Hujuma Usalama wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma Usalama wa Taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlalahoi, Nov 25, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hujuma Usalama wa Taifa

  na Mwandishi wetu

  IDARA ya Usalama wa Taifa imekuwa ikipoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kulipa ankara za simu za mkononi za watu ‘hewa’ ambao wamefanikiwa kuzinasa ‘line’ za simu zinazotumiwa na maofisa wake wa juu. Tanzania Daima Jumatano linakuthibitishia.

  Vyanzo vya habari vya uhakika kutoka ndani ya kampuni moja ya simu za mkononi, vimelidokeza gazeti hili kuwa, wamebaini kuwepo kwa mtandao wa watu waliofanikiwa kuzinasa ‘line’ hizo ambazo hulipiwa na idara hiyo kila mwisho wa mwezi.

  Vyanzo hivyo vilieleza kuwa, kampuni hiyo ilishtushwa na matumizi na gharama kubwa ya simu hizo ambazo ziko katika orodha ya maofisa wa juu wa idara hiyo wanaolipiwa ankara za simu zao za mkononi.

  Uchunguzi wa muda mrefu wa gazeti hili ulibaini kuwa baadhi ya watu wanaotumia simu hizo si maofisa wa juu wa idara hiyo bali ndugu au jamaa zao ndio waliwahi kufanya kazi katika ofisi hizo nyeti za serikali.

  Mmoja wa watu anayetumia simu zenye ‘line’ hizo alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai hayo, awali alilitaka gazeti hili kumpa muda kutoa jibu kwa kile alichokieleza kuwa haruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari bila kupata idhini ya mkuu wake wa kazi na alilitaka gazeti kumpigia simu baada ya dakika tano.

  Mtu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Jimmy Mwang’onda alipopigiwa tena baada ya muda huo, simu yake iliita bila majibu na baadaye alipoipokea, alieleza kuwa simu hiyo ni mali ya serikali na inatumiwa na watu kadhaa wanaoisaidia serikali katika kazi nyeti, kisha akakata simu.

  Alipopigiwa tena ili kutoa ufafanuzi wa maelezo yake, simu yake ilikuwa haipatikani.

  Alipoulizwa kuhusu ukweli taarifa hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, alisema kuwa serikali haina watu wanaolipiwa gharama za simu kama maofisa wa juu wa usalama wa taifa kwa ajili ya kuisadia katika kazi nyeti.

  Alisema taarifa za kuwepo kwa watu wenye ‘line’ za simu za maofisa wa juu wa idara ya usalama wa taifa zimemshtua na aliahidi kuwa, serikali itafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kwa umma ili watakaobainika kujihusisha na mtandao wafahamike kwa umma, sambamba na kuchukuliwa hatua za kisheria.


  -Tanzania Daima 26/11/2008
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Isn't this the same Jimmy Mwangonda ambaye Mwanakijiji alimwulizia katika makala yake moja kabla ya "kustaafu"?
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Could be the same.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  I dont think kama TANZANIA DAIMA inayo credibility yoyote ile ya kuchukuliwa serious

  I'd rather some habari toka kwa FMES kuliko this rug ambalo at most halitofauinani sana na lile jarida la SANI

  no news here
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.... someni sehemu ya mwisho ya "Cheche" inasema nini kuhusu fedha za Kagoda? Huyo Jimmy Mwang'onda ni mtoto wa Apson Mwang'onda mtu ambaye anayetakiwa ajisalimishe polisi mapema kwa kuweka usalama wa Taifa letu rehani. Halafu mjiulize kuhusu maana ya "nchi imetekwa nyara"... vinginevyo itabidi na hili tulichambua pole pole kama njugu lakini alichosema Mwema lina ukweli wa aina fulani.

  Yule niliyemuulizia mimi anaitwa Benjamin Mwangonda..
   
 6. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  You can't be serious,GT!
  Of course,FMES ni credible source hapa JF but Tanzania Daima has done a heck of job in exposing mafisadi,not mentioning its line-up of top columnists eg Ngurumo,Mwanakijiji,Mpayukaji,etc.Hivi habari hii ingekuwa wapi hadi iwe credible?
  By the way,naamini Tanzania Daima knows very well who they are talking about...na kwa vyovyote wasingethubutu kuchapa kitu wasicho na uhakika nacho coz they know the consequences.
  Hivi kama fedha zinafujwa mahala kama BOT ambako taarifa zake huwekwa public mara kwa mara,what about huko UWT ambako kila matumizi ni siri kwa kisingizio cha siri za taifa?

