how to get the ring.


Kwa hiyo Kongosho kama nimekusoma vizuri crritical analysis yako, kuna aina nyingi za mahusiano ya kingono kati ya mwanamke na mwanaume......mengine ya kindoa na mengine sio ya kindoa,.,,,I mean ya timeline na yasiyo ya timeline, ya good time na yasiyo ya god time ila yanaelekea kwenye uwife na ozbend material (Paloma upo)

Sasa basi mtuwacheeeeee.......maaana wanawake wajue pia kuwa sio kila mwanaume anapokutokea anataka NDOA na wewe ....hapana....au RING sijui...kwani ulingoni apo?

CC Asprin cacico Kongosho Fixed Point AshaDii
 
Last edited by a moderator:

yaani kongosho wewe ndio umenielewa haswaaaa nilipopataka. timeline kama mahusiano yenu mnaona yanaenda vema na hakuna kizuizi chochote cha kuelekea kwenye ndoa, mnapooana mnaweza kujiachia zaidi na kufanyiana mazuri zaidi. kama upo kwenye mahusiano ambayo kila siku ugomvi, unadate na mke/mume/mpenzi wa mtu mjue timeline haiwahusuu.
 
kweli, hata wanaume wanaokuja kwa gia za ndoa huwa wanaogopwa kama njaa.


kumbe huwa mnawaogopa eeeeeeh!?,,,,,,,,,,,,

ila wewe unadhani mtu kama amelelewa kwenye maadili maisha yote atakuja kwa gia gani bishosti?,,,,,,,,, hapo ndiyo linapokuja suala la kila mtu kuanzia mwanzo tu awe na mtu wanayeendana vinginevyo ni full majanga,,,,,,,,,,, umeshawahi kusikia "yule fulani ni mzuri na anamaadili mazuri lakini maskini sijui ni mkosi kila anayekuwa naye baada ya muda anamtosa"
 

Hapa nadhani unaogopa matokeo ambayo hata huyajui

I disagree

Mungu hahusiki na haya leo
Mungu ameweka kanuni basi
Zifuate nawe utaona matokeo mazuri!!!!
 
yaani wadada wa siku hizi mtu yoyote akipropose ndoa kwao jibu ni yes! kisa ndoa ndoa! aonekane ameolewa! aya bwana! mi napita tu
 
mbona una dalili za kuchakachua hii yuziful thread!

Nope!
Unataka kuanzisha mambo yakoeeeeee!!!!!!
Hatuko parokiani hapa....lol!

Tasavali usichakachue hii yuzfull siredi!!!!!!!!
 
Off course, si kila mwanamme anapokuomba tundi anataka ndoa
Na si kila mwanamke anapokubali kutoa tundi anataka ndoa


Sasa mke wa mtu na mme wa mtu wameombana matundi kwenye semina bagamoyo, hao nao wanatarajia ndoa? Au mke wa mtu/mme wa mtu kaombana tundi na single, nao watarajie ndoa?


Hata singles wote wawili wanaweza ombana matundi lakini aidha mmoja wao au wote hawaoni wanafaana kuishi pamoja, hapo napo utarajie ndoa?


Hadi wote wawili muone mnafaana ndio mtatarajia ndoa, hakuna mtu anataka kuishi na mtu asiyemfaa kwa aina yeyote. Ni hadi utakapoona anakufaa ndio utawaza ndoa.

Usikubali kuombwa ndoa wakati misismamo yako uliitangaza kuanzia awali, ni kupasuana vichwa tu.

 
yaani nimeipenda comment yako maana naona sasa umeweza kuyatazama mahusiano kwa jicho la tatu. safi sana, najua usharuhusu moyo wako kupenda tena. lol
 

Smile apo bold umenikumbusha le mutuz.....hahahaaa....sasa basi kama unadate na mtu ambaye hataki kuoa...u know ur options eeh>:shut-mouth::shut-mouth:
 
Last edited by a moderator:
Kuna jambo ambalo naona watu tunasahau hapa, hivi ni kila mtu unayetoka nae anafaa kumake life nae?? and hata hizo timelines mnazozisema hazina determinants??

najaribu kufikiri by then natoka na mtu je kila nlokuwa natoka nae labda kwa miezi ama miaka aliqualify kuwa material husband?? ama mimi niliqualify kwake kuwa material wife??

the first thing ni wewe mhusika kujiassess if at all kwamba una qualify kuwa material wife kwa muhusika before even assessing him. unapotaka kuset timelines za ring lazima kwanza uanze hapa.

and one good thing men are pple creatures ambao once wakimwona material wife huwa hawataki kumwacha manake they are afraid to loose. wala huta anza kuclaim for the ring mwenyewe atakuambia twende tukavae pete
 
nimekumiss shemeji

mi pia shem Smile, lakini kumbuka

"Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Ila mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii ili amridhishe mumewe..."... 1Kor 7: 25-34"
 
Last edited by a moderator:


Thats ma gal gfsonwin......smart!
 
Last edited by a moderator:

tunawaogopa ndio, haiwezekani watu hamjafahamiana vizuri hamjui hata kama mtaendana aanze kutangaza ndoa. kwanza mwanaume wa hivyo atakuwa na kasoro zake. lol wizi mtupu.
 
Kongosho yupo sahihi kabisa, siyo kila mahusiano ni ya kuyadaia pete....
kwa upande wangu (ingawa inawezekana kabisa mimi siyo mfano mzuri sana) pete inatakiwa ije tu, kama huyo mtu akiona ameridhika na anatamani kabisa kuwa kwa muda wake wa kuishi uliosalia anataka kuwa nawe basi akuulize kukuoa. na kama ilivyo huwa inatakiwa liwe swali, akuulize kama unapenda kuwa naye katika maisha yenu yaliyosalia, mwanamke pia anaweza akakubali au kukataa kulingana na jinsi ambavyo anaona anamuhitaji huyo mtu.
mambo ya kuulizana utanioa lini? au mbona hueleweki/husomeki....... ndo yanazuaga yale ya kutosana au kuoana mkaishia majutoni
 
Last edited by a moderator:
yaani wadada wa siku hizi mtu yoyote akipropose ndoa kwao jibu ni yes! kisa ndoa ndoa! aonekane ameolewa! aya bwana! mi napita tu

wenyewe wanaita kuondoa mikosi, lol. tatizo kufata mkumbo fulani kaolewa.
 

Kwa maelezo yako haya inaonekana kwenye mahusiano mengi hakuna mawasiliano
Kama mna mawasiliano kuna mambo yatakuwa wazi kwenu
Kuna haja mwanzo wa mahusiano mkaelezana mnakoenda ili kila mmoja ajue mankoenda

Sio mnapanda basi moja mwingine anajua linaenda Uru kishumundu wakati mwingine anajua linakwenda Sango mjoroni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…