Humphrey ahukumiwe kifo in absentia

Humphrey ahukumiwe kifo in absentia

Utamlinganisha Castro na huyo ndugu yenu

Inaonesha watanganyika na wazanzibari wakienda Cuba, wakirejea nchini wote huwa wameiva kifikra na kimtizamo wakiwa tayari kuleta mguso katika mwelekeo wa siasa na aina mpya utawala wa nchi

Polepole naye historia imempeleka huko isipokuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro mheshimiwa Adam Ali Kighoma Malima aliyesomea chuo kikuu Cuba ni mtanzania pekee ambaye hakuingiwa na fikra za kimapinduzi za kina Castro, Che na Bolivar

SOMA :


SOMA :

 
Inaonesha watanganyika na wazanzibari wakienda Cuba, wakirejea nchini wote huwa wameiva kifikra na kimtizamo.

Polepole naye historia imempeleka huko isipokuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro mheshimiwa Adam Malima aliyesomea chuo kikuu Cuba ni mtanzania pekee ambaye hakuingiwa na fikra za kimapinduzi za kina Castro, Che na Bolivar

SOMA :

Adam Malima ambae anakula mema hapo Morogoro? Au mwingine?
 
Adam Malima ambae anakula mema hapo Morogoro? Au mwingine?

Huyu ndugu Adam Kighoma Malima itikadi ya mapinduzi iliimshinda pamoja ya kusoma miaka kadhaa ktk chuo kikuu nchini Cuba, amebaki kuwa bwanyenye

Mifano ya watu waliomkosha Julius Nyerere baada ya wao kurudi kutoka Cuba wakiwa wameiva kimapinduzi ni mingi na hivyo Nyerere kuwaamini kusambaza itikadi ya Comintern (International communism) ya kina Leon Trotsky iliyowaingia kina Castro, Ernesto Guevara CHE hadi kina Humphrey Polepole wa kizazi hiki :


Saturday, February 16, 2013

Comrade Mohammed Ali Foum

1681693130094.png

Picha : Balozi Mohammed Ali Foum

Mwanzoni mwa Mwezi huu Tanzania ilipata pigo zito mno lislopata mithilika, aliyekuwa Balozi wetu wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mzee Mohammed Ali Foum aliiaga Dunia Jijini Cairo Nchini Misri.

Balozi Foum (Juni 4, 1936 - Februari Mosi, 2013) ni Mzalendo wa kupigiwa mfano wa Tanzania ambaye aliitumikia Nchi hii, Afrika na Dunia kwa Ujumla kwa Moyo wake wote na Utumishi wa Kutukuka.

Aliteuliwa na Rais Nyerere kuwa Balozi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Mwaka 1984 na akajitambulisha Rasmi kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Javier Perez de Cuellar Tarehe Septemba 14, 1984 kama anavyoonekana Pichani katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Nchini Marekani.

Ufuatao ni Wasifu Mfupi wa Mema mengi yaliyotendwa na Balozi Mohammed Ali Foum hapa Duniani ambao nimeuhariri kidogo kutoka kwenye Wasifu wa awali ulioandikwa na Mwandishi Nguli na Gwiji, Bwana Amhed Rajab. Wasifu husika ulikuwa ni sehemu ya Tanzia ya Kifo chake ambao ulichapishwa katika Gazeti la 'Raia Mwema' tolea namba 281 la Mwezi huu.

MOHAMMED ALI FOUM: MZALENDO WA KINZANZIBARI NA MSIRI WA NYERERE.

KOMREDI WA KWELI.

Mohammed Ali Foum aliyefariki dunia jijini Cairo Ijumaa usiku, atakumbukwa kama mwanamapinduzi na shujaa aliyepigania "Uhuru wa Zanzibar" na kuchangia mengi katikaM juhudi za kulikomboa Bara la Afrika.

Wengi waliokuwa wakimfahamu juu juu, hawakuutambua mchango wake uliokuwa adhimu katika harakati za ukombozi wa Afrika. Hayo si ya ajabu kwa kuwa Foum hakuwa mtu wa kujionyesha na akipendelea kuuficha umahiri wake hasa katika nyanja ya diplomasia.

Nikimfahamu tangu kufungua kwangu macho kwani sote tulizaliwa Vuga, Mji Mkongwe, Unguja. Alikuwa ni mmoja miongoni mwa kaka zetu wa Vuga waliowashajiisha wadogo zao mtaani wawe na moyo wa kuwa pamoja.

Mwenzake mmoja katika hili, alikuwa Salim Hakim, ambaye sasa ni mmoja wa mabalozi wanaosifika wa Omani. Baadaye wote wawili walikuwa mabalozi katika Umoja wa Matifa, Foum akiiwakilisha Tanzania na Hakim akiiwakilisha Omani.

Katika miaka ya hivi karihuni wakawa tena pamoja wakiishughulikia Somalia. Foum alikuwa Mwakilishi wa Muungano wa Afrika, na Hakim alikuwa Mwakilishi wa Umoja wa Kiarabu (Arab League). Lakini huko utotoni waliwatia ari watoto wa Vuga waunde timu ya soka ya Young Brothers. Nakumbuka hao wawili na wenzao wa rika lao, walikuwa na tabia ya kuitana kwa kupiga mbinja au mluzi, kama wasemavyo Bara.

Tangu utotoni, Foum alikuwa si mtu wa kukaa nyuma, Daima akipenda kushirikiana na wenzake mtaani na pia skuli. Ingawa hakuwa pocho Foum aliamua kukatiza masomo yake ya sekondari na kuanza kufanya kazi katika Ofisi ya Leba ambako pia akifanya kazi Ahmed Diria Hassan. Baadaye Diria naye atakuja kuwa mmoja wa mabalozi madhubuti wa Tanzania.

Foum alianza kuzivaa siasa alipojiunga na chama cha Hizbu, yaani Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Chama hicho kilimpeleka Havana Cuba kwenda kufungua ile iliyokuwa ikiitwa Ofisi ya Zanzibar. Huko alikuwa pamoja na Kanali Ali Mahfoudh na Komredi Salim Ahmed Salim ambao alijiunga nao kwa muda mfupi. Nyumba yao mjini Havana, ambayo pia ilikuwa ni ofisi yao, ilikuwa katika eneo la Vedado ambako wakiishi Wacuba wa tabaka la kati. Sehemu moja ya nyumba hiyo ilikuwa ofisi ya chama cha ANC cha Afrika ya Kusini.

SOGELEA UKOMBOZI.

Foum na wenzake waliwasili Havana si muda mrefu baada ya Fidel Castro na Che Guevara kuuteka mji huo katika Mapinduzi yaliyomwondoa Fulgencio Batista madarakani. Tayari wakati huo Foum alikuwa amekwishaanza kuzikumbatia siasa za mrengo wa kushoto. Huko Cuba pia alikuwa akihudhuria mafunzo ya kijeshi yaliyokuwa yameandaliwa mahsusi kwa vijana Wakikomred kutoka Zanzibar, waliokuwa wakifunzwa namna ya kupindua Serikali.

Baadaye vijana hao pamoja na kina Foum, Ali Mahfoudh na Salim Ahmed walijiunga na chama cha Umma Party cha Abdulrahman Babu na kushiriki katika Mapinduzi ya 1964. Waandishi wa habari kutoka nje waliofika Zanzibar baada ya Mapinduzi na kuandika kwamba walikuwako Wacuba huko, walikuwa kwa hakika wakiwazungumza kina Foum na makomred wenzake waliorejea kutoka Cuba na waliokuwa wakizungumza Kispanyola.

Mwaka 1963 walipokuwa bado Havana, Foum na Ali Mahfoudh waliandika kijitabu kilichoitwa: ‘Forge Ahead To Emancipation’ (Songelea Ukombozi) kilichozungumzia vuguvugu la Zanzibar la kuupinga ubeberu.

Historia ya Umma Party, inaonyesha kwamba Ali Sultan Issa, Foum, Mahfoudh na Salim Rashid ndio waliokuwa wakimshadidia zaidi Babu wakiache mkono chama cha ZNP.

UGWIJI KATIKA DIPLOMASIA, UFASAHA WA MANENO KATIKA KURAI NA UAMINIFU KATIKA KUTUNZA SIRI.

Katika miezi ya mwanzo ya Mapinduzi, Foum alikuwa pamoja na Mahfoudh kwenye kambi ya kijeshi na baada ya kuundwa Muungano, akateuliwa awe mshauri (counselor) katika Ubalozi wa Tanzania, New York. Hapo ndipo Foum alipoanza kazi zake za kidiplomasia na kuanza kung’ara katika shughuli hizo. Rais Julius Nyerere alimteua awe Balozi wa Tanzania India, Italia na pia katika Umoja wa Mataifa. Foum aliwahi pia kuwa waziri mdogo wa mambo ya nje.

Nyerere akimuamini sana, na Foum alikuwa ni msiri wake mkubwa, na hasa kuhusu shughuli za kimataifa. Mara nyingi Mwalimu Nyerere alikuwa akimtuma kuonana na viongozi wa nchi nyingine alipokuwa ana mambo nyeti yaliomfanya awasiliane na viongozi hao. Yeye mwenyewe Foum, alikuwa na uhusiano na wanaharakati mbalimbali wa kimataifa.

MAFUNGAMANO NA MALCOLM X PAMOJA NA WAPIGANIA HAKI, USAWA NA UTU WENGINE.

Miaka michache iliyopita nilimpelekea baruapepe Amiri Baraka, Mshairi, Mwandishi na Mwanaharakati wa Kimarekani mwenye asili ya Kiafrika na nikamuuliza lini alikutana mwanzo na Babu. Baraka (ambaye zamani akijulikana kwa jina la LeRoi Jones) alinijibu: “Nilikutana naye Astoria Hotel, New York, mwaka 1964 wakati uleule nilipokutana mwanzo na Malcolm X”.

Wakati huo, Foum tayari alikuwa New York na alikuwa Mtanzania wa mwanzo kujuana na Malcom X na halafu akamjulisha kwa Babu aliyekuwa akidhuhuria kikao cha Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Gamba la albamu moja ya hotuba za Malcolm X lina picha ya Foum na Babu wakiwa pamoja naye Malcolm X. Ninajua kwamba Babu aliwahi kuiona albamu hiyo na gamba lake, lakini Foum hakuwahi kuiona.

Miaka miwili iliyopita tukiwa pamoja Nairobi alinishikiia nimtafutie gamba la albamu hilo. Moja ya masikitiko yangu ni kwamba sikujaaliwa kumtimizia haja yake. Usuhuba wa Foum na Malcolm X ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwafanya wawe wanatembeleana majumbani mwao. Mwengine aliyekuwa akimtembelea Foum nyumbani kwake New York alikuwa mwanamapinduzi wa Cuba Che Guevara. Kwa ujasiri wake na licha ya kujuwa kwamba akiandamwa na majasusi wa CIA wa Marekani Foum alikuwa akifuatana bila ya kificho na Malcolm X pamoja na Che.

FOUM, KIASHIRIA CHA UTU, HESHIMA NA SERA ILIYOTUKUKA YA MAMBO YA NJE YA TANZANIA.

Kwa hilo na pia kwa harakati zake za kupinga ukoloni na ubeberu Foum alikuwa heshi kuwakera Wamarekani. Aliwakera sana kwa msimamo wake imara wakati mijadala ya vikao vya Kamati ya 24 ya kuufyeka ukoloni duniani. Foum aliteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika kamati hiyo.

Mfano wa jinsi Wamarekani walivyokuwa wakimuona kuwa ni mkorofi ni telegramu moja kutoka ujumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa iliyopelekwa kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Telegramu hiyo iliandikwa Novemba 26, 1968, wakati Marekani ilipokuwa ikizingatia kujitoa kutoka kwenye Kamati ya 24.

Ilisema hivi: “Maazimio kama hayo yanatungwa hasa na Waafrika wenye siasa kali — kama Foum (Tanzania) wakisaidiwa na Masovieti na Waarabu wenye siasa kali kama Syria na Iraq”. Diplomasia kama ilikuwa katika damu yake na inaonyesha alimrithisha mdogo Abdillahi ambaye mwaka jana tu alistaafu akiwa balozi mdogo wa Sweden mjini Addis Ababa.

WATU WEMA HAWACHOKI KUWATUMIKIA WENZAO.

Yeye mwenyewe Foum aliendelea na shughuli za kidiplomasia hata baada ya kustaafu serikalini. Novemba 22, 2002, Amara Essy, Mwenyekiti wa muda wa wakati huo wa Muungano wa Afrika (AU), alimteua awe mjumbe wake maalum nchini Somalia. Foum alijipatia sifa kwa uchapaji kazi wake na kwa jitihada zake wakati wa Mkutano wa Somalia wa Kuleta Suluhu ya Kitaifa uliofanywa nchini Kenya toka Oktoba 2002 hadi Oktoba 2004.

Alikuwa mbioni pia wakati wa jitihada nyingine zilizochukuliwa baadaye na jumuiya ya kimataifa kujaribu kustawisha amani na kuleta suluhu nchini Somalia. Aliuacha wadhifa wa kuwa Mwakilishi Maalum wa Muungano wa Afrika kwa Somalia mnamo 2007 na mahala pake pakashikwa na Nicolas Bwakira kutoka Burundi.

Baadaye kama miaka miwili hivi iliyopita alichukuliwa kwa muda na Augustine Mahiga, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Somalia, awe mshauri wake. Aliiacha kazi hiyo mwaka jana akishughulika na biashara. Ujuzi wake wa siasa za Somalia na majungu ya wanasiasa Wakisomali ulikuwa wa kupigiwa mfano. Binafsi nilifaidika nao nilipokuja kuishi Nairobi na kusimamia mradi mmoja wa shirika la UNDP la Umoja wa Mataifa kuhusu kielelezo cha katiba mpya ya Somalia.

Alinishauri na kunielekeza wapi pa kupiga hodi ili kazi zangu kuhusu Somalia zifanikiwe. Wakati mwingine akinishauri hata bila kuomba ushauri wake. Huo ni mfano wa sifa nyingine aliyokuwa nayo — ya ukarimu na kutokuwa na uchoyo.

WEMA HAWADUMU ULIMWENGUNI, MOLA AMLAZE PEMA MCHAMUNGU MOHAMMED ALI FOUM.

Hizo zote ni sifa za mcha Mungu, na Foum alikuwa mtu wa aina hiyo kama marehemu baba yake, Inspekta Ali Foum.

Safari moja nikiwa Jeddah, Saudi Arabia, mfanyakazi mmoja katika Ubalozi mdogo wa Tanzania aliniambia kwa masikitiko: “Sijui Foum mzima kwa sababu haipiti mwezi hutokea hapa kuja kufanya umra Makkah. Mwezi huu sijamuona”.

Ama mimi sitomuona tena siku za Ijumaa katika Msikiti wa Hurlingham hapa Nairobi.

"Hakika sisi ni Miliki ya Mungu, na Hakika kwake tutarejea", Mola amlaze Pema Mja Mwema huyu
 
MUNGU alivyo fundi unaweza kufa Wewe ukamuacha au ukafiwa mtu wako wa karibu mke, mme, mtoto, mama ako au baba ako Mungu huwa ni fundi sana
 
Polepole nachoweza kumshauri kama hatapitia hapa naomba akiwa anafanya press arudi pale alipokuwa mwanzo mambo ya kuonyesha mazingira na view sehemu aliyopo sio nzuri tena anakua live arudie system yake ya zamani kukaa sehemu ambayo haionyeshi view yoyote itamsandia
 
Makomredi walioishi Cuba wana historia ya akili nyingi sana na muda wote walijisomea kuongeza maarifa.

Picha ikionesha Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania umoja wa mataifa balozi Salim Ahmed Salim mwaka 1970 akiwasilisha hati za utambulisho kwa katibu mkuu wa UN

1696127370764.png

balozi Salim Ahmed Salim (kulia) mwaka 1970 akikabidhi hati zake za utambulisho kwa katibu mkuu wa UN mwaka 1970. Picha kwa hisani ya tovuti : salimahmedsalim.com

Naye Salim Ahmed Salim pia aliishi Havana Cuba ....balozi Mohamed Ali Foum Foum anasimulia ktk shajara / diary zake kuwa alianza kuzivaa siasa alipojiunga na chama cha Hizbu, yaani Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Chama hicho kilimpeleka Havana Cuba kwenda kufungua ile iliyokuwa ikiitwa Ofisi ya Zanzibar. Huko alikuwa pamoja na Kanali Ali Mahfoudh na Komredi Salim Ahmed Salim ambao alijiunga nao kwa muda mfupi. Nyumba yao mjini Havana, Cuba ambayo pia ilikuwa ni ofisi yao, ilikuwa katika eneo la Vedado ambako wakiishi Wacuba wa tabaka la kati. Sehemu moja ya nyumba hiyo ilikuwa ofisi ya chama cha ANC cha Afrika ya Kusini.
 
Makomredi walioishi Cuba wana historia ya akili nyingi sana na muda wote walijisomea kuongeza maarifa.
2 December 2024
ULUMBI na DIPLOMASIA

Msharafu; Humphrey Herson Polepole @hpolepole ni mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Kitanzania anayehudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Cuba,

View: https://m.youtube.com/watch?v=7D3-hfkcdQ0

Nafasi ya ubalozi Cuba aliyoanza kushikilia tangu mwaka 2023. Kabla ya hapo, alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi kuanzia 2022 hadi 2023.

Polepole alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na pia mbunge wa kuteuliwa na Rais John Magufuli. Kabla ya uteuzi huo, Humphrey Polepole aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa kipindi cha miezi mitano na hapo awali alihudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Musoma kwa miezi miwili.
 
