House girl wangu anatumia vidonge vya HIV

Patandi

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
399
372
Amani iwe kwenu nyote. Nimegundua kuwa house girl wangu anae nilelea mtoto wangu mchanga anakunywa vidonge vya HIV kwa siri. Je hawezi kuwa amemwambukiza mwanangu? Kama jibu ni hapana, mwanangu atakuwa salama kweli au niachane naye msichana huyu? Naomba ushauri wenu.
 
Una umri gani wewe?
 
Maslahi ya mtoto vs. Unyanyapaa.

Nadhani hapo ni wewe kupima, kwa kawaida mtoto hawezi kuambukizwa simply kwa kulelewa na mtu mwenye maambukizi. Ndio maana hata mama mwenye maambukizi anaweza kuzaa na kulea mtoto asiye na maambukizi. Lakini kuna elimu inayoambatana na namna ya mama kumkinga mtoto wake. Kama dada hana elimu yoyote basi anaweza kumwambukiza hata kwa bahati mbaya, ukizingatia mtoto mchanga ni rahisi kuambukizwa magonjwa.

Lakini kuna uwezekano pia wa dada kumwambukiza kwa makusudi mtoto, hii inategemea na nyie mnavyoishi naye hapo nyumbani. Tumeshaona akina dada wa kazi wakiwafanyia vitendo vya kikatili watoto, kwa hiyo sio ajabu akiamua kumwambukiza kwa makusudi kama njia ya kulipa kisasi kwenu.

Mwisho wa siku maamuzi ni yako. Nenda kampime mtoto. Kama yupo salama, basi tafakari, je dada wa kazi anaweza kumwambukiza kwa makusudi?? Je kuna mazingira ambayo mtoto anaweza kuambukizwa kwa bahati mbaya? Kama majibu ni hapana basi maisha yaendelee.

Kama mtoto tayari anamaambukizi jizuie usifanye maamuzi utakayojutia baadae.
 
Siku ndugu yako wa karibu kabisa. Yaani kabisa akiwa anatumia hizo dawa ndio utatumia ubongo wako kujua kama ni Sawa kukaa nae au umfukuze.

Ila kwa sasa fanya tu vile moyo wako unavyotaka
Umemjibu vizuri Sana ndugu. HIV sio kifo...tusiwahukumu kwa hali zao,wapo wengine wanazaliwa na virusi hivyo tujitahidi kuwa positive na hali hii. Inaweza kumpata yeyote na muda wote.
Stigmatization sio jambo zuri
 
Amani iwe kwenu nyote. Nimegundua kuwa house girl wangu anae nilelea mtoto wangu mchanga anakunywa vidonge vya HIV kwa siri. Je hawezi kuwa amemwambukiza mwanangu? Kama jibu ni hapana, mwanangu atakuwa salama kweli au niachane naye msichana huyu? Naomba ushauri wenu.
Hilo sio swali la kuuliza wewe kama mwanaume mlinzi wa familia.
Jibu ni jepesi unalipata kwa kutumia akili ya kawaida. Ukimrudisha kwao hasara ni kumnyanyapaa, faida ni kuondoa uwezekano wa yeye kumuambukiza mwanao kwa bahati mbaya au makusudi (kesi za makusudi zipo nyingi tu). Na kingine ni kukuondolea wasiwasi na roho juu ambayo hii bado ni unyanyapaa vilevile.

Sasa amua moja, unyanyapaa wa kimyakimya ambao madhara hamna maana hajui kama umemrudisha sababu hiyo. Au, hatari ya mtoto kuambukizwa ama kuishi kwa hofu.

Waliosema ni unyanyapaa waulize kama wanaweza oa au kuolewa na mtu mwenye maambukizi na wao hawana. Hawawezi, huo nao ni unyanyapaa?
 
Amani iwe kwenu nyote. Nimegundua kuwa house girl wangu anae nilelea mtoto wangu mchanga anakunywa vidonge vya HIV kwa siri. Je hawezi kuwa amemwambukiza mwanangu? Kama jibu ni hapana, mwanangu atakuwa salama kweli au niachane naye msichana huyu? Naomba ushauri wenu.
Kaa nae mbali chief maana sio salama kwa mwanao siku atakua anatumia na miswaki mnayotumia bila ya nyinyi kujua mtajikuta mnashare
 
Sikuhizi Nikileta housegel mpya bila kupoteza muda
1 .Lazima nimpeleke akapime
2. Lazima nimpeleke kanisani kwanza haya makanisa ya kilokole!

#Afya kwanza
 
Sikuhizi Nikileta housegel mpya bila kupoteza muda
1 .Lazima nimpeleke akapime
2. Lazima nimpeleke kanisani kwanza haya makanisa ya kilokole!

#Afya kwanza
Makamisa ya kilokole Yana nini kwani mashekhe hawawezi omba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom