Huawei yaifungulia kesi Serikali ya Marekani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
c597a1a55dfdd6f645028cd01a259b68

Marekani yazuia mashirika ya umma kutumia vifaa vya kampuni kubwa ya simu Huawei.
Kampuni ya simu ya Huawei kutoka nchini China imeifungulia kesi serikali ya Marekani, baada ya kuzuia mashirika ya umma kutumia vifaa vya kampuni yake.

Serikali ya Marekani imezuia mashirika yake kutumia vifaa vya kampuni hiyo kama simu na vingine vya eletroniki kwa madai kuwa, ni hatari kwa usalama wake.Mwenyekiti wa kampuni ya Huawei Guo Ping, amewashtumu wabunge na serikali ya Marekani kwa kushindwa kuthibitisha madai hayo, na uamuzi wa kwenda Marekani umekuwa wa mwisho, ili kupata suluhu.
Kesi hiyo imewasilishwa katika Mahakama mjini Texas na katika utetezi wake, inatarajiwa kueleza kuwa haina ushirilkiano wowote na serikali ya China kama Marekani inavyoadai.
Mbali na Marekani, Australia na New Zealand, zimeweka vikwazo kwa kampuni za nchi zao kutumia vifaa vya mawasiliano na teknolojia kutoka Huawei.
 

yonga

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
1,870
2,000
Wanatapatapa,waendelee kuisaidia Iran kukwepa Vikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui kinachoendelea mkuu hapo huawei wanajua kabisa hawezi kushinda hiyo ila wanachotaka kukifanya legal process zifuatwe huwezi kuban products fulani bila ya kua na evidence yeyote hapa huawei anataka ayaonyeshe mataifa mengine kwamba ni sheria gani au evidence zilizotumika kujudge kwamba huawei ni national security threat kwa USA kwa allies wake tena bila evidence yeyote ile

Hapa huawei anataka mataifa mengine waone hizo evidence kama sio hivyo basi itakua ni unfair competition tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

yonga

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
1,870
2,000
Wanatapatapa,waendelee kuisaidia Iran kukwepa Vikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli USA ndiyo inayo tapatapa haitaki kuona multipolar world

Kila mtu anayefanya biashara vizuri anamuwekea vikwazo hapa inaonekana ameshindwa kufanya biashara ushindani umemshinda kwa kiasi kikubwa na nchi za ulaya zimeanza kumstukia

Mfano kujenga tu bomba la gas kutoka russia kwenda Germany hataki ili tu aje kuuza LNG yake ambayo ni very expensive kwa ulaya

Na Germany imesema haitakubali watajenga tu hilo bomba maana anajua faida zake na yule ndio powerhouse ya Europe na bomba kwa sasa lipo 70%

Juzi Italy imetangaza kujiunga na silk road project ya china ambayo inapunguza karibia nusu ya gharama za biashara kwa sasa marekani alivyosikia hivyo kaanza kumpiga mkwara Italy

One road,one belt (silk) ni muunganiko wa network za barabara,reli na meli na njia zingine za usafiri kuanzia china mpaka ulaya mpaka africa kwa hiyo itafikia kipindi utatoka na gari/train kutoka china mpaka ulaya mpaka africa hapo ita harakisha sana global trade kwa kiasi kikubwa sasa hapa marekani anaona wivu sana china atapata influence kubwa mno na faida pia

kila atakaye ingia kwenye hiyo project anampa vikwazo huko ni kutapa tapa aache watu wafanye biashara kama kashindwa ushindani akae pembeni au ajipange upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 

yonga

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
1,870
2,000
Hakika mkuu
Ubaya zaidi kule china kuna xaomi ambayo ni mbadala wa iPhone ni bei affordable kabisa.

China is iPhone's largest market na sidhani kama apple wako tayari kupoteza soko la watu wengi namna ile

kiukweli China nayo haikwepeki kabisa maana kwa sasa ndio jamii yenye purchasing power kubwa zaidi kuliko hata the whole Europe sasa kama mzalishaji unaachaje market base kubwa namna ile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,862
2,000
Kuna siku iphone zitazuiliwa china,hapa apple watapata pigo kubwa sana hii michezo haihitaji hasira.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakifika uko wanazima Android system kwa simu zote zinazotengenezwa na China
Apo ndio Vita lazima mchina achemke na hana operating system yoyote. Kwa iyo itakuwa aibu kubwa Sana kwa Chinese

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,461
2,000
Wanatapatapa,waendelee kuisaidia Iran kukwepa Vikwazo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hapo marekani ina upper hand, iko na advantage. Walidanganya wakijua hawatakuja kukamatwa.

Cha ajabu huyo CFO wao anaeshikiliwa Canada analeta utetezi wa kijinga kua aliandalia power point slides yeye alikuja tu kusoma na hajui kilichokua kimeandaliwa, ujinga wa namna gani, wewe mhasibu mkuu uandaliwe slides ukazisome bila kujua zinasema nini?

Kwa hapa Marekani atawasumbua, nasikia wanajibaraguza tu kua hapo walipofika marekani haitaweza kuwarudisha nyuma na mambo kama hayo ila wanakiri kua wataathirika.

Marekani sio nchi ya mchezo.

Popolation 300.something million, china 1.3B lakini wanawekewa vikwazo, kweli akili kubwa inaongoza Dunia.
 

Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,461
2,000
Wakifika uko wanazima Android system kwa simu zote zinazotengenezwa na China
Apo ndio Vita lazima mchina achemke na hana operating system yoyote. Kwa iyo itakuwa aibu kubwa Sana kwa Chinese


Sent using Jamii Forums mobile app
WAlitengeneza ya kwao mwiaka kama 5 au 6 iliyopita, inaitwa china operating system, ila hawakutaka kutoa codes, watu wakawaruhumu kua wamecopy open source ya google. China bado dependant kwa kila kitu kutoka west.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom