Huenda watoto wakapungua Mashuleni

Huenda watoto wakapungua Mashuleni

manking

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2014
Posts
1,306
Reaction score
316
Habarini ndugu zangu,
Kwanza kabisa nawapongeza wote mlio oa na kuolewa Mungu awabariki muendelee kuijaza nchi(kuzaa)
kama tulivyoagizwa.
Binafsi nimefanya utafiti nikagundua kuwa vijana wengi sasa hivi hawako tayari kuingia kwenye ndoa(kuoa au kuolewa)
kwa madai kwamba 1.Maisha magumu
2.Kutoaminiana kwa sababu ya maadili kuporomoka.
3.Wengine wanahitaji wapate maendeleo ndipo waoe au kuolewa.
Wasiwasi wangu baadae watotowatapungua kama sio kuisha kabisa kwa sababu hawatendelea kuzaliwa wengine, na
athari ambazo zitajitokeza ni kama zifuatazo
(1) kupungua kwa ajira kwa walimu hasa wa shule za awali(chekechea) na msingi
(2) kukosa nguvu kazi mpya katika jamii hivyo kukosa maendeleo na kukuza uchumi.
Mfano wa watu ambao hawataki kuoa ni mwanamuziki Dimond , Dr. slaa na wengine wengi. Hapo ndo mwisho wa utafiti
Toa ushauri wako.
 
Kama umasikini na maisha magumu ingalikuwa kigezo cha kutozaa ama kufunga ndoa, basi Afrika isingalikuwa na watu wengi namna hii...

Mi naamini utafiti wako uko kinyume.. yaani hali ngumu ya maisha ndo inachangia sana kuongezeka kwa watoto wasiokuwa wamepangwa, ndoa zisizotarajiwa kwa sababu ya kuwahi kujiegesha mahali salama na mengineyo...

Angalia most developed countries kama UK, Germany nk, je kutokana na wao kuwa na kipato, utafiti wako unafiti vipi?

Nakaribisha arguements... sio matusi!
 
mkuu,.watu hawaoi au kuolewa lakini kila siku wanazaa. wengine wana watoto hadi 10 wakati hawajaoa/ kuolewa. labda useme kuhusu ndoa ila hapo kwenye kuijaza dunia! nadhani ungerudia itafiti wako mkuu
Kuijaza dunia kulingana na maandiko ya Mungu mkuu.
 
kumbe kuoa au kuolewa ndio kuzaa!!

mbona kati ya hao uliowataja mmoja ana watoto?
 
Kuijaza dunia kulingana na maandiko ya Mungu mkuu.

haya ni mawazo yako mkuu yanapaswa kuheshimiwa ila kama ulikuwa unamaanisha kwa mlengo wa dini ungesema" huenda idadi ya watoto halali( waliozaliwa wakati wazazi wako ndani ya ndoa) ikapungua" lakini si kusema idadi ya watoto kwa ujumla, kitu ambacho sio kweli mkuu. sababu ya kutooa/ kuolewa haiwezi ikapunguza idadi ya watoto mkuu( hasa hapa tanzania kwetu). wangapi tunawaona mitaani wakizaa bila ya ndoa?... ukweli ni wengi mno.
 
Karudie utafiti wako upya, nikupe na la kuanzia ukichunguza wenye mbaraka ya kuwa na watoto wengi ni sisi tulio na khali ngumu coz unatoka kwenye kazi yako ya suruba unapitia sehemu unagonga kiroba , kiburudisho cha mwisho ni home kwa mama yoyo tunapanga watoto kila mwaka gud,
Kwa nyie mnaofanya maneno kizungu na mmeyapatia maisha mnang'ang'ana kumeza madawa ya kupanga uzazi mwishowe mnakosa au mnapota mmoja, so kafanye utafiti upya.
 
Sample yake itakuwa ya elites ...ambao wengi wanafuata western trends...kabla ya kuzaa wana calculate gharama ya kusomesha saint fulani...lol

Vijijinu wanakwambia Mungu aliyewaleta duniani ndie atakayejua watakula nini na kusoma wapi...

Kama umasikini na maisha magumu ingalikuwa kigezo cha kutozaa ama kufunga ndoa, basi Afrika isingalikuwa na watu wengi namna hii...

Mi naamini utafiti wako uko kinyume.. yaani hali ngumu ya maisha ndo inachangia sana kuongezeka kwa watoto wasiokuwa wamepangwa, ndoa zisizotarajiwa kwa sababu ya kuwahi kujiegesha mahali salama na mengineyo...

Angalia most developed countries kama UK, Germany nk, je kutokana na wao kuwa na kipato, utafiti wako unafiti vipi?

Nakaribisha arguements... sio matusi!
 
hizi tafiti zimezidi kuwa nyingi,na mbaya zaidi ni za uongo
Nenda kwenye mahospitali wauguzi wakupe takwimu za watoto wanaozaliwa kila siku alafu urudi tena kutupa majibu
 
Mkuu vijana wanasababu nyingi hiyo ya umasikini ndo inayo sumbua wengi hasa anapofikiria anaingia kwenye majukumu
wakati kipato hakiridhishi inamuwia ugumu kuingia ktk ndoa. Siku hizi haijalishi uko mjini au kijijini kipato cha kukidhi mahitaji ni muhimu kwenye familia ghalama za maisha ziko juu pande zote.
 
hizi tafiti zimezidi kuwa nyingi,na mbaya zaidi ni za uongo
Nenda kwenye mahospitali wauguzi wakupe takwimu za watoto wanaozaliwa kila siku alafu urudi tena kutupa majibu

Utafiti wangu umefanyiwa upembuzi yakinifu mjini na vijijini, kwa wenye elimu na wasio na elimu, mfano watoto wamitaani wamepungua kiasi kikubwa(iko nje ya mada) hii ni nafuu kwa taifa. Kibaya wengi wanasema wanakula ujana wakati umri wao una kwenda tutapata wapi nguvu kazi baadae?
 
Sample yake itakuwa ya elites ...ambao wengi wanafuata western trends...kabla ya kuzaa wana calculate gharama ya kusomesha saint fulani...lol

Vijijinu wanakwambia Mungu aliyewaleta duniani ndie atakayejua watakula nini na kusoma wapi...
Mkuu hata vijijini sasa hivi wanatumia uzazi wa mpango maana hata uliokuwa muhimili wao Kilimo siku hizi ni majanga hawapati kama zamani njaa kila mwaka, wewe unazungumzia kijiji gani? zungumzia wingi usizungumzie wachache.
 
Habarini ndugu zangu,
Kwanza kabisa nawapongeza wote mlio oa na kuolewa Mungu awabariki muendelee kuijaza nchi(kuzaa)
kama tulivyoagizwa.
Binafsi nimefanya utafiti nikagundua kuwa vijana wengi sasa hivi hawako tayari kuingia kwenye ndoa(kuoa au kuolewa)
kwa madai kwamba 1.Maisha magumu
2.Kutoaminiana kwa sababu ya maadili kuporomoka.
3.Wengine wanahitaji wapate maendeleo ndipo waoe au kuolewa.
Wasiwasi wangu baadae watotowatapungua kama sio kuisha kabisa kwa sababu hawatendelea kuzaliwa wengine, na
athari ambazo zitajitokeza ni kama zifuatazo
(1) kupungua kwa ajira kwa walimu hasa wa shule za awali(chekechea) na msingi
(2) kukosa nguvu kazi mpya katika jamii hivyo kukosa maendeleo na kukuza uchumi.
Mfano wa watu ambao hawataki kuoa ni mwanamuziki Dimond , Dr. slaa na wengine wengi. Hapo ndo mwisho wa utafiti
Toa ushauri wako.

Utafiti wako hauna tofauti na ule wa akina BANSEN BANA., nani kakuambia watu wanoana ili wapate watoto? kalagaboho huku kwetu uswazi hata kabla hujaoa/kuolewa ni suna kuwa hata na mtoto mmoja... Rudi darasani mtafiti feki
 
haya ni mawazo yako mkuu yanapaswa kuheshimiwa ila kama ulikuwa unamaanisha kwa mlengo wa dini ungesema" huenda idadi ya watoto halali( waliozaliwa wakati wazazi wako ndani ya ndoa) ikapungua" lakini si kusema idadi ya watoto kwa ujumla, kitu ambacho sio kweli mkuu. sababu ya kutooa/ kuolewa haiwezi ikapunguza idadi ya watoto mkuu( hasa hapa tanzania kwetu). wangapi tunawaona mitaani wakizaa bila ya ndoa?... ukweli ni wengi mno.
Hao wakuzaa bila ya ndoa wanaitwa wazembe wsiojitambua na hawana malengo ktk maisha yao ya baadae na kadri maisha yanavo kuwa magumu wanatoweka.
 
Utafiti wako hauna tofauti na ule wa akina BANSEN BANA., nani kakuambia watu wanoana ili wapate watoto? kalagaboho huku kwetu uswazi hata kabla hujaoa/kuolewa ni suna kuwa hata na mtoto mmoja... Rudi darasani mtafiti feki
Nyie ndo mnasababisha deni la taifa lifikie tilioni 27 kwakuongeza matumizi yasio ya lazima mtalilipa wenyewe na balozi wenu wa uswazi hapo.
 
Habarini ndugu zangu,
Kwanza kabisa nawapongeza wote mlio oa na kuolewa Mungu awabariki muendelee kuijaza nchi(kuzaa)
kama tulivyoagizwa.
Binafsi nimefanya utafiti nikagundua kuwa vijana wengi sasa hivi hawako tayari kuingia kwenye ndoa(kuoa au kuolewa)
kwa madai kwamba 1.Maisha magumu
2.Kutoaminiana kwa sababu ya maadili kuporomoka.
3.Wengine wanahitaji wapate maendeleo ndipo waoe au kuolewa.
Wasiwasi wangu baadae watotowatapungua kama sio kuisha kabisa kwa sababu hawatendelea kuzaliwa wengine, na
athari ambazo zitajitokeza ni kama zifuatazo
(1) kupungua kwa ajira kwa walimu hasa wa shule za awali(chekechea) na msingi
(2) kukosa nguvu kazi mpya katika jamii hivyo kukosa maendeleo na kukuza uchumi.
Mfano wa watu ambao hawataki kuoa ni mwanamuziki Dimond , Dr. slaa na wengine wengi. Hapo ndo mwisho wa utafiti
Toa ushauri wako.

Ukumbuke pia bado TZ fertiliy rate ni 5.0+ children/woman.. Mtafitiii
 
Nyie ndo mnasababisha deni la taifa lifikie tilioni 27 kwakuongeza matumizi yasio ya lazima mtalilipa wenyewe na balozi wenu wa uswazi hapo.

kweli inatakiwa urudi darasani haraka.Maana deni la taifa haliwi kubwa kulingana na idadi ya watu, bali huongezeka kwa mikopo isiyo na tija....Uje nikupige shule ya demography bwana JAJA
 
Tutakuona maana tulikuwa timu ya watu 6 tulizunguka mikoa ya tanzania bara visiwani hatukuenda.
 
Back
Top Bottom