Humphrey Polepole ‘awashukia’ Kinana na Makamba

Polepole amenukuliwa akiwatupia vijembe vinavyoonekana kuwalenga Makatibu Wakuu Wastaafu wa ccm baada ya kukacha mahojiano juzi huko Dodoma.

"Wakati Rais anamuagiza Waziri Mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa Chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 Bandarini na hayajalipa Kodi, alivyoambiwa alipe kodi sasa ana korosho hivi moyoni kanuna vibaya mno" Polepole

“Ukizingua kwenye chama chetu hakuna mkubwa wala mdogo wote mnaitwa, ukikimbia huna tofauti na wapinzani tu, na watu wa hovyo kwenye chama chetu waondoke tu'' Polepole.

View attachment 1352950

Chanzo: Dar Mpya

==============
NB: Kama Kiongozi alikuwa ana Makontena 700 na hakutaka kuyalipia kodi ilikuwaje haikutangazwa wakati ule, anakuja kutangazwa saizi baada ya kugoma kuhojiwa?

Je, huko CCM kuna wanachama wangapi wanamadudu lakini sababu ni watiifu hamuwatangazi mnasubiri wakikosee chama ndio muwatangaze?

Kwa uzoefu wa Utawala huu je, tutarajie hawa wastaafu kupewa kesi za uhujumu Uchumi kwa kuonekana kukiabisha chama?
Wakimaliza wapinzani watahamia kwa wana CCM na mnukuu Tundu LISSU
 
Fanya siasa safi na isiyo mlenga kumuumiza au kumjenga yeyote, huo Ndio kuwa kiongozi. Ukiona unafanya siasa ili kupambana na fulani au kumsifia mtu bila kufuata kanuni na maslahi ya chama na hitaji la watu ujue siasa zako si Salama na ni Za muda mfupi
 
Yeye ana container ngapi bandarini?Yaani kuwe na kiongozi wa chama mwenye containers 700 hajalipia kodi halafu mnataka kumhoji kamati ya chama badala ya TAKUKURU/Mahakama ya Mafisadi?Huko CCM ni yupi ambaye siyo fisadi?Hiyo kamati yenu ni POLICE,TRA,TAKUKURU au Mahakama?
Ukifikiria propaganda zenu zinaweza kutufikisha kweny nchi ya viwanda vilivyotelekezwa?Mnadhani hatujitambui?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani hata hakajui maana ya makontena 700... Anadhani kontena ni sawa na kreti la soda
 
Fanya siasa safi na isiyo mlenga kumuumiza au kumjenga yeyote, huo Ndio kuwa kiongozi. Ukiona unafanya siasa ili kupambana na fulani au kumsifia mtu bila kufuata kanuni na maslahi ya chama na hitaji la watu ujue siasa zako si Salama na ni Za muda mfupi
Unatetea mafisadi .hovyo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama zipo na polisi wapo, wangewakamata na kuwafungulia mashitaka hao wahusika wa 700 containers.
Sioni mahantiki hapa, kontena ikifika bandarini ndipo utozwa kodi, kutolipa kodi kontena halitoki, sio kukamata mfanyabiasha. Naona mnachanganya mada!
 
Polepole amenukuliwa akiwatupia vijembe vinavyoonekana kuwalenga Makatibu Wakuu Wastaafu wa ccm baada ya kukacha mahojiano juzi huko Dodoma.

"Wakati Rais anamuagiza Waziri Mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa Chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 Bandarini na hayajalipa Kodi, alivyoambiwa alipe kodi sasa ana korosho hivi moyoni kanuna vibaya mno" Polepole

“Ukizingua kwenye chama chetu hakuna mkubwa wala mdogo wote mnaitwa, ukikimbia huna tofauti na wapinzani tu, na watu wa hovyo kwenye chama chetu waondoke tu'' Polepole.

View attachment 1352950

Chanzo: Dar Mpya

==============
NB: Kama Kiongozi alikuwa ana Makontena 700 na hakutaka kuyalipia kodi ilikuwaje haikutangazwa wakati ule, anakuja kutangazwa saizi baada ya kugoma kuhojiwa?

Je, huko CCM kuna wanachama wangapi wanamadudu lakini sababu ni watiifu hamuwatangazi mnasubiri wakikosee chama ndio muwatangaze?

Kwa uzoefu wa Utawala huu je, tutarajie hawa wastaafu kupewa kesi za uhujumu Uchumi kwa kuonekana kukiabisha chama?
Hata huko chadema msaliti haaambiwi akiwa ndani ya chama,ila akijitambua na kuondoka chamani huitwa msaliti,pengine ndio kanuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimae Nawe umewachoka?? Asee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona Makonda hakushitakiwa na makontena yake? Si ajabu kuwa nayo na kushindwa kulipia na kuna utaratibu, na si kosa la kifisadi kama mnataka tuamini, ila pole x2 bado nakutaka kuheshimu wazee, na kama wanamakosa ya kijinai peleka mahakamani, vinginevyo waache!
 
Yaani mtu kutukanwa atukanwe na musiba akilalamika anaitwa kuhojiwa? Hii sijawahi kuiona.bwana polepole ajikite kwenye sababu za kuwahoji hao wazee kutuletea habar za makontena ni kuhamisha magnolia. Atuacheeee
Hivi kweli Mzee Kinana awekwe kwny Kitimoto.na kina Pole pole kujibu Maswali yaliyotengenezwa na Albert Msando yule wa Gigy Money?

Hata kama ni kumtukana Kinana tutafute matusi ya hadhi yake!

Mzee Makamba ni boshen, anaetafutwa ni Jongwe Comrade Abdul rahman Omar Kinana Alhabshy!

