Huko Rwanda nako poa!

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Kigali ni safi jamani, hilo halina ubishi.Sijui wamewatoa wapi "wawekezaji" wa usafi!
RWANDA TRIP 110.JPG
 
Tuonyeshe basi picha za sehemu mbalimbali za jiji la Kigali sio hapo kwenye park moja tu. Manake hata hapa Dar ukipiga picha moja ya pale Mlimani City ukaiweka kama hii itakuwa hamna tofauti
 
ni kweli mpendwa ni pasafi sana na garden lao limependeza sana.

good work Rwanda!

cngrats Kagame!
 
uliza kamishna watra aliomba alale barabarani wakamwambiia mzee tushalipia hotel
 
Vuvuzela usiwe na wasiwasi nina picha tele.
Na cheki hii ya Ministeri ya Ubuzima,ukitaka uzima nenda Rwanda sio kwa Kakobe!
RWANDA TRIP 144.JPG
 
so clean!

hivi bongo tunashindwa nini wapendwa? au kwa kuwa tuna akina "masaburi" kila sehemu za maamuzi?
 
Wazee acheni tu; ni mji msafi sana, mimi ninapita hapo mara mbili-tatu kila mwaka nikiwa safarini kwenda/kurudi kibaruani. Dar haifikii hata 60% ya juhudi wanazofanya hawa jamaa kuweka jiji lao katika hali ya usafi na nidhamu ya usafi na usalama. Ni mwiko kukojoa ovyo, kutupa taka ovyo, na maeneo ya kutupa taka yapo, provided for that purpose. Katika bodaboda lazima riders wavae helmet, under penalty of jail time on violation. Na ainafuatiliwa kikweli. Hawa jamaa ni wa-sure, bwana. Kigali has the reputation of being the cleanest city in Africa. N akuna mengi tu mengine ya kuigwa.
 
Kigali kweli ni safi sana.

Hapa kwetu wengi hawana asili ya usafi. Hilo ni wazi kabisa. Dar Es Salaam kabla ya kuvamiwa na wakuja ilikuwa ni mji msafi sana, nani anaikumbuka Dar ya 60s na early 70s?
 
Nyie acheni kelele..Kigali...kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi for 6 hrs hakuna operation yoyote..zaidi ya usafi kuanzia kyangugu mpaka gisenyi....na inakuwa under supervision ya jeshi na majina yanaanidikwa kama attendance ya darasani......hii ni toka 2002...kwa bongo utamkamata nani...wao usipo hudhulia na ni wachache wanaweza kutrack kila mtu usipo hudhulia mara mbili kwa mwezi hupati huduma za clinic,hospital(Kijamii) hata kiserikali juu wewe hujafanya kazi za maendele0.....watanzania milini 4+ utamdaka nani dar...kuanzia kitunda mpaka bunju....kigamboni.....we acha kabisa.
 
Hatuna haja ya kuiga Kigali. Tayari tuna miji kama Musoma na Moshi ambayo ni misafi hata kuliko Kigali! Dar waige Musoma, nk
 
Vuvuzela usiwe na wasiwasi nina picha tele.
Na cheki hii ya Ministeri ya Ubuzima,ukitaka uzima nenda Rwanda sio kwa Kakobe!

Weka pia picha za maeneo yale machafu machafu ya Kigali .. kule stendi chini chini, upande ule wa ile nyumba waliyohifadhi mafuvu.. etc.
 
Rafiki yangu alikuwa Dar es salam wiki iliyopita, akapanda dala dala akitokea sinza kwenda kariakoo, wakiwa safarini alikuwepo mama mmoja na mtoto wake anakula chungwa aliporidhika kuwa amemaliza utamu wa chungwa akamuuliza mama yake nitupe wapi makapi haya? bibi mmoja aliyekuwa kiti cha jirani akaingilia tupa nje kupitia dirishani. Msomi aliyekuwa kiti cha mbele alikerwa akadakia usitupe nje tupa ndani ya basi, bibi akaendelea na msimamo wake tupa nje kuna watu wameajriwa kufagia msomi akaendelea tupa ndani kuajiriwa kwa wafagizi sio ruhusa ya kuchafua mazingira mtoto akatupa masalia ya chungwa ndani ya dala dala. Tunahitaji elimu, tunahitaji watu committed katika kazi zao, tunahitaji kila raia wa nchi hii kuwa mdau. Lakini utamadumi wa usafi hupandwa na kujengwa tangu shuleni hebu wana JF angalieni ni shule ngapi za Tanzania zina maua kama ilivyokuwa zamani usitegemee miujiza hata vyuo vikuu usafi wa kusuasua itkuwa mitaani kwa walala hoi.
 
kwa wale ambao waliowahi kuishi kigali..ukiacha sheria za usafi..maana kule hata vocha iliyotumika ukitupa ni faini ya amafaranga elf 5 hadi 15,ni pesa nyingi kdg kwa huku kwetu tz...pia wana siku maalum ya kufanya usafi nchi nzima...hapo hakuna cha rais wala nini .wote mitaa kufanya usafi..hii inaitwa MUGANDA..huwa mara moja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi....je huku tunaweza?...kuacha kazi zetu na kufanya usafi?
 
Hivi Mlimani City nipasafi eeh, basi labda sijui usafi ni nini!! Nisamehe tu mwaya
Tuonyeshe basi picha za sehemu mbalimbali za jiji la Kigali sio hapo kwenye park moja tu. Manake hata hapa Dar ukipiga picha moja ya pale Mlimani City ukaiweka kama hii itakuwa hamna tofauti
 
LdmRRvBjpg-779c9-6d9ce.jpg yes, wanajitahidi sana, nafikiri usimamizi wa kile kinachotakiwa ndio maana wanafikia malengo waliojiwekea.
 

Attachments

  • Khev8BLjpg-bb191-d763f.jpg
    Khev8BLjpg-bb191-d763f.jpg
    24.3 KB · Views: 71
  • zK1cHatjpg-11079-2f780.jpg
    zK1cHatjpg-11079-2f780.jpg
    22.7 KB · Views: 71
  • 6TfxB8cjpg-bb71e-d97b4.jpg
    6TfxB8cjpg-bb71e-d97b4.jpg
    27.5 KB · Views: 64
  • EXdieDkjpg-88403-cf08c.jpg
    EXdieDkjpg-88403-cf08c.jpg
    29.3 KB · Views: 64
  • -Rwanda-Kagame-RDF.JPG
    -Rwanda-Kagame-RDF.JPG
    77.7 KB · Views: 72
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom