SI KWELI PreGE2025 Humphrey Polepole ameandika ujumbe huu akiimuunga mkono Rais Samia

SI KWELI PreGE2025 Humphrey Polepole ameandika ujumbe huu akiimuunga mkono Rais Samia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Polepole habarileo.jpg
Polepole Jambo TV.jpg
POlepole Sep 04 - Clouds.jpg
 
Tunachokijua
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.

Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram alichapisha barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba na baadaye tarehe 18, Julai 2025 alifanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alikosoa utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema 'Wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Mchakato wa kupata wagombea tumeukosea'

Agosti 05, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Madai

Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa Humphrey Polepole ameandika ujumbe katika mtandao wa X akiimuunga mkono Rais Samia Suluhu na kusema

"Baada ya kutafakari kwa kina na kufuatilia kwa makini kampeni zinazoendelea nimebaini kuwa Mgombea Urais wa Chama chetu Dkt. Samia Suluhu Hassan atakataa wahuni, atatuunganisha na kuhuisha demokrasia. Dkt. Samia atakula sahani moja na wahuni, hakuna atakayefurukuta kwasababu nia hiyo anayo na amepata msaidizi imara Dkt. Emmanuel Nchimbi"

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo



Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa ujumbe ulionukuliwa katika taarifa hiyo ni wa kughushi kwani hujaandikwa na Humphrey Polepole kwenye mtandao wa X.

Aidha Polepole hatumii mtandao wa X kama ujumbe huo unavyoonekanakuchapishwa katika mtandao huo. Rejea hapa.

Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kutengenezwa na wapotoshaji kwani hazijachapishwa na vyombo (Clouds Media, Jambo TV na Habari Leo) hivyo kama inavyoonekana.​
Back
Top Bottom