Hukumu ya kesi ya mauaji ya George Floyd kutolewa leo

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Hukumu ya kesi ya mauaji ya George Floyd inatarajiwa kutolea leo mchana jijini Minneapolis.

Derek Chauvin ambae alikuwa askari polisi tayari amepatikana na hatia ya mauaji ya George.

Mwezi April 2020 Derek akiwa anamkamata George kwa tuhuma za wizi dukani alimwekea goti shingoni kwa zaidi ya dakika tisa kitendo kilichosababisha George Floyd kukosa pumzi na baadae kufariki akiwa anapelekwa hospitali katika gari ya wagonjwa.

Kaka wawili wa marehemu George Philonise na Terrense Floyd tayari wametoa mawazo yao mahakamani hapo kisha mwendesha kaimu mwanasheria mkuu wa Minnesota bwana Matthew Frank.

Hivi sasa mama yake mzazi Derek Chauvin aitwae Carolyni Pawlenty nae ametoa maelezo yake na anaahidi kumsaidia mwanae kwa kila hali.

Kisha atafuata Eric Nelson ambae ni mwendesha mashatakla upande wa utetezi.

Kuna viashiria vinne ambavyo upande wa mashtaka unavitumia kumtaka jaji kuweka hukumu ya kiwango cha juu ambacho ni miaka si chini ya 30.

Viashiria hivyo ni pamoja na:

1. George Floyd alikabiliwa na ukatili kutoka kwa Derek Chauvin.
2. Kitendo cha mauaji kilishuhudiwa na watoto wadogo mtaani.
3. Derek alitenda kitendo hichio akiwa na askari wenzie watatu.
4. Derek Chauvin alitumia nafasi yake vibaya kama polisi na kama mamlaka alokuwa nayo.

Jaji ametoa dakika kumi na tano kwa mapumziko.

PIA SOMA:
- USA: Askari aliyemuua George Floyd ahukumiwa kwenda jela
 
Update:

Derek Chauvin amehukumiwa kwenda jela miaka 22 na nusu.

Atakaa jela miaka 15 kabla ya kuzingatiwa msamaha.
 
Back
Top Bottom