Hotuba ya upinzani kuhusu mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya upinzani kuhusu mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Jun 13, 2011.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Mpango wa maendeleo wa Taifa kama ilivyosomwa bungeni leo 13/06/2011.

  Hii ni hotuba ya kwanza kusomwa na kambi ya Upinzani tangu CHADEMA wawe ndio kambi rasmi Bungeni.
   
 2. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duhh, hii ni hatari yaani JK kadanganywa tena?

  Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda kuwasilisha masikitiko ya Kambi ya Upinzani kuhusiana na mpango huu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 (3) (c)inasema kuwa majukumu ya Bunge ni "kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo"; Wakati ibara ya katiba ikitamka hivyo, mpango huu tayari ulishasainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tangu tarehe 7 Juni 2011 na kuwasilishwa bungeni tarehe 8 Juni kama hati ya kuwasilisha mezani, bila kuelezwa ndani ya mpango wenyewe kama kilichowasilishwa ni rasimu.

  Aidha, kwa mujibu wa mpango wenyewe, Rais ameshashukuru wadau kwa maoni yao yaliyowezesha kukamilisha mpango na ameshalishukuru bunge kwa mchango katika kukamilisha mpango husika.Mheshimiwa Spika, Wakati Rais akisema hivyo, Kambi ya Upinzani haijawahi kushirikishwa wala kushiriki kikao chochote cha Bunge kilichojadili na kupitisha mpango huu. Kwa hiyo, Kambi ya Upinzani inamtaka waziri aeleze ni kikao kipi cha Bunge, na ni mkutano wa ngapi wa Bunge, uliowahi kujadili na na kupitisha mpango huu wa maendeleo na hata kumpelekea Mheshimiwa Rais kulishukuru Bunge kupitia dibaji yake iliyochapwa kwenye kitabu cha mpango huu.

  Mheshimiwa Spika
  , Kambi ya Upinzani inalitaka Bunge lifanye kazi zake kikamilifu na serikali iwe na utamaduni wa kuheshimu hilo. Tunaitaka serikali isiwe na utamaduni wa kuamini kuwa kila jambo litakalowasilishwa hapa Bungeni basi Bunge italipitisha tu. Tunaitaka serikali kuhakikisha kuwa maoni ya wabunge yanazingatiwa na kuingizwa kwenye mpango huu kikamilifu.
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakika Watanzanai tumelogwa na kulogeka. Tunajenga ghorofa hewani.
   
 4. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  hivi mheshimiwa Rais huwa anahoji vitu vinavyopelekwa mbele yake pengine hata kuvisoma kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote? kama mtu aliyewahi kukaa bungeni kama mbunge kwa zaidi ya miaka 10 ina maana hajui lolote kuhusu ibara hii?

  Ali-sign vp mpango huu wa serikali bila hata kupelekwa bungeni kwa majadiliano? hapa Rais kadanganywa tena.
   
 5. B

  Beethoven JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  rais wa nama hii si mzigo tu bali ni tatizo na maafa ya nchi.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo huwa najiuliza umakini wa hawa wawakilishi wa cdm bungeni na upotoshaji wao wa mambo kila kukicha. Hivi watalijuwaje hilo la mpango wa maendeleo wakati wao walisusia hotuba ya Rais ya ufunguzi wa bunge alipoeleza nia yake ya kuanzisha huu mpango?

  Hiyo hotuba ya Rais ilijadiliwa bungeni kwa kina, kama wao hawajachangia hili basi leo wasipotoshe umma kwa kuwaambia hawalijui.

  Hivi kama walisusia hicho kikao basi hata hawajachungulia kwenye TV? Halafu wao wanamsusia Rais hotuba yake tu? kwa nini na huu mpango wake wasiususie? Wananshangaza!
   
 7. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Natamani kama Waccm wangejibu kipengele kwa kipengele, hakika wangeshikwa na kigugumizi.
   
 8. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Is getting weird
   
 9. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani huu mchezo wa kuweka document in word un astua sana kwani inaweza kuchakachuliwa kirahisi sana. CHADEMA muwe makini jamani
   
 10. B

  Beethoven JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  FaizaFoxy tunachoangalia si component moja ya kuidhinishwa na bunge punguza ukereketwa uangalie hata hizo figures hazioneshi kuwa ni mpango utakaokuwa feasible maana hata bajeti yake haionekani.Tupunguze kuishi kwa udanganyifu-tunadanganya wafadhili waone tuna dhamira kumbe la!tunadanganya wananchi ili wadhani serikali iko busy na maendeleo yao kumbe wapi!!!!
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  haya ndo matokeo ya shule za kata, pole mama kwa kuunguliwa na kichwa hadi kupelekea ubongo wako kuathirika.
   
 12. M

  Miruko Senior Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Taarifa: Hatuzungumzii hotuba ya rais, tunazungumzia mpango wa maendeleo ya miaka mitano 2011/2016. Ndugu yetu amka!
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Dada, hivi wewe na Malaria sugu ni shirika moja au au? Kwanini usiwe angalau unatumia ubongo wako kufikiria kabla ya kuandika? Unajua unaboa?
   
 14. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Mh kwani huo mpango uliandaliwa lini na ukafikishwa bungeni lini anataka kusema ulifikishwa bungeni wakati ule Chadem walipotoka bungeni? hapa naanza kuona uwezo wako ulivyo! pole sana
   
 15. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivyo utaratibu wa kuwasilisha hoja kama huo mpango wa maendeleo bungeni ukoje? Rais anaweza kwenda mwenyewe bungeni kuwasilisha mpango wake? au ni jukumu la Waziri anayehusika na maendeleo. Naomba ufafanuzi
   
 16. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani faiza fox anawashwa makalio ndo maana haelewi
   
 17. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Heshima kwako mkuu, nakuunga mkono, Chadema kuweni makini, watu watahribu na kurekebisha itachukua mda. Kujenga na Kubomoa ni tofauti.
   
 18. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni aibu sana kwa raisi na watendaji wake
   
 19. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwani hii document imetoka ofisi ya chadema? Letter head yeyote? au muhuri au sahihi? (Japo hata hivi vyaweza kuchakachulika vizuri tuu)Si imesomwa bungeni,na bila shaka itaingizwa kwenye ansadi za bunge. By the way format ipi isiyochakachuliwa siku hizi?
   
 20. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Inawezekana hao marafiki zako wanapata shida kweli kweli kukuelewa. Hata Nape anaanza kupata kigugumizi na kuanza kuunga mkono hoja za PEOPLES POWER. Ina maana Rais aliijadili mwenyewe kwenye hotuba aliyosoma bila wabunge kuchangia. Isome tena uielewe sio unachafua hali ya hewa kwa makusudi?
   
Loading...