Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 58
Mkuu nimekusoma.. Hizi ni Option tatu ambazo zinaweza kuchukuliwa... na sisi hapa nadhani tunajadili na kubadilishana mawazo kipi kizuri kinachoweza kufanyika..Kitu ambacho kinaweza kufanyika ni mwenye mali sasa hivi kwa maana ya serikali kutafuta mbia ambaye watajumuika kuiendesha ATCL endapo serikali itaona haiwezi kubeba mzigo wa risk at 100%.
Baada ya hapo endapo kampuni itaanza kutengeneza faida kutoka katika operations zake (Operating Profit), kuweza kuonesha kuwa kunauwezekano wa faida kuongezeka na kuimarika kifedha nk, then
hapo hisa zake zitaweza kupanda thamani na kuuzika.
Au njia nyiingine ni serikali kubaki peke yake na kufanya mikakati ya kuliimarisha na hatimaye kufikia kiwango cha kuridhisha kuweza kupata faida nk kama nilivyoainisha hapo juu.
Au njia nyingine serikali kuiuza ATCL kwa mmiliki mpya, lakini katika hali ilivyo sasa ATCL atakayenunua ndiye atakaepanga bei.
Iuzwe tu! Mbona waSwiss na waZambia wameweza? Pesa zitakazookolewa ziwekweze kwenye usafiri wa reli! Tuongeze tracks na twende kwenye umeme badala ya diesel.
Amandla......
hata sisi tunaona hivyo hivyo isipokuwa ATCL kama shirika sasa hivi inahitaji msaada kuwa bailed out..Ondoa kabisa mawazo ya hao viongozi... ktk issue hii..chukulia kama hakuna mtu hivi sasa.wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi
...wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi
...wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi
Pundamilia,
Mkuu wangu mashirika mengi nchi hizi yameingia Public yakiwa hayana sifa kubwa ya faida isipokuwa future yake ndio inawafanya watu wacheze kamari. Wall street mkuu wangu ni kamari na mara nyingi wenye kuona mbali ndio hufaidika na pato litakalotokana na uwekeshaji..Ktk mfumo huu wa soko kuna Uwazi na Accountability..hivyo agharab kesho kuanza kuulizana ilikuwaje?
Kinachotakiwa kuwavuta wawekeshaji ni mpangilio wa shrika zima kimalengo na matumaini, hali ya Usafiri wa anga sehemu hiyo, connection za kwenda nje na kadhalika..Hata Google na mashirkka mengi humu tumewekesha yakiwa hayana faida kabisa mengine yameingia Public ili kupata myaji tosha wa kuweza kuendelea iwe kutokana na mtaji mdogo demand kubwa..
Sisi Wawekeshaji tunatakiwa kusoma alama hizi na sio kusubiri hadi umeskia shirika la Bia linaingiza fedha kuliko yote ndio uingie, Au Barriccks ni shirika kubwa la kuchimba dhahabu ndio uingie.. Wajanja wote huingia mashrika madogo yenye kuuza share zake chini wakijua kwamba biashara hiyo itakuja panda..
Yes, nikirudi ktk WATU na MAZINGIRA nakuelewa sana kwa sababu hata biashara ndogo Wadanganyika husubiri mtu mmoja aanze, wakiona inaingiza fedha ndipo wote wataivamia.. kama kwenda China...Yet hii isiwe sababu kubwa kama wasomi wapo na watu wanaotakiwa kuwekesha ATCL ni wenye uwezo ambao nina hakika wana wataalam ktk maswala ya Uchumi na mazingira yetu.. Location na soko letu (demand) ambalo halina ushindani zaidi ya Air Precision ni kubwa sana hasa ukizingatia Population yetu. Hata kama asilimi 10 tu ya wananchi wana uwezo wa kupanda ndege ni mauzo ya ticket millioni 3 kwa mwaka..nauli zetu ni kubwa kuliko North America na watu wanadai usafiri wa anga kila siku utaambiwa ndege imejaa..
Pili, kivutio kingine kikubwa kuungana na mashirkka hayo aidha Emirates au Gulf na asikudanganye mtu mashirika yote ya Ulaya yanaanguka kutokana na competition kuwa kubwa.. Hapa nilipo kuna mashirika ya ndege ya ndani yasiyopungua 20 wakati nchi nzima ina population sawa na Tanzania. Now, lets say wao asilimia 80 wanauwezo wa kupanda ndege lakini kuna ndege mara elfu zaidi yetu zikiruka kila dakika..
Emarites wanafahamu soko la Tanzanioa hasa kutokea Dar na wanajua wazi kwamba over 7% ya wasafiri wanatoka bara ambao hulazimika kuja Dar kukata ticket kwa ajili ya Usafiri wa nje. Na wanapofika Dar wanakuta mashikrika mengine zaidi ya matano 5..
