Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Ikumbukwe kuwa msingi mzima wa kesi ni kuwa Lema alimdhalilisha Batilda Burian katika mojawapo ya mikutano ya kampeni. Kwamba, kuna maneno aliyasema ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji. Sasa hilo ni jambo linalowezakujadiliwa. Wale ambao mmesikiliza hukumu maswali yafuatayo yamejibiwa vipi. Binafsi sijaweza kuchukua msimamo wa hukumu yenyewe bila kuisoma vizuri na kuelewa reasoning ya jaji:
a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?
b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?
c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?