Pundamilia,
maneno yako msumari mkuu wangu hapa kula zako 5..
Kuna kitu nilitaka kukiongezea tu kuhusu Watu na Mazingira..mtanisamehe natoka nje ya mada kwa sababu inauma sana kusikia ATCL inatarajia kuruka hivi karibuni na hakuna mabadiliko yoyote zaidi kuwa bailed out, with no string attached to it!..ATCL bado ni shirika la serikali hivyo siasa juu ya biashara kama kawa... imefunika!
Unajua mkuu wangu sisi waafrika na hasa Watanzania tuna kasoro moja kubwa sana ya URITHI..
Sisi ni watu ambao urithi tunauchukulia kama vile ni radhi ya mzazi kiasi kwamba mzazi anaweza kwenda kaburini hakumrithisha mtu au kumrithisha mtu wa nje kabisa maadam tu awakomoe watoto na ule msomo Na wewe tafuta za kwako!..
Wazee wetu hata kuandika Urithi (Will) hawataki kwa sababu sio mila yetu na pia kwao will ndio kwanza kutabiriana mauti.
Hivyo utamkuta mzee ana mali, tuseme tajiri kwa kuagiza vipuri toka nje lakini contact zote anazo yeye mwenyewe, mwanaye wa kumzaa hajui baba yake anaunganisha vipi biashara zake zaidi ya kukaa dukani kuuza mali zile..Ukimuuliza mzee jibu utakalo pewa ni bora usingeuliza..Kikubwa wanachoweza kusema ni kujisifia jinsi wao walivyoweza kufika pale walipofika kuwa wame suffer kichenzi.. Now, jiulize wali suffer kwa ajili gani hakuna zaidi ya maisha yao wenyewe as individual..hivyo vita yake kupata mafanikio inaishia pale yeye alipokuwa tajiri..Bila wao kufahamu au wasijali kitu kuwa at the end of their life, wakisha kufa mali zao hupotea na pengine ndugu, marafiki na jamaa kugombania mali zile kama pilau la msibani.
Ni ktk mtazamo kama huu nimeona hata Uongozi wa nchi zetu umekuwa ktk mila na desturi kama hizi. Kuna fundo la kimeo kati ya wazazi (viongozi) wetu ambalo sifahamu limetokana na kitu gani.. sijui kama ni roho ya kwa Nini!...au pengine umaskini wa hali na mali ndio umechangia zaidi..
Kuna watu hunambia pengine Tanzania tulipata Uhuru haraka sana kabla hatujawa na wataalam wa kutosha kuweza kuendesha mali zetu lakini binafsi sidhani kuwa hii ni sababu ya msingi... Kwani walimu wetu walitakiwa kuwa wazazi wetu wenyewe sio Mkoloni..
Tazama nchi kama South Afrika, Zimbabwe, Msumbiji na nchi nyingine zilizotawaliwa kwa muda mrefu bado kunamatatizo makubwa ya Utawala wa mtu mweusi unaposhika nchi..hawa wenzetu wametawaliwa zaidi ya miaka 500 lakini ngozi nyeusi ilipokamata tu chumi za nchi hizo zimeyumba au kuporomoka...
Sasa hujiuliza ingetuchukua sisi miaka mingapi chini ya Ukoloni ili sisi tufikie uwezo mkubwa wa kitaalam na nidhamu ya kazi na kuwa responsible..Jibu la haraka ni kwamba hata kama ingechukua karne 1000, tusingeweza kitu kwa sababu Uhuru wetu ni sawa na mtumwa aliyeachiwa huru ghafla bila kujiandaa na dunia ya nje, hivyo haijalishi ni miaka mingapi mtumwa huyo alikuwa katika Utumwa iwe mwaka au karne nzima isipokuwa transition ya mtumwa huyo ndiyo Muhimu sana katika kumwezesha mtumwa huyo kuhimili ya dunia hiyo anayokwenda...
