Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jun 15, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, hukumu kuhusu kesi ya kikatiba kuruhusu wagombea binafsi uchaguzi mkuu wa mwaka huu, itatolewa na Mahakama Kuu ya Rufani ya Tanzania, siku ya Alhamisi ya kesho kutwa siku.

  Swali ni jee hukumu hiyo, italeta kicheko kwa kuruhusu demokrasia ya kweli kwenye chaguzi zetu, au ni kuendeleza kilio cha uminywaji demokrasia kama hali ilivyo sasa?, haswa kwa kuzingatia, maandalizi ya uchaguzi kupitia vyama ndio hayo yamefikia top gear na bunge ambalo ndilo linatarajiwa kufuta vifungu husika na kupitisha sheria mpya ndilio hilo hilo limetengua kanuni zake zenyewe ili kuwa Bunge Haste Haste kuwahi mchakato wa uchaguzi?.

  Jee Jaji Mkuu, Agustino Ramadhani, with his Full Bench (Majaji Rufani 7!) kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, atafanya kile akipasacho kufanya na jina lake kuandikwa katika vitabu vya historia ya nchi hii?,

  ama naye atajiunga na ule msururu wa wapiga zumari, kutupigia nyimbo zile zile zilizoshachaguliwa na aliyemlipa mpiga zumari huyo kwa mujibu wa ule msemo maarufu wa
  "He who pays the piper, may call the tune".

  Huku tukiisubiria hiyo alhamisi, hakuna ubaya tuiijadili hukumu hiyo tarajiwa kwa mustakabali wa taifa letu.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa ndipo tunakapoona ile "Doctrine of the Independence of Judiciary" kama inafanya kazi au la kwa Tanzania! I can't wait to see this!
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Nimekua na kuamini kuna uhuru wa mahakama katika nchi hii. Sasa ndo tutajua ukweli. Sitarajii kuona another episodes on air in the new season ya mambo katika nchi hii.
   
 4. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  tusubiri mahakama itoe uamuzi wake......
   
 5. T

  Thomas David Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mahakama kuu ilishatoa hukumu, bali hii verdict ni ya Mahakama ya Rufaa.

  Rekebisho kwa mleta mada.

  Thomas
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Naamini Jaji Mkuu hatawaangusha watanzania! Yeye pia anajua madhara ya kutoa hukumu ya 'hovyo hovyo' kwenye suala hili. Wagombea binafsi 'on your marks', 'get ready'......!!!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ukishaona wameitwa wale marafiki wa mahakama kutoka pale Mlimani akina Prof Palamagamba, Dr Jwan Mwaikusa,.....ujue ushindi ni wa SERIKALI. Hili la mgombea binafsi hata mimi kama raia wa kawaida kabisa siliafiki kwa sasa. Vinginevyo tujiandae kuwa na marais kama Manji, RA, Lowasa, Mengi, Bakhresa, Rage,Mtikila, ......
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi mkubwa -- CJ Ramadhani hawezi kuweka alama yake katika historia ya nchi hii. Ni mtu wao.

  Hebu fikiri kidogo: kabla ya kuwa CJ, huyu alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya hapa Bara (NEC) na pia makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Visiwani (ZEC). Sasa tuchukulie ule wadhifa aliokuwa nao katika ZEC katika chaguzi zote za kule (1995, 2000 nq 2005). yale madudu yote ya ZEC ya kuminya taratibu za uchaguzi, kuwapora washindi halisi wa uchaguzi, uchukuliwaji wa masanduku ya kura na vikosi vya serikali ya ZMC at gunpoint (uchaguzi wa 2000) na uchafu mwingine mwingi uliofanyika yeye aliuafiki kabisa. Fikiria pia mauaji ya january 2001 kule Pemba yaliyotokana na maamuzi ya hovyo ya ZEC! Lazioma alibeba sehemu ya lawama!

  Kama hakuwa anashirikishwa katika maamuzi yale ya ZEC basi na atuambie.

  Sasa leo hii tutegemee auangushe utawala wa CCM? Hell NO!

  Nionavyo mimi, sana sana uamuzi utakuwa kwamba mudani mdogo kwa uchaguzi wa mwaka huu kuwa na wagombea binafsi, kwa hivyo baada ya uchaguzi, serikali iandale utaratibu wa kuwapo wagombea binafsi kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

  Hapo JK na kundi lake watakuwa wamepeta kiurahisi October kwa msaada wa CJ Ramadhani.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Zak Malang, hii picha uliyoiona hata nami binafsi naiona picha kama hii, kuwa uamuzi ule wa Mahakama Kuu ulikuwa sahihi, ila kwa vile maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yameisha kamilika, suala la mgombea binafsi liandaliwe lakini kwa ajili ya 2015!.

