Hujafa Hujaumbika...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujafa Hujaumbika...!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PakaJimmy, Mar 5, 2010.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jana nililazimika kumtembelea huyu rafiki yangu, amelazwa pale Hospitali kuu ya Rufaa ya KCMC.
  Yuko ICU.
  Yuko hoi bin taaban. Mtu mwoga hutamtazama kwa sekunde 10!
  Mipira kadha imeingizwa mwilini kupitia puani.
  Haongei, hasogezi kiungo, hatazami.
  Ngozi yote ya asili ya mwili wake imeumuka, imetoka, kama vile amemwagiwa uji wa moto, au kama mnyama aliyechunwa ngozi, tayari kwa kitoweo!
  Kwa ufupi, ni kwamba hawezi, anasikitisha!

  Ni mwajiriwa wa TANAPA, ni dereva.
  Jumatano iliyopita23/2/2010 ilikuwa asafiri kuwapeleka wakuu wake kwenda Mkoa wa Pwani kwaajili ya vikao, lakini jumanne yake ghafla alianza kuumwa sana.
  Akakimbizwa Seliani Hospitali, ambapo walipomwangalia, moja kwa moja walimpa rufaa ya KCMC baada ya kuona ugonjwa wake si wa kawaida, na anabadilika kwa kasi ya ajabu kila sekunde zinapoongezeka, anakuwa critical!

  Kwa mujibu wa ndugu zake, madaktari hawajagundua ugonjwa, zaidi ya kususpect allergy!

  Tukiwa hapo Hospitali, kama kawaida kila anayeingia kumwona akitoka anasema lake!..Lakini kilichonivuta ni kauli za wengi wakisema :
  -Safari iliyokuwa afanye huyu ndugu, kuwapeleka wakuu wake Pwani ndiyo inayomponza!
  -Wengine wakisema, ni gari jipya alilokabidhiwa aliendeshe, ndo linalommaliza!

  Mimi si muumini wa uSHIRIKINA, lakini kauli na simulizi za watu hawa zinatisha!
  Wadau niambieni, kuna ukweli gani katika dhana nzima ya kauli kama hizi?

   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Poleni sana jamani.Ungekuwa DSM ningekwambia kamuulize sheikh yahya!!
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Chineke, kwani gari kapewa ya kwake au ni ya ofisi na ndio kazi yake ya udereva.....hey
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mkuu Bulesi,
  Du hii ni kali tena!...Uko serious?
  Unamwamini kisa alitangaza kwamba atakayegombea na Kikwete atakufa?..au kuna sababu zingine.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni signature ya bwana PAZIA (hapo juu).
  Tuheshimu matakwa yake PLZ!
   
 6. senator

  senator JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwa kweli ushirikiana especially kwa madereva na wengine wenye kazi za kipato kidogo upo kabisa.Nakumbuka kuna dereva mmoja wa serikali alikuwa anamuenda mnene mmoja.Yule bwana kila siku alikuwa kwenye gari yake anachoma ubani na kunuia nia zake azijuazo mwenyewe.Binafsi si muuumin wa USHIRIKIANA ila haya mambo yapo na mtu hulazimishwi kuyakubali mpaka yatakapokutokea.
  Pole sana kwa maswahibu yaliyomkumba huyo dereva
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mleteni hapa ufufuo na uzima ubungo, ndani ya mda mfupi atapokea uponyaji
   
 8. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duh Pole sana ndugu!

  Kwani madaktari hapo KCMC wameshindwa kutambua kabisa ni ugonjwa gani?!
  Kama wanasema ni allergy, huwa kuna sindano unachomwa ambayo baada ya half an hour unaanza kuona matokeo, amechomwa hyo sindano?!

  Kama hawaoni kitu na jamaa anazidi kuzidiwa itabidi mumpeleke kwenye maombi ya kweli, kama watu wa Charismatic Catholic wapo pande hizo nashauri muwaombe wawasaidie, au Mwakasege?! All in all, itabd aombewe big time kama hospitalini hawataona chochote!

  Kwasasa jipeni moyo na kuamini kuwa ni allergy au ugonjwa wa kawaida, tusikimbilie kuwa kachezewa...
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wala USIJARIBIWE KIIMANI mkuu PIIJEEII!nakuombea kwa mwenyezi mungu AKUKINGE NA YULE MWOVU!...nduguyo ANAUMWA ALERG YA KAWAIDA TU.....they will need sometimes to gundua it!

  POLE SANA MNDUGU!mpe pole na nduguyo...!

  YOTE YAWEZEKANA KWA IMANI,YOTE YAWEZEKANA KWA IMANI
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,867
  Likes Received: 2,620
  Trophy Points: 280
  Huyu mgonjwa si wa kubebwa na kusafirishwa, kama nimemuelewa vema PJ. Kwani hapo kanisani hamuwezi kumuombea akapona akiwa kulekule? Hakuna waumini wa kanisa lenu kule Moshi wamwombee?
  Ughwe Nnyambala bhule bhule?
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Haswaaa!!!
  Ila huyo mgonjwa jaribuni kumpeleka pale YMCA kuna dokta mmoja ni mtaalamu sana wa masuala ya mzio(allergy)

  Pia msidharau dawa za kienyeji, zinahusika sana, sijasema mkapige ramli, la hasha
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Mar 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Daa,pole yake.Ni kweli kabisa kabla hujafa hujaumbika.Rejea Mudhihiri(MB) na wengine wengi.
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Kuna mijitu haijui hii msemo "hujafa hujaumbika" wanajiona wao ndio wao ndio mwisho wa dahari.
   
 14. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ndugu kama unaamini Mungu yupo,pia amini uchawi upo na mtu anaweza kurogwa.Cha msingi aendelee kuwa hapo hospitalini,mara kwa mara walokole hupita hapo kuwaombea wagonjwa.Hakuna sekta inayoongoza kwa kurogana kama madereva wa kitanzania.
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  I prefer this zaidi
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Actually kuna myth nyingi sana juu ya mienendo mibaya ya kishirikina ya madereva!..

  Nilipata kuambiwa kuwa kuna dereva mmoja anapokaribia kwenda likizo gari yake inaharibika na kuwa grounded hadi atakapomaliza likizo, na anakuja kuiendesha mwenyewe!!

  Sijui mambo haya yanaashiria nini!
   
 17. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,033
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mungu wa mbinguni aishie milele amponye kwa jina la yesu.. Amen
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Huyu mgonjwa habebeki, kwa ufupi maneno ya kamusi ya kiswahili hayatoshi kuelezea hali anayoipitia huyu ndugu!

  Kama alivyosema Mkuu Idimi, nami nijuavyo mimi ni kwamba Nguvu za Mungu hazina mipaka, wala mkoa wala kabila!..Zinatenda kazi kwa sala tu!

  Hivyo, watu wa Mungu popote mlipo, tumwombee huyu mtu ili aponywe, mtabarikiwa sana!
   
 19. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Amen!!! Napenda watu wanaomtanguliza MUNGU kwenye maisha yao!!! PakaJimmy kuwa na uhakika kuwa huyo mgonjwa wako amepona kwa maombi haya ya hapa yanatoa tumaini. YESU KRISTO NI MPONYAJI NA ANASIKIA MAOMBI YA WATU WANAOMAANISHA!!! Glory to GOD
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Naamini kabisa!..AMEEN!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...