Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,353
Yvonne K. Fulbright Ph.D.
https://www.google.co.uk/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=1&cad=rja&uact=8&ved=0ahUKEwiqiO_9guPOAhUpIsAKHfZJCdYQFggcMAA&url=https://www.psychologytoday.com/blog/mate-relate-and-communicate/201311/how-handle-your-monster-in-law&usg=AFQjCNGli_WZiIQTnATtCOGQ6Ttdzzuowg&sig2=q4878lp7-AYFeUugKpO2SA
Nimekutana na hii habari katika pita pita zangu za leo, imeandikwa na Yvonne Fulbright, mwanamama mwenye PhD. ya pschology. Tatizo la kuishi na mama mkwe mkorofi liko karibu katika kila jamii. Mara nyingi anaona kwa malezi bora aliyompa mwanae ni kama wewe hustahili kuwa mke, mama wengine wanasahau kuwa na wewe mwenyewe unajitahidi uwezavyo kuwa sehemu ya familia yao na kuwa huko ulikotoka, malezi na makuzi yako yalikuwa tofauti kabisa. Fulbright anaeleza kuwa pia ni vizuri kuangalia tatizo liko wapi, angalia uhusiano wa mama na mtoto wake kabla ya kuja kwako wewe, inawezekana mama anaona umechukua mapenzi yote ya mwanae na yeye ameachwa mpweke.
Fulbright anausia kuwa, hata iweje, usipoteze uhalisia wako, kuwa wewe na ujaribu kumuonyesha kuwa una misimamo yako, pamoja na heshima yote utakayompa. Pia ni vizuri kuwa na "muda wa mimi". Muda huu utakusaidia kutafakari au kusahau kwa muda unayopita.
Jambo la mwisho ni vizuri kama mwenza wako atakusaidia kutojiingiza sana kwenye maswala ya familia, siyo kila linalotokea ndani anakwenda kumhadithia mama yake, na upande wako pia. Ndugu wakifahamu machache kuhusu ndoa yenu ni kheri. Pia uelewe si kila utakalo lifanya litapendwa na wakwe zako, ukiwaonyesha misimamo yako, tangia mwanzoni, wataelewa kuwa unamaamuzi yako ambayo hayawashirikishi wao.