TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,720
- 10,220
BREAKING: BONDIA CHANGARAWE
AFANYA KWELI USIKU HUU ITALY, AMTWANGA MVENEZUELA KWA KO!
Na Nsangu Kagutta, Italy
Yusufu Luccasi Changarawe usiku huu ameing'arisha Tanzania baada ya kushinda pambano lake la kwanza la kutafuta kufuzu kushiriki kwenye mashindano ya
Olympic jijini Paris, Ufaransa, yatakayofanyika baadaye mwaka huu.
Changarawe ambaye anapigana katika uzito wa Light Heavy wa Kilo 80, ameshinda kwa knock out ya raundi ya kwanza kwa kumcharaza kwa ngumi nzito bondia wa Venezuela, Perreira Diego.
Bondia wa huyo Venezuela aliingia kwa mkwara na kujaribu kumchanganya
Changarawe ambaye alionyesha utulivu wa
hali juu kudhihirisha uzoefu na mbinu
alizonazo za mchezo wa ngumi.
"Jamaa ni mzuri sana na ilikuwa vigumu kumsoma maana sikuwahi kumuona hata kwenye mitandao" alisema Yusufu Wakati akiongea na Wabongo Ughaibuni Media.
Changarawe, anayetakiwa kushinda mapambano manne ili kufuzu, anaingia tena ulingoni kesho Alhamisi kupambana na bondia wa Norway.
Mshindi huyo wa medali ya Shaba wa Michezo ya Jumuiya ya Madola, ameongozana na mwalimu Mohamed Abubakari Mohamed na Makamu wa Rais wa kamati ya Olympic Tanzania, Henry
Tandau.