How can you let it go? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

How can you let it go?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kitty Galore, Aug 5, 2011.

 1. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Aliyekuwa boyfriend kaoa tokea January this year, lakini nimeshindwa kuabsorb hii hali, mbaya zaidi tunaishi mji mmoja so mara nyingi namuona. Wadau kama ilishawahi kukutokea, ulichukua hatua gani kuiona ni ya kawaida. Najua maisha lazima yaendelee lakini duh, roho inauma jamani, the thing is haunting me badly.
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Pole sana. Lakini tangu January mpaka sasa ni miezi karibu nane sasa. Unatakiwa kuamini kilichotokea, jishughulishe na pia jichanganye na watu wengine pia. Kama unaweza kuepuka kutembelea sehemu ambazo yeye anatembelea mara kwa mara pia inaweza kukusaidia kumsahau kirahisi. Inawezekana hata namba yake ya simu bado unayo na pengine wakati mwingine huwa unashawishika kuwasiliana naye japo kwa text message. Nakushauri uache hilo na uanze maisha mapya!

  Pia epuka sana hali ya upweke.
   
 3. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kubali matokeo na kuamini kuwa wako wa moyoni anakuja. Kisicho ridhiki hakiliki hivyo riziki yako ipo tu wala hamna aja ya kuumia roho.
   
 4. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mawasilino nilishakata sihitaji tena,namba ya simu ipo kichwani kuifuta sitaweza, maeneo yote tuliyokuwa tunaenda nayaepuka na zaidi anaonekana maeneo hayo na mkewe, hili ndio linalotaka kunitoa roho, kwa kiasi nilichokuwa nampenda naona kama ndio kwanza kaoa jana.
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Adele ---- Someone like you..

  Perfect song for you....

  Sikiliza maneno yake ..
  utafute ( you tube )..
   
 6. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kumtoa moyoni si kirahisi hivyo, asante kwa ushauri lakini kama binadamu ni ngumu kuikubali mara moja
   
 7. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  ...bi mdada we ulikosea nn mpaka jamaa akaoa msichana kwingine?...
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  potezea bana,...utaumia mpaka lini,..anyway ebu tuambie ilikuaje akaoa mtu mwingine wakati wewe unampenda,...au kuna sehemu uliteleza,.....kubali matokeo maisha ndivyo yalivyo....kama vip hama mtaa
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Najua inavyouma(nimewahi kupita hiyo hali) kwa mtu uliyempenda then mambo hayakwenda kama mlivyopanga,inauma,hauna raha,unaweza uambiwe jichanganye na watu na ukafanya hivyo still ukahisi ni yeye tu!kwanza kubali that Not every relationship means to last forever,ndo maana mkadate to know each other!

  Kubwa usiwasiliane nae hata kidogo hata kama unajihisi vipi ni dawa ya ajabu,then unaweza kumwambia asikupigie simu na ww utakuwa umeshiriki kujiondoa kama yeye!tell him u hv come to the conclusion that its impossible to stay in contact with him and recover from the breakup at the same, you need time and space for yourself ,so respectfully ask him to not contact you in any way what so ever.

  Mche Mungu omba,ukiamka asubuhi sema asante Yesu maana unanipenda na ninakutumainia wewe tu ,sikiliza nyimbo zitakazokuinua zozote,kama ingewezekana jaribu kumkwepa kwa namna yoyote,KUWA NA MATUMAINI YUPO aliyeandaliwa kwa ajili yako, NAKWAMBIA YUPO TENA NI MWEMA NA MZURI KWELI! Jua kwamba never person alone is responsible when relationship fails, Mungu akuinue!
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Igwe hilo alilolifanya ndio linamfanya aumie zaidi maana she was expecting so much to be married by that guy ila kachemsha mahali mambo yamemgeuka.
  Ishatokea na kuifuta huwezi so vumia tafuta wako uendelee na maisha
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Mmekutana nae Januari tu na kishakumwaga na kuoa mwingine,ujue huyo alikuwa hajatulia.Ni ajabu pia na wewe kuwa unammiss mtu uliyekaa nae kwa muda mfupi hivyo,wapo watu wanatoswa after 5 yrs +.Pole.
   
