Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu.
[FONT=Arial, sans-serif]Mahakama ya Rufani Tanzania kesho itatoa hukumu kuhusu mgombea binafsi katika uchaguzi wa kisiasa dhidi ya rufaa iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Hukumu hiyo itatolewa baada ya mahakama hiyo kusikiliza marafiki wa mahakama ambao Aprili 8, mwaka huu walitofautiana kwa baadhi yao kuunga mkono upande wa Jamhuri na mwingine kuupinga.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Marafiki hao walioalikwa na Jaji Mkuu, Augostino Ramadhani, ni pamoja na Profesa Palamagamba Kabudi na Profesa Jwani Mwaikusa, ambao kitaaluma ni wanasheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Othman Masoud. Mwingine ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajabu [/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Kiravu.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Profesa Kabudi alikubaliana na Serikali kuwa mahakama haina mamlaka ya kurekebisha kifungu chochote cha katiba kauli ambayo iliungwa mkono na Masoud.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Hata hivyo, Profesa Mwaikusa alisema mahakama kwa mujibu wa mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili mitatu, ina mamlaka ya kutamka kifungu chochote kinachokwenda kinyume cha katiba.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Kwa upande wake, Kiravu, alisema umebakia muda mfupi kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu hivyo kama wagombea binafsi wataruhusiwa, hatua hiyo itaathiri maandalizi ya uchaguzi huo.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Walitoa maoni yao walipokuwa wakichangia hoja za mwisho kwa mahakama hiyo iliyokuwa imeketi chini ya jopo la majaji saba, wakiongozwa na Jaji Ramadhani, kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na serikali kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuruhusu mgombea binafsi.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Akizungumza na Nipashe, Wakili wa Mchungaji Mtikila, Riachard Rweyongeza, alisema kuwa amepokea hati ya kuitwa mahakamani kesho kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Kwa mujibu wa rufaa hiyo namba 45 ya mwaka jana, serikali iliwasilisha mahakamani hapo ikipinga hukumu ya iliyotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu, ambao ni Jaji Mstaafu Amir Manento, Salum Massati, Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa na Thomas Mihayo (Mstaafu), ambao walikubaliana na ombi na Mtikila na kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi nchini.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Katika rufaa hiyo, serikali imetoa sababu sita za kukata rufaa hiyo zikiwemo; Mahakama Kuu ilikosea kujipa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo; ilikosea kutengua vifungu vya Katiba ya nchi; na kukosea kisheria kwa kupunguza matakwa ya lazima ya Ibara 30(5) na 13(2) ya Katiba ya nchi.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Sababu nyingine ni kujipachika mamlaka ya kibunge ya kutunga sheria, kukosea kisheria kwa kuiweka Katiba ya nchi katika vyombo vya kimataifa na pia ilikosea kuitolea maamuzi kesi hiyo bila kuweka suala hilo bayana.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Mara ya kwanza, serikali ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika Mahakama hiyo ya Rufaa mwaka 2007, ambayo ilidai mahakama hiyo ya chini ilikosea kisheria kutafsiri Ibara ya 21(1) (c), 39 (1) (c) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Hata hivyo, rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kukubaliana na ombi la wakili wa Mtikila, Richard Rweyongeza kwamba, rufaa hiyo haina msingi na kwamba imejaa dosari za kisheria.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Awali katika hukumu ya Mahakama Kuu ilivyotolewa Mei, mwaka 2006, ililiruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu Katiba ya nchi inatoa haki hiyo. [/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Mahakama Kuu ilibainisha kuwa katiba inatamka wazi kuwa, kila mwananchi ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani. [/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Mapema Mwaka 1993, Mtikila alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, lakini licha ya uamuzi huo wa mahakama, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi hivyo alifungua kesi hiyo ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo alishinda tena. [/FONT]
CHANZO: NIPASHE
Tungoje Majibu ya [FONT=Arial, sans-serif] rufaa iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila. itakuwaje ?
[/FONT]