Hukumu ya kesi ya ndoa inakaribia kusomwa, anataka tugawane mali wakati alinikuta nimesimama. Sitaki hilo litokee, nachanganyikiwa

Andika jina la mama yako
Ukitaka kuuza inakuaje? Mama alifariki Je? Mwisho ukiandika jina la mama na ana ugomvi na baba lazima atamwambia mwanamke wako.

Kuandika majina ya Wazazi ni sawa ila waandike na wosia kabisa kwamba hizi Mali nampa Fulani vinginevyo hutoweza kuziuza na itokee ndugu wengine wamezijua si utazifanya ziwe za familia Sasa? 😆😆
 
Bora Mimi wa mama wa nyumbani ,tukigawana nahakikisha napata walau 60-70% nakuwa willing ku loose ila hao wenye salary kazi mnayo 😂😂😂😂
Mkuu,

Nimeshangaa sana watu wanavyoandika hapa. Kwamba hatujui ni. Nini chanzo cha ndoa kutaka kuvunjika na kugawana mali, Lakini mwanaume anaonekana kuchanganyikiwa! Kwamba huyo mwanamke alikuwa ni mfanyakazi tu wa ndani au ni Mke halali?

Kama alikutwa na mali zake hawawezi kugawana sawa mwanamke anaweza kuchukua 30% iliyobaki akachukua mwanaume,

sasa kinachomchanganya ni nini? Alitaka baada ya kushindwana na mapenzi kuisha yule mwanamke aondoke vile vile kama alivyokuja?

utaona jinsi gani kuna roho mbaya hapa.
Ukweli ni kwamba lazima wagawane mali Lakini kama alimkuta na mali zake hilo suala la pasu kwa pasu halipo.
 
Mgawanyo wa mali wakati wa talaka huzingatia contribution ya kila mmoja kwenye upatikanaji wa mali hiyo. Hilo ni suala la ushahidi. Hatujui ni kwa namna gani uliweza ku-prove hilo mahakamani.

Lakini kwa misingi ya haki, zile mali ulizochuma wewe mwenyewe kabla ya ndoa yenu hazipaswi hukusishwa kwenye mgawanyo maana hizo si mali zilizochumwa na wanandoa kwa pamoja (unless wakati wa uchumba wenu alikuwa tayari anachangia).

Ndoa huwa haitengenezi joint ownership ya mali, isipokuwa tu kama wanandoa mmeamua iwe hivyo. Ndoa inatengeneza kitu kinaitwa common ownership ambapo kila mwanandoa anakuwa na share kwenye mali husika. Kiasi cha hiyo share kinategemea na mchango wake kwenye upatikanaji wa mali hiyo. Zingatia hapa kuwa mchango wake si lazima uwe wa pesa, zile huduma alikuwa anatoa nyumbani kama mke/mama ni mchango tosha na una-reflect kwenye umiliki wa mali iliyopatikana wakati wa maisha ya ndoa.

Sheria inaruhusu katika ndoa, kila mwanandoa kumiliki mali yake kwa jina lake. Swali hapa ni je mali zenu zipo kwa majina ya pamoja au la mmoja wenu?, kama zipo kwa jina lako kwa mfano ulipaswa kuwa na kazi kubwa ya kuthibitisha kuwa mli-intend kila mtu amiliki mali yake, kitu ambacho kama huna ushahidi madhubuti, ni ngumu ku-prove.

Cha muhimu ni kuwa piga moyo konde, huo si mwisho wa maisha. Mali hatuzaliwi nazo bali tunazitafuta. Haki inataka nae asiondoke mikono mitupu. Natumaini mahakama itampa anachostahili kwa haki. Nafasi ya kukata rufaa utakuwa nayo ikiwa hutaridhika na mgawanyo utakaotolewa.

Mwisho kwa ushauri tu, ukianza upya, fungua kampuni, hamisha umiliki wa mali zako muhimu kwenye kampuni kabla hujaanza maisha na mwanamke mwingine ili yasije yakakukuta haya tena baadae.

Pole sana na usikate tamaa..
 
Mkuu,

Nimeshangaa sana watu wanavyoandika hapa. Kwamba hatujui ni. Nini chanzo cha ndoa kutaka kuvunjika na kugawana mali, Lakini mwanaume anaonekana kuchanganyikiwa! Kwamba huyo mwanamke alikuwa ni mfanyakazi tu wa ndani au ni Mke halali?

Kama alikutwa na mali zake hawawezi kugawana sawa mwanamke anaweza kuchukua 30% iliyobaki akachukua mwanaume,

sasa kinachomchanganya ni nini? Alitaka baada ya kushindwana na mapenzi kuisha yule mwanamke aondoke vile vile kama alivyokuja?

utaona jinsi gani kuna roho mbaya hapa.
Ukweli ni kwamba lazima wagawane mali Lakini kama alimkuta na mali zake hilo suala la pasu kwa pasu halipo.
Mjinga tuu huyo,unapoingia kwenye Ndoa lazima utarajie hayo Sasa shida Iko wapi?