 12. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  nadhani kama watu wazima mnaelewa jambo kama hili katika maisha hutokea, ni kwamba tulitengana kidogo shauri ya majukumu(kikazi) mimi nikawa mbali nae, kurudi kila kitu kimeharibika, haeleweki na mwisho wa siku nikasikia anatangaza ndoa, so mambo kama haya hutokea, tatizo linakuja ni kwenye kukubali ukweli, ndio maana naomba waliopitia wanipe experience zao, walilipokeaje
   
 13. K

  Kipenzi Chao Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana mamiii....! Ninavyoamini mimi ni kwamba kambi zingine zote zinaweza kuvunjwa kwa amani na zikavunjika milele...! Lakini sio kambi ya mapenzi...! Hivyo, inaonekana kambi yenu mliivunja kwa amani mkiamini kuwa inawezekana, na sasa uhalisia unakushinda....! Wahenga walisema usinyee kambi, lakini sio ya mapenzi...! Makosa uliyoyafanya ni haya;
  1. kuachana na boyfriend wako kwa amani, na hata kama mlikorofishana kidogo basi mlisuluhisha na wewe aidha ukatoa msamaha wa dhati, au ukadhani umesamehewa kwa dhati....!
  2. Ulisahau kuwa kila wakati unapotaka kuhamia kambi mpya, ni lazima umalize kuijenga kambi hiyo kabla ya kuibomoa kambi ya sasa....! Hivyo, wewe uliridhia kuachana na mwenzio wakati wewe bado hujajua unakoenda....!
  3. Vinginevyo, ulishindwa kusoma alama za nyakati kuelekea kuachana kwenu....!
  Kwa mtazamo wangu waweza kufanya yafuatayo;
  1. Tengeneza mazingira ya kugombana na ex-wako. Ni lazima utokee ugomvi usiosuluhishika katika maisha yenu ya hisia za mapenzi....!
  2. Jaribu kuwa na "Peace of Mind" na uridhie kuwa wa pili....!
  All the best.......!
   
 14. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  soma thread vizuri sio kukurupuka, nimesema kaoa January, sijasema nilikutana nae January
   
 15. charger

  charger JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Pole Kitty its not easy to accept this kind of truth,but what you ve to keep in mind is "that man wasnt yours" na pengine Mungu kakuepushia mambo mengi tu.The thing is we can not see the future but God can.Just go on with your life,and thank God fo everything,soon or later utapata ur perfect man.
   
 16. JS

  JS JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ulimfanyaje KG?
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kama aliweza kukuacha baada tuu ya kutengana kikazi na alikuwa na guts za kutafuta mwanamke mwingine behind your back na kutangaza ndoa jua kwamba hakuwa na mapenzi ya dhati na wewe.
  Hayo ni mapito ameshaoa na ana familia yake now muombe Mungu akupe wako. Sahau na jipe muda wa kufikiria maisha yako na sio yeye tena. Hawezi kurudi kwako wala hawezi kuwa wako tena. Na tena ukiruhusu hayo mawazo yaendeleee unampa nafasi ya wewe kukutana na nae siku moja na akakurububi mkumbushie uhusiano wenu japo unajua kwa hakika ana mke
  Kama unafanya kazi fanya kazi jichanganye na marafiki, nenda sehem ambazo hamtokutana, tengeneza mazingira ya kutomuona kama mpenzio tena ila msahau katika maisha yako.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Pole sana, vumilia tu utasahau kila kitu!
   
 19. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  I feel you. Mimi kuna sehemu nilikuwa sifiki kabisa kwa kuwa ilikuwa inanikumbusha maumivu. Lakini baada ya kusamehe na kusahau nakwenda muda wowote ule kwa sasa.

  Time is the best healer. With time utazoea tu na kuona ni hali ya kawaida.
   
 20. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  ''Seriously, evict all those tenants living rent-free in your head. I know I say it a lot. Just ONE grudge can hold you so far back! Unforgiveness might be the reason that one door remains shut! You're too blessed to be petty and bitter. Stop those monthly and yearly pity-parties, "Oh!! Oh! Oh! It's exactly one month since XXX did abcd... last year at this time XXX said defg..." Stop. Forgive, for YOUR sake!'' - I liked this post in facebook.
   
Loading...