Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,653
Asante Kidatu kwa moyo wako wa uzalendo; lakini vibaraka wa maadui wa nchi yetu hii wana historia ndefu sana; na ukipenda hata uvamizi wa Iddi Amin kwa nchi yetu usingefanikiwa kama waliokuwa kule mpakani wangekuwa wazalendo wa kweli. Baadhi ya watanzania wenzetu walimuunga mkono Iddi Amin kikamilifu na hata kuyashangilia majeshi yake yalipokuwa yanaliteka eneo la Kagera ingawa baada ya kutimiza adhma yake ile aliwageuka na kuwaangamiza kwa maelfu! Walikuwa wakijiita eti Waganda Kyaka. Kwa hiyo usiwashangae sana wakina EMT kwani kwa namna wanavyoweka hoja zao wanathibitisha kuwa na asili ya Rwanda au ni miongoni mwa maelfu wa Wanyarwanda waliojipenyeza na kuishi nchini kama wananchi lakini mioyo yao iko Rwanda! Wapo wengi wa namna hii na wanashika hata nafasi nyeti kabisa ikiwemo Ikulu!
Haya tueleze we mwenzetu una damu ya Kongo mikononi mwako kwa namna ipi?
Tatizo ni kwamba baadhi ya wachangiaji katika mada hii wanajilazimisha tu kuchangia au wanachangia kishabiki bila kuwa na ujuzi wa kijeshi kama ndugu yangu Mtazamo. Ukweli ni kwamba South Africa walikuwa kule na mission moja tu, ya kulinda amani. Hawakuenda kimapigano. Na nakuhakikishia kwa uhakika kwamba hata leo hii wakiamua kwenda kimapigano hao Seleka hawawezi kuhimili vishindo vya wa South hata kwa wiki mbili!
Well said Mkuu, I've been against most of CCM and Kikwete's policies and how they run this country; but I fully agree with his decision to send our troops to the DRC. Many of us underestimate the gravity of the problems in the eastern DRC but the fact remains that Tanzania will never be secure if there's insecurity in the harbouring neighbourhood as it is the case with the DRC. Tanzania currently hosts well over 72,000 refugees from the neighbouring DRC. The side effects of this huge refugees influx are worse than spending moneys to prevent them from pouring into our territory; ecological demage, incresed acts of crime and armed banditry are some of the known effects.
timbili, sifahamu umri wako; lakini hapo kwenye grey bold si kweli unachosema labda kama umesimuliwa vijiweni. Ukweli ni kwamba JWTZ ilihusika kikamilifu katika counter insurgency war kule Msumbiji miaka ya 1987/88 hadi kuhamasisha usitishaji wa vita na kusainiwa mkataba wa amani kati ya Renamo na serikali ya Msumbiji ambayo ilikuwa imeelemewa vibaya na waasi wale waliokuwa wakisaidiwa na Afrika ya Kusini ya Makaburu. Na hapo penye blue bold; inasikitisha sana kuwaponda kiasi hicho wapiganaji wetu waliohatarisha maisha yao kwenda kufanya kazi ngumu kiasi vile! Ukweli ni kwamba haikuwa kazi rahisi kama mnavyoelezana vijiweni, ilikuwa kazi ngumu na ndiyo maana baadhi ya nchi zilizokuwa zimeahidi kushiriki zilikacha dakika za mwisho na kuiachia Tanzania jukumu lile! Upo ukweli kiasi fulani kwamba mmomonyoko wa maadili uliopo nchi nzima umewaathiri pia wanajeshi wetu (Maana wao pia ni sehemu ya jamii yetu) lakini nasema Tanzania ina uwezo wa kufanya mabadiliko kidogo tu na ku-immobilize resources zake na kuendelea kuwa Jeshi imara kabisa.
Mwamunyange ni mmoja wa makamanda waliopigana vita vya Msumbiji !............madogo wengi humu hawajui. KAMANDA WAO AKIWA ...............AAAH HUYU ALIYEKUWA WAZIRI WA SERIKALI ZA MITAA .......AAHH HUYU MSAMBAA WA LUSHOTO - BRIGEDIA GENERALI ............!!:heh::heh: