Hotuba ya Rais imeonyesha njia; Tozo na kodi kwa mahoteli na lodge zipunguzwe

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,460
1,444
Nimesikiliza hotuba nzuri ya Rais na kubaini kuwa Rais anayo nia njema ya kulipeleka mbele taifa letu. Kwa upande wa miundo mbinu ya watalii mahoteli ni muhimu sana yakaboreshwa kwa kuyawekea mazingira mazuri hivyo nashauri mambo yafuatayo:

1. Kupunguza bei ya leseni ya TALA kwa mahoteli kama ilivyofanyika maeneo mengine ya utalii na wanyamapori kutka dola za marekani 1000 hadi dola 400 na zilipwe dola 100 kwa kila miezi 3 hii itasaidia mahoteli mengi kumudu kulipia leseni hiyo muhimu na kuiwezesha serikali kupata mapato.

2. Kufuta tozo nyinginezo zinazoathiri biashara hii

3. Kupitia tena viwango vya faini zitozwazo kwa makosa ya kutozingatia sheria za kodi na riba zake ili faini hizo ziwe zinazolipika kirahisi kwa pato halisi la mfanyabiashara badala ya kumvunja moyo na hatimaye kufunga biashara

4. Kufanya classification ya mahoteli, nyumba za kulala wageni,loji nchi nzima kwa viwango vya Afrika Mashariki ili wageni wata mbue ubora wa kila nyumba ya wageni nk

Haya yakifanyika kwa kuanzia itasaidia kutengengeneza matajiri wazalendo na kuchochea uwekezaji kama Rais alivyosema lakini pia kuchochea ajira ktk sekta ya utalii. Rais kaonyesha njia watendaji tutekeleze.
 
Hii imekaa vizuri japokuwa ni kwa sector ya utalii. Waangalie na sector zingine.. tozo zipunguzwe
 
2613493_1605082586048.png
 
Hivi NEC na ZEC kura upigaji kura wa bando kitita,ama kuwakilisha familia,taasis uliruhusiwa??
Kufikia Dec 2020 usajili wageni loji na hotel unapaswa kuanza rasmi kuratibu watalii wa nje na ndani kwa njia mtandao, wakitumia leseni udereva, nida ama pass ya kusafiria, tujiandae kuchangia pato juhudi wizara maliasili na utalii.MNRT- PORTAL.
 
WATU WAPUMBAVU HUWA HAWAELEWI HADI RADI IWALIPUE.

YANI KWELI UNAMUAMINI JIWE!!!!!!!!.
ushauri tu.

USIMWAMINI KABISA KWA AHADI ZAKE NI MUONGOBWA KUTUPWA.
 
Hittler ni mmoja wa watawala waliokuwa na hotuba nzuri mno lakini ameacha maumivu duniani.
 
Back
Top Bottom