Huenda binadamu ni silaha za kibaiolojia zilizoletwa duniani kama virusi wa kansa ili kuiharibu Dunia

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Tofauti Kati ya Dini Na sayansi/filosofi kuhusu Sababu ya Sisi kuwepo duniani Na Nani ametuleta mahali hapa Ni Moja:

Approach ya Dini katika kuelezea Sababu yetu kuwa hapa duniani inaanzia kwenye hitimisho (Religion approach is from the conclusion) kwamba Mungu ndio ametuleta hapa duniani ili tumuabudu. (Hapa dini tayari imesha conclude Sababu ya Sisi kuwepo duniani. Imetoa sentensi Moja ambayo Ni FINAL and CONCLUSIVE )

Approach ya science katika kuelezea Sababu yetu Sisi kuwa hapa duniani Ni kuelekea kwenye hitimisho (Science/ philosophy approach is toward the conclusion) Kwa maana ya kwamba Wana sayansi Na Wana filosofi Kila siku Wana jiuliza maswali magumu kwanini Sisi tupo hapa duniani Na tupo hapa Kwa lengo gani? Majibu wanayo yapata Wana yachuja Na kuyafanyia tathmini Na kuunganisha dot ili mwisho WA siku waweze kufikia kwenye hitimisho kwamba hakika Sisi binadamu tupo hapa duniani Kwa Sababu Moja mbili tatu...

Haya Sasa katika Uzi Huu mimi Nina simama kama mwana filosofi ninae JARIBU KUjiuliza maswali kwanini tupo hapa duniani .

HII ni nadharia yangu namba mbili, Nadharia namba Moja tayari nilisha andikia Uzi hapa miezi kadhaa iliyopita.

Inawezekana Sisi binadamu ni silaha za kibaiolojia "biological weapons" ambazo zimetumwa duniani kama virus wa Kansa Kwa lengo la kui destroy sayari ya Dunia.

Inawezekana HII sayari ya Dunia Ni kiumbe Hai ambacho kipo conscious. Dunia Ina Moyo , Dunia ina Maini, Dunia Ina Figo, Dunia Ina mapafu (inasemekana misitu ya Amazon ndipo yalipo mapafu ya Dunia) Dunia Ina kichwa, Dunia Ina akili nakadhalika..

Inawezekana mamilioni au mabilioni ya miaka iliyopita ilitokea vita kubwa Baina ya Galaxies Na Galaxies (Interstellar war au inter gallactical war)

Lengo kuu ilikuwa ni kuziunganisha galaxy zote ulimwenguni chini ya utawala mmoja.

Almost 99 percante ya Galaxies zote ulimwenguni zikawa conquered (There is a billions and billions of galaxies in the universe)

99 percent ya Galaxy yetu (Milky Way Galaxy )pia ikawa conquered .

Ni sayari Moja Tu ndani ya galaxy ambayo haikuweza kuwa conquered.

Sayari HII ndio HII ambayo tunaishi Mimi Na wewe Na ambayo inajulikana kama dunia ( kumbuka according to my theory Ni kwamba HII sayari ya Dunia kama zilivyo sayari nyingine Ni kiumbe ambacho kipo conscious ( kiumbe chenye utashi Na chenyewe uwezo WA kufanya maamuzi yake chenyewe kama chenyewe kama unavyo weza kufanya wewe unae soma Uzi huu)

Sayari zote katika galaxy yetu zikawa conquered Na zika surrender, sayari zote kwenye planetary system yetu zikawa conquered kasoro sayari ya Dunia ambayo yenyewe haikutaka kuwa chini ya ufalme.

Sababu kuu zilizo fanya sayari HII ishindikane kuwa conquered ni kuwa Na intelligence ya hali ya juu Sana pamoja Na defensive mechanism isiyo Julikana.

Defence mechanism ambayo iliifanya sayari HII ya Dunia kuwa impenetrable and unconquerable.

Kila attempt iliyo fanyika dhidi ya sayari HII ilikuwa foiled.

So ikaundwa kamati maalumu ya ki intelligensia (A SPECIAL INTELLIGENCE COMMITTEE) iliyo wahusisha wakuu WA intelligensia kutoka gakaxies zote kujadili mbinu ZA uhakika ZA kuivamia Na hatimae kuiteka sayari ya Dunia Na kuifanya kuwa sehemu ya ufalme WA muungano WA galaxy zote ulimwenguni..