Ni imani yangu kuwa Wamarekani weusi pamoja na kwamba wamechukua miaka mingi kufika uhuru waliokuwa nao leo au niseme hapa walipo lakini kuna kheri nyingi zimetokana na slow transition ya haki zao hatua kwa hatua.. Kwanza Uhuru wa US, kisha utumwa, ukafuata ubagulizi wa rangi -social integration..wakapigania haki za msingi kama elimu, afya, usafiri, makazi na all human rights ambazo kwa nguvu ya kutafuta haki hizo waliweza kupandikiza fikra na urithi wa wazazi wao.
Fikra toka kila hatua ya mapambanoo yao...Toka Du Bois, Fredrick Douglas hadi kina MLK, Malcom X, Kunta Kinte ni historia ambazo zimekuwa honoured na passed through generations hadi leo hii wana viongozi kama Obama..Every step forward kulikuwa na hatua in stages tofauti na sisi tulipotaka Uhuru tu tukapewa kama yule mtumwa..Hivyo aidha hatukujua tufanye nini na Uhuru huo ama ndio yale yale ambayo mimi husema kuwa ni Sinia la Pilau siku ya Kisomo (Hitma).. nikiwa na maana watu wenye njaa ukiwawekea sinia la Pilau pamoja na kwamba siku hiyo ni ya huzuni kubwa ya kufiwa (Hitma) utashangaa watakavyo weza gombania matonge na hakuna utaratibu wowote ule unaoweza kutumika kuwapunguza kazi hawa watu...Pale kila mtu na mzigo wake..
Hii ndiyo hofu yangu kubwa sana na taifa letu, sio tu kwa kuitazama ATCL bali utawala mzima wa nchi yetu(zetu)..Hatuna role model, watu kama Nyerere leo hii tayari tumekwisha watafutia mabaya yao. Kina Mkwawa, Mirambo, Mangi Sina na wengineo, hawa wote tuna taarifa nyingi za mabaya yao kuliko mazuri kuhusu historia za maisha yao, fikra zao na kadhalika.. Yote mazuri yamekuwa kuwa flushed na tutabishana sisi wenyewe utafikiri hatuna akili..matokeo yake leo hii hatuna wa kumtazama kama mfano bora isipokuwa Western World (wazungu) na mashujaa wake..
Mashujaa tuliokuwa nao (wanaotambulika) ni watu waliopanda mlima sijui Mt. Kilimanjaro, kukimbiza mwenge, waliotembea kwa miguu kuunga mkono Azimio la Arusha na mengine mengi ambayo kusema kweli hayamsaidii mrithi Mdanganyika aliyezaliwa ktk Umaskini. Haimuingii akilini huo Mlima au mwnge utaweza vipi kuondoa njaa yake ama kumpa tumaini la kesho kuwa mbora kati ya wabora..
Mkuu wangu inasikitisha sana, na hasa pale napoona kuna uwezekano mkubwa wa nchi yetu kwenda mbele lakini tunarudi nyuma kwa sababu We have no history, no one or nothing to look up to!..except Abroad..Na utamaduni wetu umekuwa kikwazo cha maendeleo yetu na yawezekana kabisa adui mkubwa wa maendeleio ya Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe..Yaani Umaskini ndio adui mkubwa wa Umaskini..
Siasa za kuokoteza na kupachika kama viraka ndizo zimekuwa muundo wa fikra za Mdanganyika..It's about Mtumwa na Nyapala na kila maamuzi ya kitaifa utaona ni vitu ambavyo zinakuwa forced to the society.. Leo, Mama Clinton ameapishwa lakini umeona cha moto amekipata kutokana na Mumewe kuwa na NGO yake..Hakuapishwa bila kupitiwa na baraza la nchi hiyo..Sisi ndio kwanza mtu akichaguliwa na rais basi kapita na he become untouchables the very first day!..
I hope, Kikwete ataweza kuyasikia maoni yako na pengine kujaribu mwongozo mpya wa Taifa letu.. na wananchi wenyewe kujielemisha zaidi ktk ujenzi wa Taifa letu kwa kuelewa mapungufu yetu.. Badala ya kwenda kujifunza kuendesha baiskeli (Elimu yetu) tujifunze kutengeneza baiskeli..hata tukianza na zile spokes au baiskeli inayorudi nyuma..Kwa sababu nimechoka na elimu zetu tunapojisifia kuendesha baiskeli, jambo ambalo kusema kweli sio elimu isipokuwa ni mazoea tu..