William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
JK tumeona ulivyolishughulikia la Richmond na tunangoja utekelezaji wa Pinda.
JK tumeona ulivyolishughulikia la BoT na tunangoja utekelezaji wa tume.
Kuhusu ujenzi wa bara bara ya kanda ya kusini, mbona mwanzo ilitangazwa kwamba itajengwa bara bara ya Tunduru - Songea - Mbambabay? hapo mbona amepunguza kilomita nyingi sana? yaani Tunduru- Namtumbo na Mbinga Mbambabay. Katika ilani ya CCM bara bara hii inatambulika na imeahidiwa kujengwa. kulikoni?
Hilo la richmond amelizungumzia indirect...kwa kutaja jina la Waziri Mkuu mpya....
Sasa mlitaka ataje scandals zilizo kikumba chama chake? Huyo atakuwa sio mwanasiasa. Wanasiasa hawaongelei matatizo, wanaongelea mafanikio.
Kuhusu wananchi wa kawaida nafikiri kuna faida kwenye UKIMWI na Malaria.
Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.
Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.
Kwanza hebu fafanua una maana gani ya kusema watu masikini
Kwenye haya mkuu D, tuko wote yaani kwenye the same page.
Kama wewe mtoto wa Fisadi, au ndo Fisadi mwenyewe hutakuwa uelewi maana ya neno masikini, ila kwa jamii ya Tanzania neno ili ni kawaida,
Vipi mnashirikiana na bwana mkubwa kututia kwenye kaango la umasikini nini, mbona unamtetea huyu Fisadi? au ndo nyie anao walinda nini? Maana unanitisha kama uelewi maana ya neno Masikini wewe ni hatari sana
Matatizo makubwa sana yalikuwepo kabla ya ubinafsishaji, kwa nini viwanda, mashirika, mabenki, mashamba tulivyo vitaifisha na tulivyojenga wenyewe vifikie mpaka kubinafsishwa? jibu ni rahisi sana, tulishindwa kuviendesha na vikafa ndio vikabinafsishwa. Kipi ambacho kiliweza kujiendesha kwa ufanisi na kuliingizia taifa faida kilibinafsishwa?

Wakati tukiwapongeza Wakenya kwa mafanikio yaliyopatikana na kuwapa pole kwa magumu yaliyowakuta yatupasa kujiuliza mafunzo gani tunayopata. Mafunzo hayo ni muhimu ili tujiepushe na kasoro zilizowafikisha hapo. Kwa maoni yangu, fundisho kubwa sana tuliloliona ni kuwa kuendeleza ukabila ni jambo hatari sana kwa taifa. Bahati nzuri, katika nchi yetu tatizo la ukabila halipo, lakini linaweza kuwepo tusipokuwa waangalifu kwa vile makabila yapo. Nawasihi, ndugu zangu, tusiwape nafasi wale wote wanaofanya vitendo vinavyoweza kuturudisha kwenye ukabila.
Lakini, kwa nchi yetu lililo hatari la kujiepusha nalo si la ukabila tu, lipo la udini na yapo masuala ya ubaguzi mwingineo. Kenya hawakuwa na tatizo la udini lakini la ukabila lilitosha kuivuruga nchi. Je, kama lingeongezeka na tatizo la udini ingekuwaje? Tufanye kila tuwezavyo tuhakikishe kuwa tunapiga vita kwa uwezo wetu wote vitendo, fikra au hata mwelekeo tu unaoweza kutugawa kwa misingi ya makabila yetu, dini zetu, rangi za ngozi zetu, maeneo tutokako na mengineyo. Wale wenzetu wanaotaka kutupeleka kubaya tusiwape nafasi. Tusivumilie kauli zao za uchochezi au matendo yao ya kibaguzi. Misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa letu hususan hayati Mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Amani Karume daima tuienzi. Tukiipuuza ole wetu.
