba kuna mambo mengi ambayo sikuwaambia wakati ule yatatokea kwa kupatwa huko kwa jua Huu ni mwaka 2010 na mwaka huu unatawaliwa na nyota ya kumi ambayo ni nyota ya Mbuzi Nyota hii inasimamiwa na sayari ya Saturn au Zohal na inahusika na Mambo Mabaya, Kutenganisha wanandoa, vita, Kukusanya zana za vita, Kuvunjika mambo, kuvunjika Shughuli zozote, kufifia kwa mambo. kushamiri Fitina, na uvumi au mambo ya umbea, Kugombanisha watu, na kutokea magomvi kati ya viongozi wa kisiasa.

  Kupatwa kwa jua tarehe 15/1/2010 kunaashiria vurugu , umwagikaji wa damu, harakati za kijeshi na kashfa za kipolisi , mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbali mbali , uasi wa ghafla katika serikali katika nchi ambazo ambazo zilipitiwa na kupatwa kwa jua ,nchi za Chad, Somalia, Tanzania, Zanzibar ,Congo, Kenya, India, Sri Lanka, Bangladesh na Mayanmar, Vile vile kutokea vurugu za uchaguzi katika nchi hizo.watu kufanya maasi na matukio ya kigaidi kushambuliwa kwa vyombo vya usafiri, kupotea kwa maisha ya watu na mali

  Vile vile kutatokea harusi za viongozi na mazishi ya kitaifa. Vifo vya watu maarufu, matatizo ya kifedha na uchumi, ukame, matetemeko ya ardhi, kulipuka kwa volcano na habari nyingi zitakuwa ni zile zinazihusiana na majanga ya kidunia.

  Kutokana na hayo:-

  Natabiri kwamba hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu Mwaka huu


  Natabiri kwamba Hakutakuwa na mpasuko ndani ya CCM

  Natabiri Uchaguzi ujao robo tatu ya Wabunge wengi walioko madarakani wataanguka.

  Natabiri Bunge lijalo litakuwa litakuwa na sura nyingi mpya na wanawake wataongezeka sana.

  Natabiri Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume Kuongezewa Muda

  Natabiri Nafasi ya urais Zanzibar itakuwa na ushindani mkubwa kuliko miaka mingine yoyote.


  Sheikh Yahya Hussein
  Mnajimu maarufu Afrika mashariki na kati
  Alhamisi 25/3/2010

  Source: Global Publishers na redio za nchini.

  Mh!!!! Huyu inaelekea anatumwa na serikali kufikisha ujumbe kwa wananchi!!!!
   
 19. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nina wasiwasi na elimu ya huyu mtu.

  Wakati mwingine akiulizwa jambo fulani anajibu ovyo ovyo tu. Huwa hajibu maswali kama alivoulizwa, yeye ni mahiri wa kuongea tu kilicho kichwani mwake.
   
 20. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee hajachapwa siku nyingi, simba walitaka kumchapa juzi juzi.Kweli anaota ndoto za kuzimuni.Uchaguzi upo pale pale.
   
Loading...