Kamati hiyo iligundua kwamba sayari ya dunia imeendelea sana kiteknolojia. Teknolojia yake Iko more advanced kuliko teknolojia waliyo nayo muungano wa galaxy zote kwa ujumla.

Kamati hiyo iligundua kwamba endapo sayari ya Dunia itagundua kwamba Ina teknolojia kubwa kuliko muungano wote wa galaxies basi inaweza kuzivamia galaxies zote na kuziteka na kuziweka chini ya utawala wake..

Jambo hili lilikuwa threat kubwa Sana Kwa watawala WA Umoja WA galaxy zote ulimwenguni wakihofia Hatari ya kuupoteza ufalme wao utakapo fika wakati WA sayari ya Dunia kuujua ukweli Huo ambao Ni ukweli sayari ya dunia ilikuwa inafanya upelelezi wa kiinteligensia (clandestine) kwenye sayari zilizopo katika Umoja WA galaxy ili kuhaini nguvu Yao Iko wapi kabla ya kufanya offensive attack (kuivamia)

Kamati iligundua kwamba Kwa teknolojia iliyokuwepo kwenye muungano wa hizo galaxy isingekuwa rahisi kui conquer sayari ya Dunia.

So kitu pekee ambacho wangeweza kukifanya ni kujaribu kuilipua Kwa lengo la kuiteketeza kabisa sayari ya Dunia isiwepo kabisa ili kuondoa potential threat.

So wakakubaliana kwamba sayari ya Dunia ilipuliwe. Je Nini kilitokea? Nakuja kuendelea soon.

INAENDELEA

Hesabu ZA ki intelligensia zika ifikisha kamati kwenye conclusion kwamba ili sayari ya Dunia ilipuliwe basi Ni lazima itumike sayari ambayo IPO jirani Na sayari ya Dunia.

Sayari hiyo ilikuwa Na ukubwa mara Kumi ya ukubwa WA sayari ya Dunia Na uzito mara Mia ya uzito WA sayari ya Dunia so kama sayari hiyo ingesukumwa Kwa Kasi kutoka kwenye orbit yake Na kuelekezwa kwenye orbit ya sayari ya Dunia basi sayari hiyo Inge gongana Na sayari ya Dunia Na sayari ya Dunia Inge lipuka Na kuteketea Na Huo ungekuwa ndio mwisho WA story ya sayari ya Dunia.

SAYARI INATUMWA KUELEKEA DUNIANI KWA AJILI YA KUILIPUA SAYARI YA DUNIA

Wakati sayari HII ikiwa inakuja Kwa Kasi njiani Kwa ajili ya kuigonga sayari ya Dunia ilipuke, sayari ya Dunia kutokana Na kiwango cha juu cha intelligence ilicho kuwa nacho Na kiwango cha juu cha teknolojia iliyo kuwa nayo ikawa tayari imesha dictate Hatari iliyo kuwa inakuja mbele yake, ukubwa wake na suluhisho lake

So sayari ya Dunia ikaachilia vitu mfano WA miale yenye nguvu Na yenye kuvuta kama sumaku.

Miale hiyo ilifanya mambo makuu matatu. Kwanza ili lipua karibu asilimia tisini Na Tano ya sayari hiyo ambayo ililipukia huko huko ilipokuwa kabla haijafika kwenye Anga la Dunia. Sehemu ya sayari hiyo iliyo baki ilikuwa ndogo Sana kiasi hata ingekuja kugongana Na sayari ya dunia kusingekuwa Na madhara makubwa.

Pili miale hiyo ili I capture sayari hiyo ( kama nyara). Intelligensia ya sayari ya Dunia iligundua kwamba sehemu ya sayari hiyo iliyo tekwa ingeweza kuwa Na matumizi mengine muhimu Kwa sayari ya Dunia

So Jambo la tatu ambalo sayari ya dunia ililifanya Ni kuichukua sayari hiyo Na kwenda kuifix Mahali ambapo sio Mbali Sana Na lilipo Anga la sayari ya Dunia.

