Hukumu ya kesi ya ndoa inakaribia kusomwa, anataka tugawane mali wakati alinikuta nimesimama. Sitaki hilo litokee, nachanganyikiwa

Amenikuta nina mali zangu tayar na pia hata baadaye ununuzi wa viwanja ilikuwa ni kwa cash yangu bila kuomba sent ya mshahara wake kwenye ajira yake
Kwa sheria ya ndoa dada hawezi kuondoka na chochote ambacho ulinunua wewe kabla ya ndoa yenu. Kwa vitu vilivyochumwa ndani ya ndoa haina budi kugawana ila pia si lazima mgawane pasu kwa pasu. Endapo ukipata wakili mzuri atakayeionyesha mahakama kuwa Kwa asilimia kubwa ni wewe ndio ulisimamia show, hawezi kupewa 50% maybe 30 or 20% .

Ila zaidi msihi Mungu upate haki yako. Usiroge mtu kaka, Mungu aliyekupa nguvu na maarifa ya kutafuta kipindi kile atakuwezesha tena
 
Asipokufunulia mapaja mbona unapeleka kesi hadi kwa wazee, kijana unapaswa uelewe hayo yote yalifanyika na ukapata utulivu wa kutafuta hizo mali ndio point ilipo hapo, kuoa maana yake ni kutafuta utulivu wa mwili na nafsi.... tatizo mnaendeshwa na hisia mnasahau uhalisia.
Huko kwa Wazee mnaenda gawana mali?? , Kwamba watu ambao hawajaoa hawawez pata mali kwasababu hawafunuliwi mapaja hivyo hawana utulivu ??
 
Tupe mrejesho tarehe 8 imepita
Kuna habari niliona humu kua kuna mwanaume kajiuwa baada ya hukumu ya Mahakama kutoka kua mali zigawiwe pasu kwa pasu na mkeo! Sijui kama itakua same story au is just a coincidence!!
 
Pole Sana
Sasa Hujaeleza Kwa Undani Endapo Ulichuma Mali Yako, Mke Hataweza Kupewa Kitu Asichochuma Nawe Mkiwa Pamoja
 
Asipokufunulia mapaja mbona unapeleka kesi hadi kwa wazee, kijana unapaswa uelewe hayo yote yalifanyika na ukapata utulivu wa kutafuta hizo mali ndio point ilipo hapo, kuoa maana yake ni kutafuta utulivu wa mwili na nafsi.... tatizo mnaendeshwa na hisia mnasahau uhalisia.
Basi sheria ngumu sana et
 
Nahisi kuchanganya sana, hukumu tar 8 mwezi huu, shida yangu sio kuachana naye au kwamba siwezi maisha bila yeye bali naumia sana swala kugawana mali kichwa inawaka moto na katika ukweli amenikuta tayari nina maisha yangu, nyumba viwanja na mengine ila leo hii anataka mgawanyo.

Naamini kabisa ikiwa kitatokea hivi basi uchumi wangu utashuka na kuyumba kwa zaidi ya 70%, ni kama kuanza upya maisha, mipango yangu itakwama ghafla.

Inaniuma.. inaniuma.. inaniuma! Umri wangu ni kijana ambaye nimejitafuta na nikajipata kwa sehemu fulani. Alhamduallah.

Kuuuza mali akili haijawa tayari kuyapokea haya, sipo tayari kwa namna yoyote. Nasubir Mungu anitendee haki kama kweli yupo hata ruhusu haya na akiruhusu haya yatokee inaweza kuwa ndio mwanzo na mwisho wa kusali au kutoa sadaka, mwanzo na mwisho wangu kuabudu, haiwezekani.

Najua wapo wataonitukana kama ambavyo imekuwa kawaida, namwachia Mungu, huenda mimi sio haki yangu hata kuishi ila wao wanayo.

Mwanamke mmoja anaweza anaweza sababisha ukachukia wote.

We Mungu weeeeee, siku zinavyoenda afya yangu inazirota naiona kabisa, mvi zinadizi kuongezeka kwa stress, mambo yangu na miradi inasimama, ufanisi hakuna tena.

Jina langu pia ni kubwa sana kibiashara mkoa nilipo katika umri huu wa miaka 34 lakini huenda anguko likawa kubwa kuliko chochote ambacho nimewahi shuhudia kikianguka.

Tuombeane amani. Nimejikuta nakumbana na maadui wengi ambao sikuwahi hata kuwakosea. Leo wanashangilia na kumtakia mema mwanamke apate anachotaka!

Nahitaji msaada sana kuliko fedhea, lawama au vicheko.
Mkuu Acha akili ya kipumbavu kuwa mkigawana Mali ndiyo mwisho wako wa kuabudu na kutoa sadaka. Uoni kama una mdhihaki aliyekupa. Chamsingi hukumu ikitoka kubaliana nayo tu. Then muombe Mungu akupe nguvu ya kurejesho kile kilichotoka. Na kama watachukua yote pia omba na Mungu atakuzidishia mara Mia ya hiyo muhimu husikate tamaa.
 
Back
Top Bottom