hujaeleweka....
viwanda sina uhakika ila hivi vingine vina usahihi....!!! Amejitahidi Japo kuna matatizo
kikwete huwa ni kauzu zaidi ya dagaa,wewe imagine "guts" za kusema maisha bora ni pamoja na foleni za magari,watu kupanda ndege na kununua bajaji kwa ajili ya wagonjwa mahututi kupelekwa hospitali!!!!this coastal indigenous has got balls.
Wana jamii nimeuliza hili swali kutokana na sehemu ya hotuba ya rais kufunga bunge niliyoisikiliza jana.
Rais katoa takwimu mbalimbali, katika mambo mbalimbali kudhihirisha kuwa kuna maendeleo yanaonekana ukilinganisha mihula yake ya uongozi na mingine iliyopita.
Nimebaki na maswali kwenye hayo maeneo mawili zaidi japokuwa pia hatuwezi kuhakiki sana usahihi wa hizo takwimu zilizotolewa katika nyanja tofauti tofauti. Alisema kuwa siku hizi familia zina gari la baba, mama na mtoto/watoto, je ni familia zipi hizo anazosemea? Isikute sana sana zote zenye uwezo huo ni hizo zenye wanachama wa chama chake maana sababu ndio wanaowezeshwa kwa kupatiwa kazi na nafasi zenye ulaji (ufisadi au rushwa), na zile za wanasiasa (hasa wa chama tawala) ambao wao moja kwa moja zinajulikana uadilifu wao.
Wa kawaida sio rahisi sana labda akijipinda sana apate kavitz na hapo deni utakuta kapitia saccos au against salary, hapo ataweza kumnunulia mke na mtoto?
Kuhusu kupanda ndege rais ametumia neno kama ka kejeli, nanukuu ''watanzania nao siku hizi wanapanda ndege'' ni maendeleo haya jamani. Inawezekana anaona airport kunafurika na akajua uwezo wa mtanzania umeongezeka anapanda ndege. Lakini wanaweza kuwa wanapanda kujiepusha na ajali za kila leo kwa kujikusuru tu, hawana sana lakini uzima tu ni muhimu zaidi kuliko kubania halafu hufiki salama, ukifika salama utapambana na ya kesho.na wengine wanalipiwa na ofisi, kwa uwezo wao wasingeweza.
Na zaidi ya hapo audience iliyokuwa inamshangilia ni wale wenye huo uwezo uliotajwa, sidhaani kama wale wanaogawiwa kofia, kanga na pilau na wakagawa kura walikuwepo kwenye hao washangiliaji
mipaka iko salama na jeshi lipo tayari kwa vita yoyote...!!! -JK
Hizo ndo mi naita sifa za kijinga jinga... Muulize serikali yake ime-subsidize kwenye bati, sementi,n.k kwa kiasi gani...??
Hajui kuwa watu wake wanakula mlo mmoja ili tu waweke akiba kuzijenga hizo nyumba na kununua hayo magari..?? Wa hovyo sana huyu! Bora liende!