Hugo Chavez: Mjamaa, muuza unga, mgonjwa wa “totoz”

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Image may contain: 1 person

Hugo Chavez ni shujaa wa itikadi ya Ujamaa mpaka kifo kilipomchukua Machi 5, 2013. Watu wenye imani isiyoyumba ya falsafa zote za Mrengo wa Kushoto (Left-Wing), kwao Chavez alikuwa jemedari kinara dhidi ya Ubepari.

Chavez aliuchukia ubepari na aliijenga Venezuela kuwa taifa la Kijamaa kupitia vyama vya Movement for the Fifth Republic kati ya mwaka 1997 mpaka 2007 kisha United Socialist Party kuanzia mwaka 2007 hadi roho yake ilipotengana na mwili wake.

Hata sasa, mwili wake ukiwa umepumzishwa kwenye makaburi ya Cuartel de la Montana, yaliyopo Caracas, Venezuala. Chavez anakumbukwa kama mwasisi wa Serikali ya Bolivarian.

Desemba 17, 1982, Chavez aliasisi Vuguvugu la Kimapinduzi la Wana-Bolivar-200 (Revolutionary Bolivarian Movement-200) ambayo kwa kifupi hutambulika kama MBR-200.

Vuguvugu hilo, Chavez alilianzisha kwa kushirikiana na maofisa wenzake wa jeshi, Felipe Carles na Jesus Hernandez. Jina Bolivar, walilitumia kama heshima kwa Simon Bolivar, ambaye alikuwa mtawala wa kijeshi na kisiasa, aliyefanya kazi kubwa kuasisi mataifa ya Venezuela, Bolivia, Colombia, Ecuador, Peru na Panama katika miongo minne ya mwanzo ya Karne ya 19.

Maono na nadharia za kiutawala za Bolivar ambaye alijulikana pia kama El Libertador, ndiyo sababu ya Chavez na wenzake kuita harakati zao kuwa Vuguvugu la Kimapinduzi la Wana-Bolivar.

Februari 4, 1992, Chavez akisaidiwa na Serikali ya Cuba, chini ya hayati Fidel Castro, walifanya jaribio la kwanza la mapinduzi ya kumwondoa aliyekuwa Rais wa Venezuela, Carlos Perez. Kushindwa kwa jaribio hilo, kulisababisha Chavez na wenzake wafungwe jela.

Novemba 27, 1992, jaribio la pili lilifanyika kumwondoa madarakani Perez, wakati Chavez akiwa jela. Vijana watiifu wa MBR-200, walipokea maagizo kwa Chavez, aliyesuka mpango akiwa jela. Hata hivyo, jaribio hilo pia lilikwama.

Julai 1997, MBR-200 walibadili jina na kujiita Movement for the Fifth Republic (MVR) ili kitambulike kuwa chama cha kisiasa, lengo likiwa kumwezesha Chavez kugombea Urais katika Uchaguzi wa Rais wa Venezuela mwaka 1998.

Uchaguzi ulifanyika Desemba 6, 1998, Chavez alishinda kwa asilimia 63.5 dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Carabobo, Venezeula, Henrique Romer.

Kuanzia hapo, Chavez aliamua kuifanya Venezuela kuwa nchi ya Ujamaa, akifuata nyayo za Castro wa Cuba ambaye alikuwa Mkomunisti kindakindaki na mfuasi wa falsafa za ‘manabii’ wa Ukomunisti, Carl Marx na Vladimir Lenin, yaani Marxist-Leninist.

Chavez alijitangaza kuwa Marxist kisha kutengeneza ushirika na Serikali za Kijamaa za Evo Morales (Bolivia), Rafael Correa (Ecuador) na Daniel Ortega wa Nicaragua.

Hiyo ndiyo sababu ukimgusa Chavez, unaweza kukutana na hasira za wafuasi wa itikadi za Mrengo wa Kushoto. Misimamo ya Chavez dhidi ya Marekani ambalo ni taifa kiranja la Ubepari duniani, ni jambo ambalo humfanya atetewe na Wajamaa kokote duniani.

CHAVEZ MUUZA UNGA

Sakata la Narcosobrinos nchini Venezuela ndilo ambalo lilifanya watu wengi kuamini kwamba kweli Chavez alikuwa muuza dawa za kulevya. Japokuwa enzi za uhai wake alikuwa akishutumiwa tu bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

Narcosobrinos ni maneno ya Kispaniol (Spanish au Castilian) yenye maana “Wapwa Wauza Unga”. Narco ni Wauza Unga na Sobrinos ni Wapwa.

Narcosobrinos ni maneno yaliyotumiwa na vyombo vya habari kutambulisha sakata la wapwa wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flores, waliokamatwa na kilogramu 800 za cocaine Novemba 10, 2015.

Wapwa hao wa Rais Maduro, wanaitwa Efrain Antonio Campo Flores na Francisco Flores de Freitas, walikamatwa na maofisa wa kikosi cha ujasusi cha kupambana na dawa za kulevya cha Marekani (DEA), walipokuwa Port-au-Prince, Haiti, wakijaribu kuingiza mzigo huo wa cocaine Marekani.

