Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .

Mbona hamutaki kumwelewa Rahisi? JK amesema hivi: Bilioni 90 ndio zilichukuliwa na yale makampuni ambayo uchunguzi wake umekamilika maana data zao zinapatikana kwa urahisi injini. Hao ndio wameombwa kwa heshima na taadhima warudishe fweza kufikia jana ili wasikatwe na sheria ni msumeno. Na wamesharudisha takribani asilimia 76 ambayo ni Daraja A ama Festi Klasi. Hivyo vijisenti vilivyobakia vilichukuliwa na yale makampuni ambayo uchunguzi wake ni mgumu kupindukia kwa kuwa data zake wanazo wenzetu huko ughaibuni hivyo tunategemea usamaria wema wao ndio tuzipate. Bado kina Mwema wanawabembeleza watupe data hivyo UCHUNGUZI UNAENDELEA! Au unadhani hii ni JUST KIDDING?
 
Companero,
It boggles the mind. Wizi umefanyika Tanzania yet data tunasubiri watupatie wenzetu
walioko ughaibuni. It boggles the mind.
 
Hebu niulize ni lini huyu Rais aliongea something which make sense to majority of Tanzania?

-Alipowahutibia kwenye kampeni mkasema ni chaguo la Mungu!
-Alipohutubia Bunge Disemba 2005 mkasema kweli Rais tunaye!
-Alipowahutubia Ngurdoto mkasema hakika ni Tumaini Lililorejea!
 

Mkuu Sober very strong indeed, infact according to the dataz kuna copies za cheki ambazo Mkapa alizisaini few minutes kabla ya kwenda Uwanja wa Taifa kumkabidhi Kikwete urais, ambapo hela zilichukuliwa BOT kwenye huu mlolongo, mstaafu wa idara knew about it kwa sababu he was involved, na ni wakati huu matatizo ya Balali yalipoanza rasmi.
 
Companero,
It boggles the mind. Wizi umefanyika Tanzania yet data tunasubiri watupatie wenzetu
walioko ughaibuni. It boggles the mind.

Sasa tungepataje data za Vijisenti vya RADAR kule kisiwani JERSEY bila washirika wetu wa Maendeleo kule UK kuchunguza BAE? Kiwi cha Macho!
 
Muda wote nimekuwa kimya na kuutaka ukweli juu ya jambo hili .Wakati Rais akisema pesa zinarudi wengi tumetaka kujua account ipi zinaingia na majina ya wanao rudisha na ngapi zimerudi in reallity badala ya kuaminishwa kwamba zinarudi .

Habari za uhakika zinasema kwamba ngoma hii ni nzito maana hakuna aliye rudisha pesa bali wote hawa wanatoa hesabu ya namna zilivyo tumika .Ndiyo maana utata umetanda na utaendelea bila ya majibu ya msingi na hakutakuwa na majibu hadi mwaka 2010 plus .
Ukweli ndiyo huo hakuna pesa inayo ingia katika pembejeo wala nini .Again another game toka juu .Kama kuna ubishi basi walete majina ya makampuni yaliyo rejesha na Account number na Bank ipi ili tujiridhishe .

Naomba kutoa hoja
 

Yaani walikuwa wanatarajia mtu mwingine kurejesha fedha usiku wa manane? Hivi kabla ya muda kuongezewa kiasi gani kilikuwa tayari kimerudishwa na kiasi gani kimerudishwa ndani ya miezi karibu miwili ya nyongeza?
 

43 Billion zilitumika kumuelect JK as a president. Sasa anachofanya ni common sense accounting, ana writte off 43billion.

Kusema kweli yaani i wish Mahakama ya dunia ingeingilia na kutangaza warrant kwa JK. Sababu JK anachofanya ni kuwaibia watanzani, tofauti yake na raisi wa Sudan ni kwamba wa Sudan anawaibia wananchi through vilonce, na JK anatumia partner wake kama Rostam Aziz.

The whole slogan ya kwamba 76% ya pesa za EPA zimesharudishwa hili ni kwaajili ya kumtetea Rostam Azizi, sababu Rostam can afford kurudisha, lakini wale masecretary walio sign deal na kuchukua 5Million wameshazitumia, and they cant bring back anything. So, what is happening now ni kwamba little guy is about to get maximum penalty, wakati the BIG FISH kama Rostam and Mkapa they're running loose.
 

Halafu kuna wa-Tanzania tunaoamini kwamba hawa wana nia njema ya kutuingiza OIC?
 