Kwa kuwa sayari hiyo ilisha Poteza sifa ZA kuwa sayari, sayari ya Dunia ili ifanya sayari hiyo kuwa satellite ya sayari ya Dunia , satellite hiyo ndio Huu mwezi tunao ufahamu Mimi Na wewe.

Sayari ya Dunia ilizitumia nguvu ZA uvutano Kati yake Na mwezi kujibadilisha ama kubadilisha muonekano wake WA ndani au muonekano WA baadhi ya maumbile yake ya asili (nitalielezea hili baadae) Kwa mfano ukaribu kati ya Dunia Na mwezi ulileta mafuriko makubwa Sana ambayo Dunia iliyahitaji Kwa Sababu yalisaidia kubadilisha muonekano wa Dunia kama vile kutenganisha Mabara nakadhalika (Kwa mujibu WA Nadharia hii kabla ya tukio hili Mabara yote yalikuwa yameungana)

(SAYANSI INASEMA HAPO ZAMANI DUNIA HAIKUWA NA MWEZI. MWEZI ULIKUJA BAADAE. KWA MUJIBU WA THEORY YANGU HII NDIO SABABU YA MWEZI KUJA DUNIANI,ULITUMWA KAMA SILAHA, INTELLIGENCE YA DUNIA IKAIDHOIFISHA , IKAITEKA NA KISHA KUITUMIA KWA MANUFAA YAKE)

Back to The galacticos...

Tukio hili lili ufedhehesha Sana ufalme WA muungano WA galaxies. So ukarudi Tena kwenye kamati ya USALAMA NA INTELLIGENSIA ( SECURITY AND INTLLIGENCE CONMITTEE) kujaribu kutafuta suluhisho jingine

Kamati ikaja Na wazo kwamba njia iliyo baki ya uhakika ambayo inaweza kuidestroy sayari ya Dunia Ni kutumia silaha za kibaiolojia " biological weapons" silaha hizi zitakuwa Na Kazi mbili.

1. Kuidestroy sayari ya Dunia from within.( Task HII itakuwa ya taratibu lakini ya uhakika. Kamati iligundua itakuwa ngumu Sana Ku I destroy sayari ya Dunia Kwa haraka)

2. Kutumika kama point of contact Kati ya security agencies wa kwenye Umoja WA galaxies. ( Yani security agencies wa Umoja Wa ufalme WA galaxy watapata taarifa kutoka sayari ya Dunia kupitia viumbe hao. Kwa maana nyingine viumbe hao watatumika kama spies. Zitapandwa chip kwenye viumbe hao, chip ambazo zitakuwa Na direct contact Kati ya Dunia Na security agency WA Umoja WA galaxies.Security agencies WA Umoja WA galaxies wataweza kuona Kila kinacho endelea katika sayari ya Dunia kupitia chip zilizo pandwa kwenye viumbe hao)

So kampuni mbalimbali ZA GENETICAL ENGINEERING zikakusanywa Na ufalme Na kupewa mchongo WA kutengeneza kiumbe kupitia teknolojia ya genetical engineering, kiumbe atumwe duniani kama mbegu ambayo baadae ata evolve Na kuzaliana Kwa wingi Na hatimae kusave purposes ZA ufalme kama nilivyo eleza hapo juu.

Kampuni iliyo shinda Tenda Ni Ile iliyo SEMA kwamba inaweza kumtengeneza kiumbe aitwae DINOSAURI. Kiumbe huyo angeweza kutimiza lengo Hilo la ufalme.

Kiumbe dinosaur ana tengenezwa kwenye maabara kama mbegu, mbegu hizo zinawekwa kwenye comets ( vimondo) ambavyo huja duniani Mara Kwa mara ( sio threat Kwa sayari ya Dunia. The earth is familiar with those comets so haiwezi kuzilipua ) then mbegu hizo zinasafirishwa Hadi duniani Na muda mchache baada ya kufika duniani mbegu hizo au Mayai hayo Yana mature Kisha wana tokea DINOSAURI Na kuanza kuzaliana Kwa wingi Duniani.

Chakula kikuu cha Wanyama Hawa Ni majani , majani ambayo yanapatikana kwenye sayari ya Dunia Na ambayo Ni muhimu Kwa survival ya sayari ya Dunia.

Kwa Sababu ya ukubwa wao Na kiwango cha majani walichokuwa Wana Kula, ilikuwa estimated kwamba baada ya miaka kadhaa mimea yote duniani ingekwisha na automatically sayari ya Dunia ungekuwa destroyed.

Je, nini kitatokea

ITAENDELEA
 
Kwanza nitoe mawazo yangu juu ya kuamini kwamba duniani binadamu ndio mwenye akili kuliko viumbe wengine,mimi siamini kwa sababu sisi binadamu tunaishi kwenye mazingira na hali ya ubinadamu wetu bila kujua hali za utashi wa viumbe wengine.

nawaza unajuaje wewe una akili kuliko mbuzi wakati wewe unamfuga mbuzi kama bosi,unahangaika kumtafutia chakula na maji na sehemu ya kulala ili uje umle,wakati hiyo ndio destiny yake, maana yangu ni hii tunajiona tuna akili wakati hatujui akili na utashi wa ulimwengu wa viumbe wengine,kimsingi binadamu ni kiumbe muoga na dhaifu kuliko wengine, sisi ni watumwa wa mbwa, paka, ng'ombe, mbuzi na nguruwe tunaowafuga kwa kuhangaika huku wao wanastarehe bandani, tunawatafutia hadi majike ya kufanya nayo mapenzi.

Binadamu ni muoga na dhaifu ndio maana kakimbia ziliko mbuga za wanyama kajitanga nao badala akae huko huko apambane, wewe angalia akija simba kijijini watu wanavyojambiana kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi kapuku kama mimi ndani hakulaliki,sasa kama mna akili na nguvu kwanini kijiji kizima kiogope simba mmoja?

Yakitokea majanga makubwa ya kimazingira binadamu ndio mhanga mkubwa wa kwanza kuliko viumbe wengine,maana yake ni kiumbe dhaifu na kitakua cha kwanza kuwa perished in case of calamities, tuache kujisifu ujinga.

Hivi unakuta mtu anafuga paka ambaye hana kazi, zaidi ya kula na kulala kama boss,sasa nani hapo ana akili? Kuna mtu anasema ili akamate panya,imagine sasa hata panya hana shamba wala ghala lakini anakula vyako na huna unachomfanya...hahahahaaa
 
yaani binadamu na simba wote wanakula mbuzi lakini ili binadamu ale mbuzi lazima amfuge kwa kumbembeleza kwa kila aina ya huduma,lakini simba yeye hafugi mbuzi lakini anawala kila akipata njaa...sasa hapa nani ana akili na nguvu kati ya simba na binadamu.

sisi tumewakimbia simba sababu wana akili,nguvu na utashi kuliko sisi..
 
Kwanza nianze kwakukuuliza ulimwengu ni nini?
Afu hao wakuu wa hizo Galaxies ni kina nani hao?
Hafu kitu chochote kilicho agizwa kuharibu vp kiweze kujisahau na kufanya starehe nyingine
Unachokifikiria chief ni matumizi mabaya ya Akili,fikra na muda
 
theory yako inaweza ikawa na na some sort of weakness,na sisi binadamu tukawa na akili kuliko hao viumbe wengine.

Akili ni nini? Kwa tafsiri ya kawaida ni uwezo wa kutambua,kutafakari,kuchambua jambo na kuja na suluhisho la nini kifanyike juu ya changamoto fulani.

Wanyama utashi wao hawaongozwi na critical thinking,wao hufikiri partially tu mfano paka njaa imemuuma zaidi akikosa panya atakuibia kuku wako na kudokoa mboga zako hapo ndio mwisho wa kutatua shida yake ya njaa,lakini binadamu akikosa chakula ndani basi ataenda kuomba kazi kwa binadamu mwenzie ili alipwe fedha kiasi apate kununua chakula,sasa nani hapo ana akili? aliyedhurumu au aliyepata kwa haki?
 
kwanza nitoe mawazo yangu juu ya kuamini kwamba duniani binadamu ndio mwenye akili kuliko viumbe wengine,mimi siamini kwa sababu sisi binadamu tunaishi kwenye mazingira na hali ya ubinadamu wetu bila kujua hali za utashi wa viumbe wengine.