Novemba 18, 2016, wapwa hao wa Rais Maduro walikutwa na hatia. Maelezo yaliyotolewa mahakamani ni kuwa wapwa hao walikuwa wametumwa tu, kwamba wahusika ni Rais Maduro na mkewe Cilia ambaye ni Naibu Rais wa Bunge la Venezuela.

Ilielezwa kuwa fedha hizo za cocaine zilikuwa kwa ajili ya kusaidia familia ya Rais Maduro kuendelea kubaki madarakani. Ikaongezwa kuwa familia ya Rais Maduro inaongoza mtandao mpana wa unga ambao imeurithi na kuuendeleza kutoka kwa Chavez.

Mhariri wa Washington Post, Jackson Diehl, alipata kuandika habari kuhusu mtandao mpana wa dawa za kulevya kwenye Serikali za Amerika Kusini, akasema kuwa Chavez na timu yake ya Serikali ya Mapinduzi ya Bolivarian, walikuwa wanaongoza genge hatari la wauza unga.

Kwa mujibu wa Diehl, mtandao wa Bolivarian, ulianza kutengeneza fedha nyingi miaka 1980 walipoanza harakati za kuchukua madaraka nchini Venezuela, na kwamba fedha nyingi walizopata ziliwezesha Chavez kushinda Urais mwaka 1998.

Ilibainishwa kuwa mtandao huo wa Chavez una nguvu kuliko genge lolote la unga katika Bara la Amerika Kusini kwa sababu lenyewe linamiliki Serikali. Hata sasa baada ya Chavez kufariki dunia, mrithi wake Maduro anaendeleza ‘libeneke’.

MGONJWA WA WANAWAKE

Promiscuity ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtu mwenye tabia za kufurahia kuwa na wapenzi wengi kisha kuwabadili mara kwa mara. Kwa mwanaume, msamiati huo hubeba maneno mengine yenye kumaanisha mwanaume mchezea wanawake kama vile Womanizer au Philanderer.

Mfululizo wa simulizi za mapenzi za Don Juan huleta karibu tafsiri ya mwanaume mchezea wanawake kimapenzi. Don Juan ambayo simulizi yake ya kwanza iliandikwa mwandishi wa tamthiliya wa Hispania, Tirso de Molina, humpambanua mtu wa kufikirika anayeitwa Don Juan kuwa kiboko ya wanawake, yaani kila mwanamke anayemwona humtaka.

Misimamo ya Chavez kisiasa, hufanya watu wengi kuamini alikuwa ‘mgumu’, lakini ukweli ni kwamba vitendo vyake vilisababisha watu kumwita Don Juan. Wakimfananisha na Don Juan pendapenda, anayetamani kupanda kitandani na kila mwanamke.

Si tu kwamba Chavez alipenda wanawake, vilevile wanawake walimpenda Chavez. Aliwahitaji nao walimtaka, kwa hiyo akawa anawapanga kwa foleni, nao walijisogeza kwake angalau kupata kumbatio au busu.

Chavez alipenda kuwa katikati ya matukio yenye kuhusisha wanawake. Chavez alipata kumshika mkono Malkia wa Uingereza, Elizabeth II na kutembea wakiwa wameshikana mikono, kitendo ambacho alifahamu fika kuwa hakiruhusiwi kwa utamaduni wa Uingereza.

Kashfa nyingine ni kuwa Chavez, aliwahi kufanya jaribio la kumbusu Malkia Sofia wa Hispania, vilevile aliyekuwa Rais wa Chile, Michelle Bachelet.

Chavez pia anadaiwa kutaka kufanya mapenzi kwa nguvu na mwandishi wa habari wa CNN idhaa ya Espanol, Patricia Janiot, vilevile mwanaharakati wa Marekani, Cindy Sheehan pamoja na mtangazaji wa televisheni, Barbara Walters.

MAISHA YA NDOA

Chavez ana msururu wa wanawake ambao alitenda nao dhambi ya zinaa. Hata hivyo, katika maisha yake yote alioa wanawake wawili tu.

Alipokuwa na umri wa miaka 23, Chavez alifunga ndoa na mke wake wa kwanza, Nancy Colmenares ambaye ni mama wa watoto watatu wa kwanza wa Chavez ambao ni Rosa Virginia, Maria Gabriela na Hugo Rafael.

Chavez akiwa kwenye ndoa, alikutana na mwanahistoria wa mapinduzi, Herma Marksman. Baada ya kukutana wakadumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 10, kipindi chote hicho, Chavez alikuwa kwenye ndoa na Nancy.

Ripoti nyingi zinaeleza kuwa Herma ndiye mwanamke ambaye Chavez alimpenda sana. Kwamba mwanamke huyo ndiye alimshawishi Chavez kufanya jaribio la kumpindua Perez na Serikali yake mwaka 1992.

Chavez alipokuwa jela mwaka 1992, gazeti la Televen la Venezuela, liliripoti kuwa Chavez alimwandikia ujumbe Nancy kumwomba msamaha kwa sababu kipindi chote akiwa na Herma, alimwacha mpweke bila fedha za matumizi, na mwishowe yupo jela. Baada ya hapo, ndoa ya Chavez na Nancy.