Hivyo ukiwapa data za kuonyesha kuwa wasafiri wanaochukua BA, KLM au Swiss air wengi wao wanatoka bara,pia ushirika wao utapunguza karaha za wasafiri kuja Dar kukata Ticket kwa kutumia ATCL, bila shaka Emirates wantakuwa interested..
Hayo mashirika yote yaliyoungana na mashrika ya Afrika sio kwa sababu yalikuwa ayakifanya vizuri.. as a fact mashirika mengi yalikuwa yakifanya vibaya isipokuwa yamekuja inuka baada ya kuunganisha na mashirika ya nje...Toka Zambia Airways, hadi Kenya Airways mapato yao yamezidi toka wajiunge na mashirika ya nje..Hata NWA walikuwa miguu juu wakachukuliwa na Delta kwa sababu ya baadhi ya safari zza nmdani NWA ataweza kuwaunguanishia wasafiri wanaokwenda Asia na Europe kwa hivyo NWA end up to be a profitable deal akuinunua.
Just imagine kwa nini msafiri toka Mwanza aje hadi Dar kuchukua BA au KLM wakati anaweza kabisa kukata ticket ATCL toka Mwanza na akapata connection Kili au Dar ambayo Emirates watamfikisha London kesho yake..Zile gharama za kulala Dar, karaha za kutafuta ticket ambazo unaweza ambiwa full booked hadi next week zinaondoka..
Ndio maana nasema inatakiwa watu wakae wakune vichwa kabla ya kufikiria kutupa bahati hii ovyo tukajutia kesho, Hiyo Option ya pili pia nzuri lakini nionavyo mimi kutokana na watu na mazingira yetu swala la Bakhresa pekee kuchukua ATCL litakuwa na utata mkubwa zaidi ya kuwekwa sokoni..Bakhresa atanunua hisa na kuwa ktk board ya wakurugenzi na kutakuwepo vichwa vingine ambavyo wananchi kina yakhe sisi tuliona Bakhresa kaingiza fedha tutafuata...Maadam ni shirika la serikali hadi sasa nadhani kuwapa wananchi nafasi sawa ni it's good Politics kuliko zile za uuzaji nyumba!
Mkuu nitajari bu kukufahamisha mtazamo wangu kwa mifano..Mkandara,
pamoja na analysis yako ndefu lakini je unakubaliana kuwa Emirates wako comfortable na soko la Tanzania? Kwanini wajiingize kwenye ATCL ambayo haina faida kwa sasa? Kama nilivyokueleza hapo awali kuwa ATCL is not profitable kwa hiyo siyo kazi ya Emirates kuifanya ATCL iwe profitable. Kazi ya kuifanya ATCL iwe profitable ni kazi ya mwenye mali kwa sasa. Inshort bidhaa ATCL hainunuliki kwa sasa.
Pundamilia,
Mkuu nitajari bu kukufahamisha mtazamo wangu kwa mifano..
Kwanza nianze na swala la Emirates.. hakuna shirikja ambalo liko confortable ktk biashara za usafiri wangeweza wangeongeza ndege zaidi kuja Tanzania ikiwa kuna wasafiri wengi..Au wangechukua safari za nchi nzima lakini kutonana na sheria na regulations hawana uwezo huo zaidi ya ku run international flights..
Kumbuka mfano niliokupa hapo juu ni kwamba Emirates hawata lazimika kununua ATCL isipokuwa tunashirikiana kibiashara Ubia ambao utamsaidia kila mmoja wetu..
Ubia huu utamwezesha Emirates kuwa na wateja zaidi kwa sababu wasafiri wanaotoka bara wataweza ku book ticket zao toka mikoani na kurahisishwa safari zao kwa connection Dar au Kili..Kwa hiyo Emirates badala ya kuleta ndege moja kwa siku wanaweza kuwa na misafara zaidi ya miwili kwa siku.. Na Upande wetu ATCL itakuwa na wateja zaidi ambao watatoka mikoani wakijua connection ya kwenda Ulaya, Asia au Arabuni unaipata kwa ticket moja tu..hivyo itaongeza soko la ndani kwa ATCL.
