Huenda Rais Magufuli akawa ameumaliza rasmi ule ubishi wa Chuo Kikuu gani bora kati ya SAUT na UDSM

Tulinganishe Kwa Kozi moja moja au faculty Kama ifuatavyo
1.Engineering ya udsm na Engineering Ya saut Kwa vigezo vya Ufaulu wa cutt off points, vifaa vya kujifunzia, maabara, wataalam
2.LL.B ya udsm na LL. B sauti Kwa vigezo vya cutt off points, wataalam, maktaba nk
3.Education
4.udsm school of journalism na saut school of journalism
5.udsm College of social sciences na saut faculty /college of social sciences
 
Umesema sasa hv kimebaki jina tu maana ya kwamba hadhi yake kielimu imeshuka,
Njoo kwenye kwenye point hao wanaotumbuliwa wamesoma sasa hv? Au chuo kikishuka hadhi hata waliosoma zamani nao elimu yao inashuka hadhi.
Nijibu hapa
 
Unasema UDSM ilikuwa zamani sasa limebaki jina tu, eb tueleze hao unaosema wanatukanwa pumbavu na rais walisoma UDSM ipi, je ni hii unayoisema imebaki jina au ni ile iliyotengeneza jina. Mi naona kusema UDSM imebaki jina kwa kutumia mfano wa Kabudi ambaye kasoma pale UDSM ikiwa hot zaidi ya sasa ni hoja mfu, uking'ang'ania hoja hiyo inabid utuambie UDSM haijawahi kuwa bora tangu ianzishwe ukilinganisha na SAUT maana hao kina Kabudi wamesoma pale zamani mnoo ukisema chuo kimebaki jina kwa kuwatumia wao kama mfano ni nani wengine sasa watakuwa walisoma UDSM kabla yao.
Vilevile unasema Rais anatumbua watu wa UDSM, ni lini na ni wapi uliona ametumbua mtu wa UDSM na akaweka mtu wa SAUT japo sisemi anatumia kigezo cha chuo kutukana watu au kuchagua watu.
SAUT ni mbali sana, linganisha UDSM na ARDH, MUHAS, SUA 😀😀.
Mjadala wa kulinganisha UDSM na SAUT ni kupoteza mda maana nchi na dunia vinajua kipi ni chuo bora.
 
Chuo kilichobaki Tanzania na UBORA wake ni Ardhi pekee
Hivi siku hizi ubora wa Chuo nyie mnaupimaje.Mimi zamani babu yangu mzaa baba wakati tunachagua chuo cha kujiunga kabla ya kufanya mtihani wa mwisho nilimuuliza nichague chuo gani bora kuliko vyote,Jibu.Nyerere amefanya vyuo vyote vimekuwa na ubora unaolingana kutokana na fani inayotolewa chuoni hapo.Hivyo chagua chochote.Na hili nilikuja kuliona baada ya kumaliza chuo kwa kuwa,utendaji wa mwanafunzi yeyote aliyemaliza kipindi hicho wote kwa fani zao tofauti tofauti ulikuwa wa hali ya juu sana.Ndio hao walioifikisha Tanzania hapa tulipo pamoja na kwamba hapa katikati walipoingia wazamiaji wakapoteza mwelekeo mzuri uliokuwepo.Wewe Ubora chuo unaupimaje.Njoo huku tuelewane aisee....
 
Sample ya wasomi wa udsm

Jk
Museven
Chato boy
Kabudi
Lile RC la mbeya

Ndu guy

Acha niishie hapo maana sampuli ya wasomi inajulikana inapoelekea
 
Tanzania leo tunalalama uchumi mbovu, hakuna utawala bora lakini ni matokeo ya unyumbu wa viongozi ambao wamesoma jalalani.......

Jalalani sasa hivi pamebakia na experience ya miaka tu na sio ubora wa elimu....sasa hivi mbakie mnajisifu kuwa jalala lenu lina umri mkubwa tu...

Imagine mwanafunzi anamaliza sheria udsm lakini akienda law school hatoboi, akitoboa ni kwa kusuasua sana compared na wenzie wa vyuo vingine,

Hata kwenye ajira siku hizi watoto wa udsm wanapelekwa mswaki tu.

So professor kabudi hakukosea aise, udsm mtabaki kuwa chuo mama lakini sasa mmepata vyuo baba, nyie bakini kuwa mama tu.....

JALALANI OYEEEEE
 
Yaani kuwaita wahitimu wa chuo fulani, ambao wamekosea kitu katika utendaji wao wapumbavu ndio ihalalishe chuo kingine kuwa bora? SAUT ni chuo kichanga sana ktk game hii ya uelimishaji. After all waliokosea ni walimu wa miaka ambayo SAUT ilikuwa haijazaliwa. Pia tusisahau wahitimu wa UDSM wa miaka hiyo ndio waliweka misingi ambayo tunajivunia kama taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…