Katika hitimisho la hotuba yake, Mheshimiwa Rais ameongelea mafunzo kutoka Kenya kwa ufupi mno kana kwamba alimlazimu akatishe hotuba yake na asiwe mpembuzi wa kina wa tulichojifunza. Ama amekwepa kuwa mkweli kuwa tuna mambo mengi ambayo ni chumvi na pilipili zinazosaidia fukuto ambalo laweza kutufanya tufikie mpasuko na utengano kama yaliyotokea Kenya.
Nanukuu
Kwa Tanzania, tatizo la kwanza litakalo leta machafuko ni lile la Matabaka ya WenyeNacho na WasioNacho! Mgawanyiko huu mkubwa ambao umeweka zege kali kati ya Masikini na Matajiri iko siku utafikia tamati na damu itamwagika.
La pili ni lile la Rangi/Dini (Zanzibar)! Tayari tumeshaona roho zisizo na hatia zikipoteza maisha kule Zanzibar na hata kwenye machafuko ya kidini bara.
Nitaomba nimuulize Mheshimiwa Kikwete, umesema ni muhimu tujiepushe na kasoro zilizotokea Kenya na kuleta vurugu, Je Serikali yako na Chama chako CCM vinaafikiana na kauli zako? Maana ikiwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto, Ubabe wa CCM na unazi wa Serikali kwa kuzembea haki itawale wiki mbili zilizopita kulihatarisha usalama na karibu roho zipotee je ni jitihada gani unazifanya wewe kama Rais na Mwenyekiti wa Chama tawala kutuepusha na hizo kasoro kama ulivyotutahadharisha?
Je ni lini utahakikisha kuwa kuna Muafaka Zanzibar?
Umesema "wale wenzetu wanaotaka kutupeleka pabaya tusiwape nafasi". Chama chako CCM na Serikali yake imejijenga kwa kuwa na tabaka la kung'ang'ania madaraka na zaidi kuwa na kundi la viongozi ambao wanakimbilia kujilimbikizia mali kwa njia zozote (Mafisadi) mpaka kuhujumu na kusahau dhamana yao kama viongozi na wajibu wao kulitumikia Taifa. Utafanya nini kwa nguvu zako za Kiserikali na Kichama kuhakikisha ule upenyo uliokomaa wa Uhujumu kwa makusudi au uzembe unazibwa na kuwa tunakuwa na Viongozi waadilifu ambao ni mfano chanya wa kuigwa ili kuchochea uzalishaji mali kwa njia halali kuondokana na umasikini na si kutafuta njia fupi fupi ambako kumeishia kujenga mgawanyiko wa tabaka la matajiri na masikini?
Je utaruhusu Sheria na Haki vifanye kazi yake kusahihisha makosa na uhalifu uliotokea (BOT, RICHMOND) au utaendelea kuruhusu mchakato ulioko sasa hivi wa kusameheana kimya kimya kwa kuona aibu kuumbuka?
Je Juma aliyeko Makunduchi na Bundala walioko Maswa wakijirudi makosa na kurudisha walichochokua kwa njia danganyifu, watapewa msamaha na heshima ya kuwa huru kimya kimya kama hao wanaorudisha pesa za EPA?
Kama unatamka tusiwape nafasi wale wenye kuwa vichochezi vitakavyoishia kuleta vurugu, inabidi uitumikie kauli yako kwa mifano niliyokupa hapo juu.
Nakutakia kila la heri katika kikao cha Kamati Kuu wiki ijayo!
Sasa mlitaka ataje scandals zilizo kikumba chama chake? Huyo atakuwa sio mwanasiasa. Wanasiasa hawaongelei matatizo, wanaongelea mafanikio.
Kuhusu wananchi wa kawaida nafikiri kuna faida kwenye UKIMWI na Malaria.
Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.
Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.
Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.
Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.
Kikwete na waandishi wake wa hotuba ni zero kabisa.
Kasema kuna mambo matatu lakini kaongelea mawili tu, lile la tatu kaliogopa!
What a joke!