Swala la kuuza ATCL mkuu wangu lina utata mkubwa sana zaidi ya kile tunachosoma magazetini. Kumbnuka wakati ATC ilipotakiwa kuuzwa Ufisadi ndio ulikuwa ktk hali ya juu sana, hivyo mimi na wewe hatuwezi kufahamu masharti yaliyofungamana na ununuzi wa ATC kumbuka tu mkono wa serikali ulikuwa bado upo ndani..Kwa mfanyabiashara yeyote ambaye hapendi siasa ndani ya biashara ni vigumu kuwekesha fedha zake pale serikali inapokuwa mdau kwani politics zitaingia. Kwa hyo ATC kama ingekuwa shirika binafsi na likataka kuuzwa ungeona mashirika kama Gulf na Emirates yakijitokeza.. My point being, kama leo tunataka kuuza ATCL ni lazima mkono wa serikali utoke..ATCL iwe shirika huru incoporated la wanahisa ndio member of the board across. Na hata siku moja sifikirii ATCL inaweza kutoka ktk pango hili ikiwa chini ownership ya serikali 100%...Tazama tofauti kati ya ATCL na mashrika yote duniani hata hiyo Air Canada, Ba, SAS au hata Kenya Airways!..wameweza kusimama kwa sababu ya kuuza shares. Hao Uganda Air imekufa kwa sababu kama zetu..
ATC na South Africa ilikuwa deal tu mkuu wangu kwa sababu jinsi ATC ilivyoendeshwa inaonyesha wazi kabisa kwamba ATC ilikuwa another goldmine..
Naweza kusema tatizo kubwa la ATCL kwa South Africa limekuja badilika wakati soko la biashara kwa wananchi wafanyabiashara lilipohamia Ulaya na Asia..wasafiri wengi walikuwa wakienda China, India na Europe badala ya South kama ilivyokuwa awali...Na panga la South lilipokuwa zito kwetu (kulingana na mkataba) tulijikuta hoi bin Taaban na kama ulivyosema Kenya, Suth Africa na Precision wote hawa hawakuwa wanunuzi isipokuwa kutafuta kutawala soko..Kosa kubwa lililofanyika wakati wa kujiengua hatukuwa tayari ku face dunia mpya ya biashara za usafiri wa anga..
Option zipo nyingi mkuu wangu kama ulivyosema lakini bado naamini kabisa hili linawezekana ikiwa kuna Uwazi na ATCL kuingia ktk soko letu, sii ajbau huyo mwenye Emirates mwenyewe anaweza kununua share!
Mkandara:
Unajua waholanzi wengi wanakuja Tanzania kwenye utalii kwa kutumia KLM. Ninavyosikia KLM walitaka kuingia ubia na ATCL, lakini inasemekana dili na South Africa ilijaza mifuko ya watu. Hivyo KLM wakabwagwa chini.
Zakumi,
Nadhani huna taarifa kamili ya waholanzi(KLM) Serikali ya Tanzania(ATC).
Waholanzi walionesha nia ya kuingia kwenye ubia na Tanzania kwenye ATC katika kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza chini uongozi wa Mwalimu. Waliweza kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya kusomesha marubani na mafundi wa ndege za aina ya Fokker 27. Nia na malengo ya waholanzi pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kutuuzia ndege za aina Fokker 27. Na kweli tulinunua ndege hizo na tukaendelea kufanya nao biashara ya vipuli na matengenezo makubwa. serikali pia ikanunua ndege ya aina Fokker 28 na pia baadae Fokker 50. Lakini utengenezaji wa ndege hizo ulikwisha koma kutokana na sababu mbalimbali.
Wakati waholanzi walipokuwa na interest ya kuingia ubia, sera za nchi yetu zilikuwa haziruhusu kwani Azimio la Arusha lilikuwa bado liko hai. (Njia kuu za uchumi lazima zimilikiwe na umma). Kwa maana hiyo basi statement yako ya kusema kuwa KLM walikataliwa kwa vile South African walikuwa wamewajaza watu mifuko inaonesha mapungufu katika kufanya utafiti (RESEARCH) wa hali halisi ya mambo.
Hizi hapa ni facts, sasa unaweza kuzifanyia kazi.
1) Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hatukuwa na uhusiano wowote na serikali ya Afrika Kusini wakati huo kutokana na sera za ubaguzi wa rangi.
2) Wakati serikali ilipouza hisa zake 49% kwenye ATCL, KLM ilikuwa tayari inamiliki 26% ya hisa za Kenya Airways ilizokuwa imezinunua muda mrefu.
3) Kumbuka hata serikali ya awamu ya Tatu haikuweza kuuza hisa zilizokuwepo ndani ya Air Tanzania Corporation (ATC) kwa vile shirika hilo lilianzishwa kwa kutumia sheria maalum ya bunge (Act of Parliament). Serikali ilichokifanya ni kuanzisha Kampuni nyingine Air Tanzania Co. Ltd (ATCL) kwa kutumia ile sheria maarufu iliyopo katika chapter 212 (Cap. 212 of Companies Ordinance Act)
Nadhani nimejaribu kuweka mambo kwenye mstari