Nimeona wengi tuu wamegawana Kwa utaratibu huo ,ila kudhani mwanamke atatoka Kapa haitokaa itokee na kama hajui hayo basi ajiandae Kufa na kupooza 😂😂
 
Nahisi kuchanganya sana, hukumu tar 8 mwezi huu, shida yangu sio kuachana naye au kwamba siwezi maisha bila yeye bali naumia sana swala kugawana mali kichwa inawaka moto na katika ukweli amenikuta tayari nina maisha yangu, nyumba viwanja na mengine ila leo hii anataka mgawanyo.

Naamini kabisa ikiwa kitatokea hivi basi uchumi wangu utashuka na kuyumba kwa zaidi ya 70%, ni kama kuanza upya maisha, mipango yangu itakwama ghafla.

Inaniuma.. inaniuma.. inaniuma! Umri wangu ni kijana ambaye nimejitafuta na nikajipata kwa sehemu fulani. Alhamduallah.

Kuuuza mali akili haijawa tayari kuyapokea haya, sipo tayari kwa namna yoyote. Nasubir Mungu anitendee haki kama kweli yupo hata ruhusu haya na akiruhusu haya yatokee inaweza kuwa ndio mwanzo na mwisho wa kusali au kutoa sadaka, mwanzo na mwisho wangu kuabudu, haiwezekani.

Najua wapo wataonitukana kama ambavyo imekuwa kawaida, namwachia Mungu, huenda mimi sio haki yangu hata kuishi ila wao wanayo.

Mwanamke mmoja anaweza anaweza sababisha ukachukia wote.

We Mungu weeeeee, siku zinavyoenda afya yangu inazirota naiona kabisa, mvi zinadizi kuongezeka kwa stress, mambo yangu na miradi inasimama, ufanisi hakuna tena.

Jina langu pia ni kubwa sana kibiashara mkoa nilipo katika umri huu wa miaka 34 lakini huenda anguko likawa kubwa kuliko chochote ambacho nimewahi shuhudia kikianguka.

Tuombeane amani. Nimejikuta nakumbana na maadui wengi ambao sikuwahi hata kuwakosea. Leo wanashangilia na kumtakia mema mwanamke apate anachotaka!

Nahitaji msaada sana kuliko fedhea, lawama au vicheko.
Tangu mwanzo wa kesi ungeweka mwanasheria wa kukusimamia lakini pia sio shida, document ya hivyo vitu si unazo na zinaonesha tarehe kwamba ulinunua lini, assets zote zenye majina na tarehe kabala ya ndoa yako sidhani kama zinamuhusu
 
"Nasubir Mungu anitendee haki kama kweli yupo hata ruhusu haya na akiruhusu haya yatokee inaweza kuwa ndio mwanzo na mwisho wa kusali au kutoa sadaka, mwanzo na mwisho wangu kuabudu, haiwezekani"

Kwa akili hii lazima ndoa ikushinde, kwa akili hii hata hukumu italushinda, kwamba unamtishia Mungu na tusadaka twako, na kwenda kumwabudu kama rushwa, ngona afyeke uto tu hela kote ndo utaelewa kwamba hazihakiwi.
🤣🤣🤣🤣😁😁😁😁😆😆😆😂😂😂😂
 
Lazima Mali zigawanywe pasu pasu, si ulikua unalala naye? Ule utamu uliopata Ni sh ngapi?
Halafu siku hizi Sheria inamtetea Sana mtoto wa kike na watendaji wengi mahakamani Ni wanawake.
Kwani kulala naye raha naye alikua hapati??
Au hujui kisaikolojia mwanamke hupata raha ya tendo kuliko mwanaume??
Pia ni nani aliyekua akihudumu familia kiminajili ya uchumi??
 
Hizo ni taratibu za mtaani kaka. Talaka za mtaani hazitambuliki kisheria. Unaanzia BAKWATA ,then mahakamani. Mahakamani kesi inaanza upya, haijalishi wewe ni mkristo au muislam
Hiyo ni kwa taratibu ya kiislam.
Na BAKWATA ndio wanatumia sheria hiyo ya wao kukupa go ahead uende mbele kama mahakamani au kama mtamalizana hapo hapo BAKWATA.
Usinibishie kaka hii ndoa yangu ya sasa ni ya tatu nishaacha wake wawili.
 
Ushauri: Tafuta mwanasheria nguli, hukumu ikitoka cha kwanza kata rufaa, cha pili weka zuio la kisheria kutekelezwa hukumu, kisha andaa vielelezo vinavyoonyesha mali zilipatikana kipindi gani?. Risiti na mikataba ya manunuzi nk mkabidhi mwanasheria
Haya ya kutafuta vielelezo n.k alipaswa kuyafanya huko kesi ilipo. Mahakama inaposikiliza rufaa haipokei ushahidi mpya ambao haukutolewa kwenye mahakama ya chini.
 
S
Kwani kulala naye raha naye alikua hapati??
Au hujui kisaikolojia mwanamke hupata raha ya tendo kuliko mwanaume??
Pia ni nani aliyekua akihudumu familia kiminajili ya uchumi??
Uluhisho la huyu mwathirika Ni kukaa mezani na mwenza wake waachane na talaka, warudiane maisha yaendelee. Vinginevyo mwanamke atafaidika zaidi wakiachana especially kama huyo mmama anajua Mali zote za jammaa na zilipo.
Kama mwanamke Ni mchaga au mpare jamaa aanze kuhesabu maumivu.
Jamaa ameyagusa lazima yamnuke.
 
Ukimtafuta wakili mwenye weledi na ikafuatwa historia ya mali chanzo chake na vikatizamwa vile ambavyo wamechuma pamoja mahakama ya familia itaamuru vigawiwe vile ambavyo vilipatikana mkiwa wote sio alivyokukuta navyo.
Chang'ombe Temeke kuna Family court pale kama jamaa yupo Dar es salaam aende atashinda mchana kweupeee.
Pia ile mahakama inatizama sababu ya kuachana nini chanzo nini cha kuachana,kama ikigundulika utata wa mwanamke aisee mwanamke anaweza akaondoka kapa.
 
Hiyo ni kwa taratibu ya kiislam.
Na BAKWATA ndio wanatumia sheria hiyo ya wao kukupa go ahead uende mbele kama mahakamani au kama mtamalizana hapo hapo BAKWATA.
Usinibishie kaka hii ndoa yangu ya sasa ni ya tatu nishaacha wake wawili.
Nikubishie sababu gani. Bakwata hawana mamlaka ya kuvunja ndoa. Hao wake zako wangeamua kwenda mahakamani, sakata lingeanza upya. Acheni kuachana kienyeji. Mimi mwenyewe nilienda huko ,wao kazi yao ni usuluhishi tu
 
Bakwata ni moja ya chombo cha serikali ama laah??!!
Ukioa kiislam vyeti vya ndoa vinatoka BAKWATA ama havitoki??
Ukienda mahakamani ukipeleka cheti cha ndoa kama wewe muislam unatumia cheti gani kama sio kile ulichopewa Bakwata??
Bakwata inayo mamlaka ya kuvunja ndoa kulingana na sababu za ugomvi wa kutaka kuivunja ndoa.
Na kama ni suala la mali ninyi muelewane je mnayamaliza pale pale ama mnafikishana mpaka mahakamani.
Unaposema umeenda na mimi nimeenda huko huko na nikafuata taratibu hizo nazokueleza hapa acha ubishi wa kitoto.
Yani BAKWATA cheti cha ndoa kiwe valid halafu kuvunja ndoa kwao iwe invalid???
Inaingia akilini hiyooo??
 
Hawana mamlaka kisheria kuvunja ndoa, wao ni washauri na wasuluhishi. Tena siku hizi vyeti vya sijui BAKWATA havitakiwi. Kuna wakala wa kila dini waliosqjiliwa kwa ajli ya kufungisha ndoa na wanatumia vyeti vya serikali
 
T

Hata mimi nilianzia BAKWATA, labda hao BAKWATA nao wamevunja hiyo ndoa kihuni. Huwezi peleka sijui hiyo hukumu yako RITA na ukasajiliwa na kupewa cheti cha talaka. Acha ubishi, kubali tu umevunja kienyeji. Ipo siku utakutana na kiboko yako na atakupeleka mahakamani.
 
Nenda kapate elimu zaidi.
Hivi unajua mie kugawana na mkewangu wa mwanzo mali nilienda mahakama ya familia??
Na unajua niliambiwa nitoe vielelezo vya talaka kutoka BAKWATA??
Ona unavyojichanganya wakala wa dini ya kiislam ni BAKWATA.
Ukioa cheti kinatoka kwao kikiwa na sehemu ya picha kesha unaenda RITA kuhakiki hiko cheti cha ndoa.
Rudi kaulize tena narudia rudi kaulize tena.
Maana hata ukienda mahakamani utaulizwa mumeachana kwa misingi ipi kama mie nilivyoulizwa mahakama ya familia na mirathi Chang'ombe Dar es salaam ,nikatoa nyaraka za BAKWATA hatua zingine zikafuatwa.
 
T

Hata mimi nilianzia BAKWATA, labda hao BAKWATA nao wamevunja hiyo ndoa kihuni. Huwezi peleka sijui hiyo hukumu yako RITA na ukasajiliwa na kupewa cheti cha talaka. Acha ubishi, kubali tu umevunja kienyeji. Ipo siku utakutana na kiboko yako na atakupeleka mahakamani.
Asa unaniambiaje mbishi ilhali mahakamani nimefika??
Mbona unachekesha we jamaa??
Nimefika mahakama ya familia na mirathi Chang'ombe na kumaliza process zilizobaki.
Utasemaje BAKWATA kazi yake usuluhishi tu???
BAKWATA imeundwa kusimamia misingi na kanuni za uislam.
Hivyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitambua hiyo BAKWATA.
Waislam tuna taratibu zetu za kuachana ambazo BAKWATA watasimamia na unaweza ukaendelea mbele na safari ingine kwa waraka wao.
 
Back
Top Bottom