Hukumu haipo mnavyodhani

Taarifa zinazosambaa kuhusu hukumu ya Lissu nashangaa sana !

Itakuwa Tofauti kabisa


Britanicca
Hakika..
Si kama ambavyo inazushwa au kusemwa na kina Mange Kimambi na JasusiTV aka Evarist Chahali
Tundu Lissu ni mshindi..
Hakuna hukumu ya adhabu ya kifungo wala kifo kwa Tundu Lissu..
Inaeleweka sana kuwa wabaya wa Tundu Lissu, wanataka apotee bila kujali ana kosa au la..
Lakini mwenendo wa kesi yote tells everything, kuwa, hakuna kosa linalostahili adhabu yoyote astahiliyo TL..
In a spiritual realm, Tundu Lissu ni huru na hakuna awezaye kuuchukua uhuru wake..
Amina🙏
 
Nitamlaumu sana Lissu siku zote,zile kauli hakupaswa kuzitoa kwa upeo wake ni lazima watu wenye mtizamo tofauti na wake wange-take advantage japo kisheria wamefeli wenye mashtaka(kwa tusiojua sheria bali kupima hoja za pande zote)
Asingetoa zile kauli,asingekamatwa. Hivyo zigo lote la MO29 angeangushiwa yeye!
 
Hukumu yoyote ile itakayotoka, itakuwa ni hukumu haramu kwa sababu kesi yenyewe si kesi halali. Ni kesi ya kubambikiwa tu.
 
Wakuu hukumu inaandikwa na watu ambao majukumu na mazingira yao siyo ya siri kivile, hivyo pengine siyo sawa kuyapuuza maoni ya waja.
Kuna uwezekano ikaandikwa then ikabdilishwa baadaye ikaandikwA tena na kubadilishwa hadi siku ya hukumu kama kweli kuna mkono wa mtu aliye juu ya wanaoandika. Ila ni fact kuwa Majaji hadi sasa wanajua kama jamaa ni mkosaji au laa na pengine wanajua kama anastahili kufungwa au laa. Vilevile walio karibu na majaji wanajua nini kinaendelea hadi sasa. hakuna siri ya watu wawili na hakuna hukumu ambayo huwa ihaijulikani hadi siku ya kusoma. Waja huwa wanajua nini kitatokea siku ya hukumu na mara nyingine huwa wana mtonya mtuhumiwa.
Note kwa tathmini yangu, mananeo ya mtuhumiwa na mawakikili wenye hoja wiki ya conclusion ni kama yanatoa picha kuwa wote wanakubali kuwa mtuhumiwa hastahili kunyongwa, hivyo apewe adhabu ndogo. inavyoonekana walitaka ionekane hana hatia kwenye kosa mama, ila akutwe na hatia katika magonjwa nyemelezi. Inavyoonekana Mtuhumiwa alielezwa hivyo ndio maana aliweka mkazo mkubwa katika kujenga hoja kuwa hana kesi katika magonjwa nyemelezi wakati huohuo wenye hoja walikazia sana kwenye magonjwa nyemelezi kuliko kosa mama. Haya ni maoni yangu naweza nisiwe sahihi wakuu
 
Asingetoa zile kauli,asingekamatwa. Hivyo zigo lote la MO29 angeangushiwa yeye!
Mkuu wewe ni muona mbali, Mungu alimwepusha na kikombe kichungu! Mungu mara nyingine utumia njia yenye miba ili kumwepusha mja wake na majanga mbeleni.
Mungu aliamua kutumia njia ngumu kumfunga mdomo jamaa, kwani alijua angeendelea na hoja zile hadi siku ya tukio pengine hali ingekuwa mbaya zaidi siku ya tukio na pengine tungempoteza jamaa mazima. hivyo akamuhifadhi ili akwepe kikombe kile.
Ndio maana tunaambiwa tushukuru kwa kila jambo na tutende wema na haki na tuwe na upendo na tusiache kumtegemea Mungu wa Mbinguni.
 
Kwa maelezo ya Katuga siku ile anafanya mawasilisho ya mwisho ni dhahiri hukumu ya Lissu itakuwa si ya kunyongwa bali itakuwa ya kwenda jela! Nadhani maelekezo toka juu ni hayo. Hii haihitaji elimu kubwa kuelewa. Hii serikali haiwezi kumwacha huru kbs maana wanaogopa atawasumbua zaidi watashindwa kufanya kazi zao kwa uhuru!
 
Imajini system ya judiciary ilivyo corrupt yani badala isimame yenyewe inavyoona na kwa jinsi kesi ilivyoenda...badala yake wanasubiri mawasiliano na nani sasa...
 
unawezaje kuita hukumu kwa kesi batili..tafuta neno jingine labda, hakukuwa na kesi dhidi y Lissu.
 
Hukum itakuwa hivi.. Majaji watamhukum Lisu hukum ya kifo lakini hapo hapo wa kesi itafutwa kwa amri ya Samia kujifanya yeye ndiye aliyemuokoa na hukum ya kifo.

..Na Lissu ataendelea kuwapelekea moto.

..suluhisho ni Ccm kuacha uhuni na kutaka kuhodhi siasa za Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…