Yaani walikuwa wanatarajia mtu mwingine kurejesha fedha usiku wa manane? Hivi kabla ya muda kuongezewa kiasi gani kilikuwa tayari kimerudishwa na kiasi gani kimerudishwa ndani ya miezi karibu miwili ya nyongeza?

Mzee wa Kijijini una maswali magumu.Hizi figure utapewa tu baada ya muda ukiuliza mkuu atakuwa kesha sahau alichosema maana hakuna kinacho endelea
 
Yaani walikuwa wanatarajia mtu mwingine kurejesha fedha usiku wa manane? Hivi kabla ya muda kuongezewa kiasi gani kilikuwa tayari kimerudishwa na kiasi gani kimerudishwa ndani ya miezi karibu miwili ya nyongeza?

Tusubiri kidogo, timu ya Mwanyika inasema itatoa taarifa rasmi kesho
 

You're the only one who can understand this President! Kweli waTanzania hatujielewi kuwa na sisi ni Nchi! How do you rely "datas" for your country to be given to you by another country; let us admit that we have no infrastructure as a country to deal with our own problems or else ni uvivu wa akili zetu kufikiri? A president of a country depending on another country for the "thieves" who are known in his own country; does this sound real to you?
There is already evidence established these guys (companies) took money illegally from treasury, this is already established; this was already a warrant to make an arrest and pending investigation! Believe this President is buying time; and he knows exactly what transpired.
 
Rais alisema itatoa taarifa leo, na wao wanasema watatoa taarifa kesho.. hivi hawa watu wanazungumza kwenye hiyo serikali yao?
 
Rais alisema itatoa taarifa leo, na wao wanasema watatoa taarifa kesho.. hivi hawa watu wanazungumza kwenye hiyo serikali yao?

Mzee, wewe hujashangaa zaidi yangu maana nimezungumza na Mwanyika mwenyewe na kila nilivyojitahidi kumbana anieleze kwa nini imekuwa hivyo, amekuwa na majibu ya kurukaruka tu!!!
 
Jamani suala la kujiuliza ni je ingekuwa tume imeundwa na Bunge tungepata matokeo tofauti? Let say, tume ya wabunge kutoka kambi zote? kwangu mimi suala zima halina transparency, ni ujanja ujanja na halina hata chembe ya legitimacy kwa umma wa kitanzania.

Sulala hili nitanedelea kupiga kelele si la kuwa dealt na rais, bali bunge. Kwangu mimi, Mh. Rais ni kama ameliteka nyara suala zima la EPA. Tume ya wananchi kupitia wawakilishi wao ingeleta legitimacy na matokeo tofauti. Jamani wanasiasa wetu na sisi sote tunatakiwa kubadilika. Ukifuata suala la separation of power, hili suala la umma lilitakiwa lishughulikiwe na Bunge na serikali ilitakiwa iwajibike kwa Bunge katika utekelezaji wa maamuzi ya tume ya Bunge kuhusu EPA na siyo Serikali kujichunguza...kaazi kweli kweli, Mh. Rais, checks and balances tujaribu kuirudisha na ionekane ikifanyika. Tuache unazi wa kichama linapokuja suala la utaifa na hatima ya taifa letu. Angalia wenzetu, Gavana kapewa "kijimsaada" cha kufanyiwa ukarabati wa nyumba yake ... leo yuko matatani na Congress imempeleka kortini na kifungo kinamnyemelea ...tubadilike si suala huyo ni mwenzetu kama ni suspect wa wizi , hacha wananchi kupitia wawakilishi wao wafanye uchunguzi na kuwafikisha mbele ya dola kujibu mashtaka. Kama tunaamini katika sovereignty of the people kama katiba inavyosema, nathubutu kusema Rais tume uliounda haina legitimacy.
 
If what they say about the dead turning in their graves, I think Julius Nyerere is Summer saulting in his...... Wishing he could come back and chapa viboko honourable mr president of the united republic.
 
Mwanakijiji,Mpita Njia,Lunyungu,

..Raisi amefaidika kwa namna moja au nyingine na wizi wa EPA.

..AG Mwanyika,IGP Mwema,na Dr.Hosea, hawana uwezo wa kushughulika na kulipatia ufumbuzi suala hili.

..kuendelea kuwaandama hawa ni kuwaonea tu. mhusika mkuu ni Raisi na genge la wana mtandao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…