How to survive a wild Animals?

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,738
Uzi maalum wa kushare pamoja jinsi gani ya kuepuka wanyama wakali kama simba,Chui,Nyoka,Tembo,Mamba n.k......Wataalamu Njooni huku tusaidiane! Kama umewahi kunusurika au kudhurika ndio sehemu yake hii karibuni wote....
 
Mlokole kakutana na simba badala hata ya kutimua mbio na kuingia nyumba jirani , alipiga magoti na kumuomba Mungu amuepushe na kifo , wakati huo nae simba anamshukuru Mungu kwa chakula kilichopo mbele yake . Mshindi akawa simba na mlokole akawa kitoweo cha simba .

Sent using Jamii Forums mobile app
Utani vunja mbavu mkuu kwaiyo mlokole hajaokoka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza ukawa na kiberiti na majani makavu lakini hiyo panic utakumbuka kuwasha ? Omba usikutane na simba nafuu tembo utampiga chenga ya woga ! Ila ukiweza kuwasha moto simba hakaribii , atakaa mbali asubiri uzimike

Asifanye utani na tembo kwa kumdharau unene wake, kitakupata kilichompata yule mpigapicha wa UDOM mwaka juzi, tembo anambio kukushinda wewe.
 
Mlokole kakutana na simba badala hata ya kutimua mbio na kuingia nyumba jirani , alipiga magoti na kumuomba Mungu amuepushe na kifo , wakati huo nae simba anamshukuru Mungu kwa chakula kilichopo mbele yake . Mshindi akawa simba na mlokole akawa kitoweo cha simba .

Sent using Jamii Forums mobile app
Imani ni kitu kingine kuna bwana alishushwa kwenye Fuso ilikuwa inaelekea Katavi kutokana na kuwa na nauli katikati ya pori lakini alitembea kwa miguu kurudi Inyonga usiku ulipofika akalala chini ya mti baada ya kusali mpaka kulipokucha alikuwa anawaona Chui na Simba anasimama wao wanaondoka na yeye anaondoka

Hakuwahi kusema akimbie roho ilikuwa inamkataza.
 
Mi njia kubwa niijuayo kwa wanyama weng km simba, chui na wengne jamiii hio ni kuwakazia macho (naongea kwa ushuhuda),

NOTE: hapa sizungumziii faru wala mamba,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom