Kitenge: Akandwanao Alikanda Unga wa Ngano

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,776
24,211
Akandwanao Alikanda Unga wa Ngano

Kila mtalii aliyekuja Zanzibar alikuwa na hamu ya kula chapati za maji na za kukanda kwasababu ya uwezo wa kijana Akandwanao kuyageuza maji na unga wa ngano kuwa chapati tamu zenye ladha ya peponi,Siku zote hapa Zanzibar watalii wanaishi kwa tabasamu maridhawa kwasababu ya ufundi mkubwa uliopo kwenye mikono ya Akandwanao kwenye kugeuza unga wa ngano kuwa mithili ya medali shingoni.

Kule bara jina la Akandwanao limeandikwa sana kwenye vibao vya almasi kwasababu uwezo wake wa kuyageuza maji na unga kuwa chapati ya maajabu na zaidi kumgeuza Mlandege kuwa Mlasimba.Kwasasa kule bara hadithi za vijiweni ni kuhusu Akandwanao ilikuwaje akaweza kugeuza chapati kuwa goli maridhawa mbele kaka Ayubu, hakika vikombe,birika na kahawa yenyewe vimefurahi sana kusikia hadithi nzuri ya binadamu ambaye mikono yake iliigeuza msimbazi nzima kuwa chapati mbaya.

Enyi watu wa bara na visiwani nawaambieni kazi zote zinaohusu kuugeuza unga wa ngano kuwa matumaini kuwa faraja kuwa heri mpeni Akandwanao bila shaka atazifanya vizuri kabisa, kwasababu Mwenyezi Mungu alimuumba akampa mikono na miguu kwa ajili ya kazi hiyo lakini alimpa pia akili ili chombo muhimu cha kugeuza kila rangi nyekundu kuwa chapati nyembamba kuwa moyo wa mwanasonono.

@omarrkombo
 
Daah huyu kitenge ni mkorofi
1705327843999.jpg
 
Jamaa alichambua chuya zote akabaki na mchele safi, aliwachambua beki wa kolo fc kama anachambua karanga vile, asipomwaga wino yanga au azam hatakuwa hajatendewa haki kabisa, jamaa ni fundi kwer kwer.
 
Jamaa alichambua chuya zote akabaki na mchele safi, aliwachambua beki wa kolo fc kama anachambua karanga vile, asipomwaga wino yanga au azam hatakuwa hajatendewa haki kabisa, jamaa ni fundi kwer kwer.
Zanzibar Kuna vipaji sana
 
Back
Top Bottom