Kipindi hicho, Herma aliendelea kuwa karibu na Chavez, akimtembelea jela na kumhudumia lakini uhusiano huo ulianza kudorora na ulivunjika Julai 1993, wakati Chavez akiwa jela. Baadaye, Chavez akiwa Rais wa Venezuela, Herma alikuwa mmoja wa waliopinga utawala wake.

Mwaka 1994, Chavez na wenzake waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Rafael Caldera, aliyeingia madarakani mwaka huo, na miaka miwili baadaye, Chavez alikutana na mke wake wa pili, Marisabel Rodriguez.

Marisabel alikuwa mrembo na mtangazaji wa redio. Katika ndoa yao, walifanikiwa kupata mtoto mmoja tu ambaye ni Rosines. Chavez na Marisabel walifunga ndoa mwaka 1997 lakini ikavunjika mwaka 2004.

Sababu ya ndoa hiyo kuvunjika, Marisabel alisema ni tabia ya Chavez kuwa na wanawake wengi, kwamba aliyachukia maisha ya Chavez kwa jumla. Hata hivyo, Chavez alijitetea kuwa Marisabel alikuwa mwanamke mwenye hasira ndiyo maana waliachana.

Chavez na Marisabel walipeana talaka kisheria na kukubaliana malezi ya mtoto, ingawa kila mmoja alitaka yeye ndiye amlee. Chavez alisema Marisabel alikuwa anaonesha vitendo vibaya vyenye kuathiri ukuaji wa mtoto, wakati Marisabel alisema kuwa Chavez alikuwa mgomvi nyumbani.

Baada ya kuachana na Marisabel, Chavez alianza kuwabadili wanawake kwa fujo bila aibu, maana hakuwa tena kwenye ndoa. Inaelezwa kuwa Chavez alikuwa na mwanamke mmoja kwenye Jiji la Ciudad Bolivar, Venezuela, ambaye alikuwa akisafiri naye kwa ndege ya Rais, wakati kiongozi huyo alipokuwa kwenye ziara.

Mbunge wa Colombia, Piedad Cordoba, mwanamuziki wa Marekani, Courtney Love na mtoto wa mwanasiasa wa Venezuela, Jose Vicente Rangel, ni kati ya wanawake ambao Chavez aliwabadili na kuwazungusha kwa nyakati tofauti.

NAOMI CAMPBELL

Mwaka 2007, vyombo vya habari nchini Venezuela na vile vya kimataifa, viliripoti kuhusu penzi motomoto lililokuwepo kati ya Chavez na mwanamitindo wa Uingereza, Naomi Campbell.

Naomi wakati alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu Chavez, alijibu: “Rais siyo nyani, lakini anafanana na ng’ombe.” Kauli hiyo ya Naomi ilisababisha magazeti mengi yairudie kwa wiki kandhaa nchini Venezuela.

ALICIA CASTRO

Balozi wa zamani wa Argentina nchini Venezuela na Uingereza, Alicia Castro, alizama pia kwenye mapenzi na Chavez. Uhusiano wao ulianza wakati Chavez akiwa bado kwenye ndoa na Marisabel.

Alicia aliwahi kukanusha habari hizo, akijitetea kwamba alimpenda Chavez kwa sababu za kimapinduzi na siyo mapenzi. Hata hivyo aliandamwa na vyombo vya habari kuwa walikuwa na mapenzi motomoto.

RUDDY RODRIGUEZ DE LUCIA

Muigizaji na mrembo aliyeshinda taji la Miss Venezuela World, Ruddy Rodriguez de Lucia, aliwahi kuandikwa na vyombo vya habari kuwa katika mapenzi na Chavez.

Pamoja na Ruddy kukana, vilevile katika hili ilibidi na Chavez mwenyewe aseme kwamba walikuwa wanamsingizia.

MARIA GABRIELA

Huyu siye mwanamke wake, bali mwanaye. Hata hivyo, baada ya kuachana na Marisabel, Maria ndiye aliyepewa hadhi ya kuwa First Lady wa Venezuela, kipindi chote baba yake akiwa madarakani kuanzia mwaka 2004 mpaka alipofariki dunia.

Maria ni mtoto wa pili wa Chavez, alipendwa na baba yake kwa sababu ndiye pekee katika watoto zake aliyependa kufanya siasa. Chavez alimpa nafasi kubwa ili kumkuza kisiasa.

Wakati Chavez akiumwa matatizo ya saratani na mapafu, Maria ndiye alikuwa karibu kumhudumia baba yake mpaka alipofikwa na mauti akiwa Hospitali ya Jeshi, Caracas, Venezuela.

Chavez aliugua kwa miaka miwili mfululizo, na matibabu yake alifanyiwa nchini Cuba kwa swahiba wake, Castro.

Huyo ndiye Chavez, komredi hasa lakini mwenye kashfa ya kuuza dawa za kulevya, vilevile mgonjwa wa wanawake.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Hongera Sana kwa us maridhawa
 
m
 
Back
Top Bottom