nawaza unajuaje wewe una akili kuliko mbuzi wakati wewe unamfuga mbuzi kama bosi,unahangaika kumtafutia chakula na maji na sehemu ya kulala ili uje umle,wakati hiyo ndio destiny yake...maana yangu ni hii tunajiona tuna akili wakati hatujui akili na utashi wa ulimwengu wa viumbe wengine,kimsingi binadamu ni kiumbe muoga na dhaifu kuliko wengine,sisi ni watumwa wa mbwa,paka,ng'ombe,mbuzi na nguruwe tunaowafuga kwa kuhangaika huku wao wanastarehe bandani,tunawatafutia hadi majike ya kufanya nayo mapenzi.

binadamu ni muoga na dhaifu ndio maana kakimbia ziliko mbuga za wanyama kajitanga nao badala akae huko huko apambane,wewe angalia akija simba kijijini watu wanavyojambiana kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi kapuku kama mimi ndani hakulaliki,sasa kama mna akili na nguvu kwanini kijiji kizima kiogope simba mmoja?

yakitokea majanga makubwa ya kimazingira binadamu ndio mhanga mkubwa wa kwanza kuliko viumbe wengine,maana yake ni kiumbe dhaifu na kitakua cha kwanza kuwa perished in case of calamities...tuache kujisifu ujinga.

hivi unakuta mtu anafuga paka ambaye hana kazi,zaidi ya kula na kulala kama boss,sasa nani hapo ana akili?...kuna mtu anasema ili akamate panya,imagine sasa hata panya hana shamba wala ghala lakini anakula vyako na huna unachomfanya...hahahahaaa
Ur making a very good point
 
But sijasema Sisi tuna akili kuliko viumbe wengine nimesema huenda binadamu Ni silaha za kibaiolojia " biological weapons ambazo zimetumwa duniani kama VIRUSI WA KANSA Kwa ajili ya kui destroy sayari ya Dunia.
 
Hahaha duh nimeishia tu kucheka aisee
 
Great thinker bravo!
💪💪💪
 
binadamu anahangaika kwasababu hiiDunia si asili yake.
binadamu ndiye kiumbe pekee hadi leo anapambana kuyakabiri mazingira hi ni tofauti kimaumbile mwingine yoyote.
 
But sijasema Sisi tuna akili kuliko viumbe wengine nimesema huenda binadamu Ni silaha za kibaiolojia " biological weapons ambazo zimetumwa duniani kama VIRUSI WA KANSA Kwa ajili ya kui destroy sayari ya Dunia.
Sorry hiyo reply yangu ilipaswa kuwa quoted kwa reply mojawapo kwa mkuu Complicator iliyomo ndani ya thread yako.
 
Mzee LIKUD
Ni kweli Dunia imeshajaribu mara kadhaa kujisafisha kutoka kwa binadamu tangia ijue kuwa binadamu siyo kiumbe kizuri.

Dunia imekuwa ikitumia silaha mbali mbali kudhibiti hawa binadamu baathi ya silahaa inazotumia mojawapo ni maradhi

Ilishatunga maradhi hatari sana Bubonic plague, Spanish flue, ebola , na nk lakin huyu kiumbe binadamu siyo mchezo anaweza kuhimili makombora hayo kutoka kwa dunia. mbali na mwilini mwake kuwa na kinga asili dhidi ya maradhi pia kichwani mwake ana akili za kuboost immine system yake artificially.

Binadamu mwaribifu sana anatumia hovyo rasilimali za dunia na kufanya uharibifu mkubwa sana hivyo dunia ikaja na mbinu nyingine kuwagombanisha hawa binadamu kuwafanya wagombanie hizo rasilimali, basi bita ya kwanza na ya pili zika chapwa. Baada ya vita ya pili kuisha mwanasansi maarufu Arbeit eistain alikotiwa akisema hajui vita ya tatu itakuwaje but anachojua ya nne watu watapigana kwa fimbo na mawee.

Hatari sana mazee hii dunia saa ivi ina Coronaa hilii gemu hilii sijui nani atashinda huyo mmdudu wa korona ni swala la mmuda tuu kuja na program ya kuhasi wote itakaowapata lakini binadamu naye fundi ameshahifadhi mbeguu za kike na kiumee.

Tusubiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom