RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 59,486
- 135,391
Hakika hapa Jf kuna vichwa !
Jf's member anaesomeka kwa username Kyenju , ndiyo amenifanya niandike thrade hii.
Kyenju kupitia comment yake , humuhumu Jf amehoji kwamba Humphrey hadi saa 5 na ushee jana usiku , alikuwa chanel 10 kwenye kipindi (live) .
Binafsi mimi nilikua nakiangalia kipindi hicho .
Hoja muhimu ya Kyenju , anahoji tujiulize magazeti yanakua yamemakamilika kuchapishwa muda gani ?
Na tuanzie hapo :
Uzoefu unatuambia/tuonesha by saa 5 - 6 usiku magazeti hua tayari yashachapwa , na yaendayo mikoani hua tayari yako njiani .
Point muhimu hapa , ni saa ngapi Mr slowslow alifika home , na ni saa ngapi alivamiwa ? Saa ngapi polisi walifika kum'resque (kama ilivyoripotiwa gazetini)
Na ni muda gani habari zilifika chumba cha habari cha gazeti , zikahaririwa na kueditiwa ?
Na asubuhi zikaamka kwa walaji gazetini.
Ikumbukwe gazeti lililoripoti , ni gazeti lenye mahusiano na Uhuru/Daily news.
Wadau wangu hii makitu inaingia akilini ?
Tamthilia either !
Habari inasema USIKU WA KUAMKIA JANA.....una zaidi ya masaa 24 kutoka usiku wa kuamkia jana hadi leo hii.....tukio la usiku wa kuamkia jana lina siku nzima ya jana kuyafikia magazeti.....ingekuwa USIKU WA KUAMKIA LEO ndio hoja yako na wengine kwamba limewezaje kutoka kwenye gazeti la leo ingekuwa na mashiko.
Hata kama wanatengeneza 'sinema' hawawezi kuwa wajinga kiasi hiki....au mimi ndio sijui USIKU WA KUAMKIA JANA maana yake nini??!!