Mwandishi wa habari hizi ni mjinga asiye na elimu. Jeshi la Tanzania limekomboa Comoro juzi juzi hapa yeye anadai hatujaingia kwenye action for more than 30 years. Tanzania imejihusisha na amani ya Sudan, Somalia, Lebanon nk na kote huko Jeshi letu limeingia kwenye action na kufanya vizuri.... Asubiri aone. Habari hii ni ya uzushi tu!!
Mkuu hapo kwenye RED kuna walakini...!
- Sina hakika kama kweli huyu mwandishi ni "Mjinga na asiye na elimu" kama unavyodai; Ukitafakari kwa makini utagundua kuwa hii vita ya msituni anayoongelea ni rahisi kabisa kwa jeshi la Tz na hilo la SA kushindwa na hao M23. Uzoefu umetuonyesha jinsi wataleban walivyowaangaisha wamarekani japokuwa wamarekani wana vifaa na teknolijia za juu kabisa! Mfano mwingine ni Israel Vs Hizborah.
- Si kweli kuwa majeshi ya UN uko Sudani au Lebanon yanakuwa kwenye Action. Ulizia vyema hao askari maarufu kama "Blue helmets soldiers" uwa wanaingia katika mapigano au wao ni kutunza amani? Hata DRC walipopewa mamraka ya kujibu mapigo hatukuona lolote zaidi ya M23 kujitwalia maeneo.
Jifunzeni kutoka Afrika ya kati (CAR), ambapo waasi wametwanga wanajeshi wa serikali wanaosaidiwa na nchi kibao ikiwamo SA. Kuliko kwenda vitani ni bora wakamfunze Kabila jinsi ya kujenga jeshi la kulinda nchi yake!