  Nadhani jamaa walishaamua maamuzi mazito, hii chelewa chelewa toka siku zile mpaka leo, ni kuyapitisha maamuzi hayo huku na kule, hatimaye CJ ametiwa siagi na kulainika, ndio maana amechelewa kutoa uamuzi kwa kujivuta vuta, ili angalau wapigania demokrasia ya kweli, wamwelewa kuwa muda uliobakia ni mdogo.

  Hii ndio nafasi pekee, the great opportunity kwa Jaji Ramadhani kusimama ahesabiwe na kuacha his mark kwenye justice pillars za nchi yetu. Nyalali (RIP), ameacha mark kwenye Tume ya Nyalali, hii sasa ndio nafasi ya CJ Agustino Ramadhani kuacha dole gumba lake, vingenevyo siku zijazo atajaishia kukumbukwa zaidi kama mpiga kinanda bora zaidi alikipiga kwa miaka mingi zaidi pale kanisani St. Alban.

  Na tusubiri mlio wa zumari, ataleta wimbo mpya au wa yule aliyemlipa?. Jibu ni Alhamisi!.
   
 10. T

  Thomas David Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alhamisi ni siku ambayo itakumbukwa katika historia ya Tanzania kwa mambo mawili:

  1. Tanzania tuna Mahakama huru yenye kulinda maslahi ya nchi na watu wake

  2. Ama kinyume chake

  Wito kwa Chief Justice Ramadhani

  Do what is right and do it right!

  JK hawezi kukutimua! Hana mamlaka hayo kikatiba.

  Mwisho: Kesho kutwa itakuwa siku ambayo watanzania wataihukumu makama ya rufaa.

  Hukumu hiyo tuisubiri

  Thomas
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,642
  Likes Received: 4,747
  Trophy Points: 280
  Kuwepo kwa mgombea binafsi ni faida kubwa kwa siasa za nchi yetu, tatizo watu wengi wanaliangalia kwa nafasi ya urais zaidi. Faida ninayoiona mimi ni kupanua wigowa demokrasia kwa wanasiasa wetu. Tunakumbuka wote yaliyowakuta wabunge 43 wa CCM wakiongozwa na Thomas Nyimbo, walisimama kidete kuihami NBC na TANESCO dhidi ya makaburu,lakini mwanyekiti wao wa chama wakati huo Benjamin Mkapa aliwasambaratisha kwa kuwatishia kuwanyanganya kadi za ccm nao wakanywea, laiti kingekuwepo kipengele cha mgombea binafsi wangeweza kusimama veme katika nafasi zao za kuwakilisha wapiga kura wao badala ya kutumiwa ka muhuri kulita chama cha na serekali yake.Kuwepo mgombea binafsi ni ukombozi kwa watanzania kuweza kupata uwakilishi sahihi na kupata wabunge wanaoweza kulitetea Taifa dhidi ya watawala mafisadi kama waliopo madarakani hivi sasa.
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  In a society of lawlessness mnategemea kutendeka haki kweli??? Mie nishakata tamaa na nchi hii sitoshangaa na uamuzi wa ajabu alhamisi na wala sijisumbui maana ni bure
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Buchanan, hii "Doctrine of the Independence of Judiciary" hapa Tanzania ipo na tumeishuhudia mara nyingi tuu ikifanya kazi, utata labda upo kwenye "Principle of Separation of Powers" kati ya mihimili hii mitatu ya Dola, Bunge, Serikali na Mahakama, wakati Mahakama inakubali kazi ya kutunga sheria ni kazi ya Bunge, Mahakama ni kutafsiri sheria hizo na serikali ni mtekelezaji wa sheria hizo. Kuna wakati serikali kupitia Ewura, iliingilia uwezo wa mahakama wakaifungia petrol station ya TIOT pale Morogoro, Mahakama ikaifungulia, Spika Sita akamaind, akailaumu mahakama na kiita imepotoka, CJ akamjibu kuwa ameteleza ulimi, Spika kawa mbogo akaliambia Bunge, hatuwezi kuiacha mahakama ikijifanyia inavyotaka. (Hapa waliingilia uhuru wa Mahakama) huku spika akidai hizo ndicho checks and balance.

  Katika kesi ya msingi, Mahakama Kuu, imetamka kuwa kifungu cha sheria kilichotungwa cha Bunge kulazimisha lazima wapitie vyama, ni kifungu batili, hivyo kuamrisha kiwe scraped off toka kwenye katiba na kuamuru serikali ilete vifungu halali.

  Serikali imekata rufaa sio kupinga kupinga amri ya Mahakama Kuu kutoa humu ile, bali inachallenge uwezo wa Mahakama Kuu, (jurisdiction), kuamua ilichoamua.

  Hivyo hukumu hiyo ya Rufani, ni muhimu sana sio tuu kwa ajili ya kuruhuru wagombea binafsi, bali umuhimu wake zaidi ni kuhusu Mamlaka ya Mahakama Kuu, ambayo yameainishwa kwenye katiba kuwa ina mamlaka yote (inherent jurisdiction), lakini katiba hiyo hiyo inataja uwepo wa Mahakama ya Katiba kushughulikia kesi zote za kikatiba, 'a court that has never existed', hivyo uamuzi wa Mahakama Kuu, unatafsiriwa kama kuingilia kazi ya Bunge kutunga sheria, hivyo hukumu hiyo ni uthibitisho wa nani zaidi kati ya mtunga sheria, aliyetunga sheria mbofu mbofu inayokwenda kinyume cha katiba ya nchi, ama mtafsiri sheria, mwenye mamlaka ya kusema sheria ipi, ina maana gani, na kama mtunga sheria akileta sheria mbofu mbofu, mtafsiri ana uwezo wa kuzifulia mbali na kuzitupa ....

  Serikali inashikilia, eti Mahakama Kuu ingeishia kuishauri tuu serikali na sio kuiamuru, yaani ikiombwa kuendeleza kubembelezana hata kwenye issue za haki za msingi za binadamu.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndio ukisikia a society of lawlessness. Sheria zipo kwenye madaftari no one respects them
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  .
  Mdondoaji, kukata tamaa ni udhaifu!, ili pia udhaifu ni sehemu ya maisha au choice of life, kwa wengine kuamua kuitumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutochagua chochote, kutofanya chochote, kutojishughulisha na chochote to make things right, simply because, kuna wengine watafanya yote yawapasayo kufanya kwa ajili ya nchi yao, ili na nyinyi wengine mliojikatia tamaa, muendelee kuishi kwa amani na utulivu.
  ule msema wa kila mtu ajiulize anaifanyia nini nchi yake,hauna maana sana.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kaka mie sijakata tamaa naisubiria kwa hamu hukumu hiyo ila nahisi sijui kama itakuja. Mie nachokisema ni hali halisi ya Tanzania ya leo hakuna utawala wa sheria kabisa mambo yanijiendea endea tu
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  You could be right Zak, lakini there is one glimmer of hope in CJ Ramadhani. Pamoja na 'madudu' unayosema aliyafanya kule ZEC, lakini nafikiri yalitokana na kuwa overwhelmed na makamishna wenzie. Nasema hivi kwa sababu huyu huyu Ramadhani aliwahi kutamka, katika kipindi cha pili cha awamu ya Mkapa kwamba yeye binafsi haamini iwapo NEC ni huru kutokana na composition yake. Aliyatamka hayo katika kongamano moja la masuala ya demokrasia (sikumbuki sawasawa ni lipi hilo) na akatilia mkazo kwamba hayo yalikuwa maoni yake binafsi.

  Hata hivyo suali ni kwamba: Kwa nini aliendelea kukitumikia chombo ambacho yeye binafsi hakiamini uhuru wake?
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tehetehetehe Tanzania bana kama alikuwa haamini kuwa NEC haiko huru kwani aliendelea kukaa kwani asingeliquit??? Halafu mnaexpect afanye la maana Alhamisi sijui pengine maana binaadamu hubadilika
   
 19. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Punda ni yule yule tafauti ni masoji tu ,msije mkapigwa na Butwaa siku ya alhamis.
   
 20. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nina imani na mahakama kuu ya rufani Tanzania!

  Hatima ya kesi hii ni ama mahakama iwape watanzania haki yao au mahakama fasiri vema sheria mbovu inayowanyima wananchi haki zao, iwanyeme haki! Tuombe Mungu watupe haki yetu!
   
Loading...