Ontario, Canada

MIGUNA MIGUNA UMUHIMU WA WANAOTAKA MADAILIKO / MAPINDUZI
SUNDAY LIVE| In Miguna's View [Part 2]

View:

Agusia vijana ni mota ya kuwasha injini ya mabadiliko katika jamii, na umuhimu wa vijana kukataa kuongozwa na viongozi waliofeli kuongoza nchi
Miguna Miguna atoa mifano ya kina Fidel Castro wa Cuba, Trotsky wa Russia, Mapinduzi ya Ufaransa kungoa utawala wa kifalme n.k

GenZ ya kina Castro ambao katika ujana wao 1958 waliongoza mabadiliko pale kulipotokea mkwamko wa kiuongozi wa taifa kukengeuka na kusahau madai ya umma kutaka mabadiliko kwa njia za maridhiano iwe ya kidemokrasia kupitia uchaguzi au watawala wenyewe kukataa kuongoza mabadiliko yanayodaiwa na umma


Kina Fidel Castro, Trotsky walibezwa na wazee kuwa wakingoa utawala nchi itakosa amani kwa kuwa vijana hawajui kuongoza taifa kama kina Bastista walioongoza kungangania madaraka kwa muda mrefu kupitia vyombo kandamizi vya dola n.k
 
Kumbuka hivi vitu kabla haujaamua chochote kuhusu raia wa Tanzania.
1. Hakuna mungu mtu, wala hakuna malaika mtu, kama una uwezo wa kula chakula kwa kukitafuna na baadaye kwenda chooni kutoa uchafu basi fahamu sote tupo sawa kwenye uso wa dunia. Unaweza kuwa na walinzi zaidi ya elfu moja ila hawawezi kumzuia malaika mtoa roho akija kuchukua cha mwenyezi Mungu.

2. Tanzania ni serikali ya kidemokrasia na haina maana kwamba ni lazima Kassim Majaliwa awe Waziri Mkuu ama Samia awe Rais, ila amepata nafasi ya kutuwakilisha ila haina maana kwamba anaongoza upeo ama akili kubwa nambari moja kuliko watu zaidi ya milioni 65, ni ujinga kudhania kuwa Samia ni Mtanzania nambari moja! Hayati Baba wa Taifa hakuwahi kujionesha kuwa yeye ni Mtanganyika nambari moja.

3. Moja ya sifa bora na njema sana ya Kiongozi bora ni kukubali kukosolewa. Ni kawaida kulala na kuamka ukiwa na matongotongo kwenye macho. Viongozi wenye akili hutumia nafasi ya wao kukosolewa ili kujifunza na kujirekebisha sio kujiona wao ni hawakosei!

4. Anachokifanya Polepole ni sawa na mahubiri ambayo yanayolewa kanisani ama hutuba msikitini halafu usikie Majini yakisema mahubiri hayo ni mabaya na inapaswa Kiongozi wa dini asiendelee kuongea. Polepole anatumia haki zake kama Katiba inavyosema, sio miongozo ya Samia wala CCM bali katiba.

NB: TAFUTA MUDA USOME MAANA YA UHAINI, NA MAKOSA YANAYOONEKANA KAMA NI UHAINI, SOMA KWA UTARATIBU KABSA UTAELEWA MAANA YAKE.
 
ni ujinga kudhania kuwa Samia ni Mtanzania nambari moja! Hayati Baba wa Taifa hakuwahi kujionesha kuwa yeye ni Mtanganyika nambari moja.

3. Moja ya sifa bora na njema sana ya Kiongozi bora ni kukubali kukosolewa

Wameziba masikio na kujikuza kupita Jamhuri / Republic na kujivika ufalme / umalkia wakidai ni Mungu ndiyo amewachagua na mbaya zaidi baadhi ya viongozi wa kiroho / imani nao wamehongwa kurudia wimbo ni Mungu ndiyo aliyemsimika kiongozi wa CCM kuwa rais
 
1. Kwanini Mheshimiwa asihukumiwe kifo in absentia? Siku akikamatwa ni utekelezaji tu ufanyike pale Uwanja wa Uhuru mchana peupe ili iwe fundisho kwa wote

2. Anatumia lugha ya kuudhi na uhaini. Adhabu yake NI KUNYONGWA HADI KUFA.
Na bado hajamaliza, hakuna pa mahala mtatokea ni nondo za kichwa hadi muombe poo!!
 
Ontario Canada

WATAWALA WAITEKA NYARA, SOVEREIGNTY NA JAMHURI


Miguna Miguna azungumzia kitu kinachoitwa sovereignty kinavyotumiwa vibaya na walio madarakani, kwa kupora haki ya msingi ya sovereignty waliyonayo raia wa nchi iliyo Jamhuri / Republic

| SUNDAY LIVE| In Miguna's View [Part 1]


View: https://m.youtube.com/watch?v=t_4VlmXY7l0
 
Back
Top Bottom