Kazi kubwa inayowakabili kina Pole pole ni kulinda Mapinduzi ya 1964 kwny Uchaguzi huu lakin wao kwa ugen wao wa Siasa wanadhan kazi kubwa ni kumsambaratisha Mzee Kinana ambae kwa hiyari yake aliamua kuacha Ukatibu Mkuu!

Unaenda kucheza Mechi ya Fainali lakin uko busy kutuhumu na kudhalilisha Bench lako la ufundi na Kamati ya Ushindi

CCM imevamiwa na Nzige wanaohatarisha Uhai wa Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NB: Kama Kiongozi alikuwa ana Makontena 700 na hakutaka kuyalipia kodi ilikuwaje haikutangazwa wakati ule, anakuja kutangazwa saizi baada ya kugoma kuhojiwa?

Je, huko CCM kuna wanachama wangapi wanamadudu lakini sababu ni watiifu hamuwatangazi mnasubiri wakikosee chama ndio muwatangaze?

Kwa uzoefu wa Utawala huu je, tutarajie hawa wastaafu kupewa kesi za uhujumu Uchumi kwa kuonekana kukiabisha chama?

Nangojea Kamati ya Maadili ya CCM imuite Mkapa kumhoji kuhusu Kiwira Coal Mine na kuuza mashirika ya umma kwa hasara!
 
POLEPOLE JIFUNZE KUNYAMAZA HAO SI VIJANA WENZAKO NI BABA ZAKO, CHEO KWENYE CHAMA KISIKUTIE KIBURI.
Utaratibu huu wa kusema huyu ni mkubwa mimi mdogo siwezi kumkosoa ndio umesababisha ufisadi kushamiri kwa kiwango cha kutisha.

Tabia mbaya sana miongoni mwa waafrika ndio sababu Afrika hatuendelei.
 
Polepole amenukuliwa akiwatupia vijembe vinavyoonekana kuwalenga Makatibu Wakuu Wastaafu wa ccm baada ya kukacha mahojiano juzi huko Dodoma.

"Wakati Rais anamuagiza Waziri Mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa Chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 Bandarini na hayajalipa Kodi, alivyoambiwa alipe kodi sasa ana korosho hivi moyoni kanuna vibaya mno" Polepole

“Ukizingua kwenye chama chetu hakuna mkubwa wala mdogo wote mnaitwa, ukikimbia huna tofauti na wapinzani tu, na watu wa hovyo kwenye chama chetu waondoke tu'' Polepole.

View attachment 1352950

Chanzo: Dar Mpya

==============
NB: Kama Kiongozi alikuwa ana Makontena 700 na hakutaka kuyalipia kodi ilikuwaje haikutangazwa wakati ule, anakuja kutangazwa saizi baada ya kugoma kuhojiwa?

Je, huko CCM kuna wanachama wangapi wanamadudu lakini sababu ni watiifu hamuwatangazi mnasubiri wakikosee chama ndio muwatangaze?

Kwa uzoefu wa Utawala huu je, tutarajie hawa wastaafu kupewa kesi za uhujumu Uchumi kwa kuonekana kukiabisha chama?
Ndio maana tunawaambia ccm wote ni majizi ila hamtaki kukubali moja kwa moja japo uhalisia ndio huo.

Mkuu chama chochote kina kustiri pale unapokuwa nao tu. Ukitoka ndiyo utatolewa madudu yako. Hii siyo ngeni tena. Iwe ccm, iwe chadema au Act wazalenda kuchunguza wote waliohama chama. Mfano mdogo tu mwita waitara na Dr Molell unakumbuka waliambiwaje baada ya kukihama chadema?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Haka ka chakubanga bhana....

Kalikuwa kanamwita Lowassa fisadi alipokuwa upinzani. Tena hakakuishia hapo bali alimwita mgonjwa anayejinyea.... alivyorudi CCM hatukasikii tena kakibweka...

Yaani mtu anaonekana mchafu akitoka CCM...

Chadema pia ivo ivo tu. Mwita na Mollel mliwaitaje?

Hapa ndiyo ule msemo :usemao nyani haoni kundule ndiyo sehemu yake

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Chadema pia ivo ivo tu. Mwita na Mollel mliwaitaje?

Hapa ndiyo ule msemo :usemao nyani haoni kundule ndiyo sehemu yake

Sent from my iPhone using JamiiForums
Sio CDM wala CCM tu. Wanasiasa wote mwalimu wao mmoja
 
Walimwambia alipe kodi kama ambavyo wewe pia unaweza kuambiwa, lakini yeye akitaka afanye huo ufisadi, sasa kanuna, kwa maana hiyo ufisadi hautakiwi kwa sasa.
Ueleweki nani akuambie wakati sheria inataka hivyo, na kama alikuwa anaomba msamaha wa kodi ni haki yake ku-apply, kama hana vigezo anakataliwa na ni mambo ya utendaji na sio siasa, naomba mutenganishe kazi na siasa.
 
CCM wanajuana wanachofanya ni kutuvuruga wananchi, kwenye kuiba wanaiba pamoja wanakula pamoja ila wanakuja kuchenjiana kwenye maslahi binafsi sio ya nchi.!
 
Ueleweki nani akuambie wakati sheria inataka hivyo, na kama alikuwa anaomba msamaha wa kodi ni haki yake ku-apply, kama hana vigezo anakataliwa na ni mambo ya utendaji na sio siasa, naomba mutenganishe kazi na siasa.

Sasa kwa nni anune, kama tataka kusamehewa na wengine hawatatakiwa kulipa kodi itabidi wasamehewe, yeye alikuwa kiongozi hivyo ni wajibu aonyeshe mfano.
 
Back
Top Bottom