Unapokuwa na Katiba kama hii ya kwetu na mifumo dhaifu ya uongozi inayotegemea aliyeko madarakani huwezi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ile ukakosa kashfa. Na hata kama itakuwa ndogo kwa kiasi gani, inaweza kukuzwa na kumtia mtu kwenye hatia kubwa tu. Ni hekima zilizokuwa zikifanywa na viongozi waandamizi waliotangulia tu ndizo zimeleta utulivu hadi hivi leo. Akina polepole wajifunze uhalisia huo. Wanaanzisha utamaduni mbaya sana kwenye taifa. Utamaduni wa visasi. Ni vizuri wajikite kujenga Taifa lenye mfumo imara unaoanza na Katiba imara. Nguvu hii waliyonayo inatokana na Katiba hiyo hiyo itakayotumika na "watoto" wa akina Makamba na Kinana kuibua kesi dhidi ya wababe wa leo.
Haya wanayokuja nayo CCM sasa hivi, tutarajie makubwa huko mbele. Si muda mrefu kinga kwa Marais itakuwa historia. Na hapo ndipo tutakapokuja kujua thamani ya uvumilivu, "kupotezea" na heshima kwa viongozi wastaafu.