Njoka Ereguu
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 821
- 336
Kama kweli serikali imehusika hata kama Rais asingeliongelea bado ukweli unabaki pale pale kuwa serikali haitakaa ikubali kuwa imehusika.
Unajua kwa namna moja au nyingine upo uwezekano kuwa askari wanaotajwa wamefanya hicho kitendo kwa ufisadi wao wa kifikra kwa kuwa walikabidhiwa jukumu la kufuatilia mwenendo wa mgomo, kwa kuwa kazi hiyo ilikuwa inawanyima muda wao wa kufanya kazi nyingine kwa kuitwa kila mara kuelezea kinachoendelea waliona ni jambo la busara sasa kutumia ufinyu wao wa kufikiria (kwa maana hapo ndipo akili yao ilipofikia ukomo) wakaona ni bora kumuua Dr. Ulimboka.
Kwa mazingira hayo upo uwezekano Mkubwa kabisa kuwa viongozi waliowapa kazi ya kufuatilia mwenendo wa mgomo wa Madaktari kushindwa kuamini kama askari hao wangeweza kutenda unyama huo.
Tatizo lingine linalojitokeza hapa ambalo halijatolewa ufafanuzi ni kwamba katika maelezo ya Dkt Ulimboka, anaeleza kuwa walienda leaders na Dkt. Mwezake na hata wakati anatekwa walikuwa na Dkt. Mwenzake ambapo watekaji walisema hawana shinda na mtu mwingine ila yeye tu Dkt. Ulimboka, iweje huyo Dakt. waliyekuwa naye anashindwa kuelezea kilichotokea na wakati walikuwa na Ulimboka muda wote? na kwa nini alichukua muda mwingi bila kumfuatilia mwenzake? katika hali ya kawaida uko na rafiki yako au jamaa unaona amekamatwa ni busara tu kuwa angefuatilia kujua anapelekwa kituo gani cha polisi na hivyo angesaidia kupatikana kwa taarifa mapema kuliko alivyojinyamazia. Upo uwezekano wa kuwa na mashaka na huyo Dakt. katika hili.