Sisi wa Sikonge, kijana Said "Hitler" Nkumba aligawa pesa ili MSONDO NGOMA wanunue Kinanda.
Wakati huo kwa sasa hapa Sikonge, mwaka huu njaa kali sana na watu hawana chakula.
Heri huyo walau kapeleka hilo kopo kuliko sisi kumpa Msondo hiyo pesa ambayo sijui waligawana saa ngapi.
Mbunge Wa Jimbo la Sikonge Tabora Saidi Mkumba akimkabidhi Kiongozi wa Bendi ya Msondo ngoma Saidi Mabera Kitata cha Shilingi Laki Tatu kwa ajili ya bendi.
Watanzania wenzangu, kama mnavyojua Tanzania iliondoa kodi kwa mtu yeyote anayeingiza kompyuta nchini. Lakini hata hivyo kuna sheria zilizowekwa kusimamia uchakavu wa vitu vinavyoingizwa Tanzania ili kuzuia nchi yetu kuwa dampo. Nimejaribu kuangalia hii picha kwa makini nimeshindwa kupata la uhakika, ila kwa mtazamo na maoni yangu niliamini kuwa hapa huyu Mbunge Makalla anatania au kuudanganya umma. Naamini hapa atakuwa anatamba kuwa ametoa msaada wa kompyuta, na printa, lakini inaoneka hivi vifaa ni vya zamani. Angalia hata keyboard.....jamani tuacheni kudanganya umma.
Wadau toeni maoni kuhusu hii picha hapa.
Laki tatu tu(300,000.00) njoo uchukue lakini hakikisha zimefika sikonge.
Sometimes ni vizuri kuliangalia jambo kama lilivo na usiende beyond.... Umeona Mazingira ilipopelekwa ni dhahiri kua hio comp labda ndo mwanzo... Hata wakipeleka Mackintosh hapo inakua haina maana, bora nyiingi kwa bei nafuu... Mradi ziwe na ubora...
Ni bora huyu aliyekumbuka jimboni kwao kuliko wale hata kuja kuwatembelea wapiga kura wao ni issu ila next time aangalie vitu vinavyokwenda na wakati
Kutoa msaada kuna ubaya gani?