Mimi kuna kitu kinaniumiza katika hili, Mnaposema sema fukuza huyo house girl as if yeye ndio mwanzo wa matatizo wakati hao wanandoa ndo wana matatizo wenyewe. HOUSE GIRL mmemfanya kama sio mwanadamu mwenye haki wala sioni thamani yoyote mnayompa (FUKUZA HOUSE GIRL). Kumchakachua umemchakachua, kumfukuza kazi unamfukuza halafu kinafuata nini?? Unamfukuza kwa kosa gani, hataa mbwa akifukuzwa anakuwa amekosea kitu.
Unasema umetubu labda kwa Mungu na kwa watu pia, kama kweli umetubu kwa kumaanisha, unaposema umfukeze house girl au mlizi unataka waende wapi?? Maskini wa Mungu walikuwa wanajipatia mkate wao wa kila siku kwa kukufanyia kazi wewe. Lakini kwa tamaa zenu mnawanyima furaha, hasa huyo binti maskini kakosa nini??
Nyie wote wanandoa mjue mlikuwa mnakomoana, yawezekana huyo mkeo, aliamua kutoka namlinzi baada ya kujua kwamba unatoka na house girl. Daaa mi kinauma kwa kweli, watoto wetu hawa wanaofanya kazi nyumbani kwa watu, yani nyumba nyingine sio nyumba kabisa ni mlango wa kwenda jehanamu.
Mi sijui kama nimekusamehe, mpaka nitakapojua, umechukua uamuzi gani juu ya huyo binti na huyo kaka.
Wala sioni cha kukwambia zaidi ya hili. TUBU KWA KUMAANISHA KUACHA, KAA NA HUYO MKEO MTUBIANE UOVU WENU. Mgeuke kuwa baba na mama wenye mfano wa kuigwa. MKISHAFANYA hivo kama unamfukuza huyo binti ujue anakwenda wapi kufanya nini, na maisha yake yataendelea je?? Yani ningekuwa mwamuzi wa hii kesi TUKUTUKU sijui ningekupa adhabu gani ................................basi tu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na hata kama umetunga. Kuna viumbe vinafanya mchezo kama huu. Washindwe!!!