  Is it the credibility of Tanzania Daima you are having problems with or its alleged owner?
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kila siku tunalalamika kuwa UWT hakuna kitu watu mnabisha yaani wamelala tu hakuna wanacho fanya kama namna hii wananufaisha ndugu na jamaa zao.Ngoja nifatilie kuna jamaa mmoja niliwahi msikia anaongelea maswala haya ya line kupiga simu bure nilikuwa simwelewi kumbe ndo dili zenyewe hizi duh kama wanaweza UWT nayo wabinafsishe tu hakuna.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  nAMI NAKUBAlinana na wewe kuwa UWT wamelala tena usingizi mnono...wameshapitwa na wakati..karne hii sio yao tena labda wafanyiwe mabadiliko makubwa sana la sivyo..watakuja shuka hadhi kuwa sawa na "mgambo wasiovaa uniform" hawana jipya n majungu tuuu
   
 9. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  They need to change their culture to more modern, feedback oriented, result oriented, transparent approach sometimes and not just putting on black glasses and after the president. They should be widely distributed in even communities and work positively and timely. This era does not allow false pretencies any longer
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu siyo wao peke yao. Kwani wapi bado kuko salama?? Kila mahali kumechafuka na wanaotakiwa kusafisha uchafu wote (WaTZ) bado wanapata kigugumizi cha miguu na mikono. Lakini si muda mrefu wataamka na gari lao litaondoka kwa gear ya kutisha! Nahisi kama ndoto vile!
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Tanzania Daima si gazeti la kuliamini hata kidogo

  this is a non issue
   
 12. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Toa Sababu ndg yangu na sio kusema tu si gazeti la kuliamini Kabisa
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hata wewe basi

  acha hizo
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tusaidie basi mwanzetu,lipi ni gazeti la kuaminika?Na pengine unaweza kwenda mbali zaidi kwa kutufundisha vigezo vinazolifanya gazeti (HASA LA KITANZANIA) kuwa la kuaminika.

  Is this non issue kwa vile imeandikwa na Tanzania Daima au is it the whole thing?

  GT,kama ungekuwa umefanya utafiti mdogo tu kuhusu best selling papers za Tanzania basi sidhani kama ungefikia conclusion hiyo ya kutokuaminika kwa Tanzania Daima.I'll help you a little bit on this:Best selling Dailies ni Tanzania Daima na Mwananchi na best selling weeklies ni Raia Mwema na Mwanahalisi (kabla haijafungiwa).PLEASE NOTE: Hapa nazungumzia SERIOUS NEWSPAPERS,na nime-exclude magazeti ya udaku.

  Method of enquiry:kuwauliza news vendors,visiting news stands in evening to see which papers are sold out,observations at news stands to see which paper sells fast.

  Tukiamini imani zako kwamba gazeti hilo sio la kuaminika hata kidogo basi ina maana Watanzania wengi wanaolifanya liwe among best sellers wana mapungufu ya uchaguzi wa kilicho bora.

  Kama siko sahihi,prove me wrong...pleeeez!
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tanzania Daima linatoa habari njema sana tena za undani za mafisadi. Huyo anayekataa kuwa halina habari nyeti au pengine ni za kizushi tena eti analifananisha na Sani ana yake mambo. Jamani personal hatred tuweke pembeni. Tunapopambana na joka FISADI na GRAND CORRUPTION tuwe objective. Yaliyoandikwa kuhusu hujuma hiyo TIS ni kweli and it is even beyond what the TD reported!!!! Kwa nchi yetu mambo yanavyoendeshwa kiholela bila work/emplyment ethics (public/civil) sioni cha ajabu. Kwani unaonaje hata magari yao wanavyoyatumia, ukizingatia hayajaandikwa namba za initials za serikali e.g STJ wanatumia kama kawaida (misuse). Ukitaka kujua wewe angalia landruisers na RAV 4 with private numbers lakini kwenye kioo kweupeeeeeee i.e no any sticker!!!!! Ukiachilia mbali manissan, saloon cars , you name all!!! Hivi kwanini wasiwe wanafanyiwa Auditing????? Au wanafanyiwa mimi ndo sielewi????? Yaani kama audit ipo naamini Audit query ni nyingi na abnormal zingehitaji independent audit ya Ernest and Young ya EPA. Expenditures yao ni ya kutisha!!!!
   
 16. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama sio la kuaminika kwako kwangu na kwa wengine wengi bado linaaminika sana tu mkuu kulinganisha na vyombo vingine kibao nchini.


  Siwezi kushangaa huenda ni katika harakati za kujitetea na kijenga imani ya UWT kwa raia, kitakuwa ni kitu cha kushangaza kama hawapo hata humu JF.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwani Muungwana alipotakiwa kupangua alihitajiwa hata na huku kwenye usalama wa Taifa kupangua na kuweka vijana wepya ,simu za watu hao au za chombo hicho kutumiwa kiholela ni hatari na pia ni nyenzo zinazoweza kuwapa taarifa majambazi na majangili ,au kutumika kuwasiliana na majambazi na kuwapa green light ni yaleyale ya akina Zombe ,bado tunao akina Zombe katika system za Usalama.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...