Hotuba ya Mhe Moh Dewji: April 25, 2009

Nilikuwa namheshimu huyu kijana kutokana na kuonekana kuwa active katika mambo mbalimbali ya kijamii lakini unfortunately hotuba yake hii imenifanya nimuangaliea tena upya kutokea upande wa pili.

Pamoja na makosa kadhaa katika kutaja idadi ya pesa alizotoa ambapo shilingi milioni mbili zimeripotiwa kama shilingi milioni 2,000,000 na vitu kama hivyo, hotuba hii imedhihirisha kuwa jamaa huyu ana jambo analotaka kuficha katika nafsi yake ndiyo maana amekuwa anatumia maneno "Mimi nimesaidia hivi na vile ....." Angekuwa ana nia ya kusaidia watu wake bila kutegemea hifadhi fulani kutoka kwao angetumia lugha nyingine kabisa; lugha kama.... niliwaomba Mohammed Foundation watusadie jimboni kufanya hili na lile nikafanikiwa.... ingekuwa na ujumbe mzito zaidi kuliko kusema nilitoa hela yangu binafsi kuwasaidia watu wa jimboni kwangu.
 
Siyo hilo tu hata ile ilikuwa ikiitwa sukari kijiko kimoja ilikuwa ni kashfa kubwa tu lakini kwa sababu ni Tanzania Rupia ilipenyezwa mambo yakamalizwa kimyakimya. Kwa wasiofahamu ni kwamba ile sukari ilichanganywa na kemikali fulani kuiongezea utamu. Waliotoboa siri sasa hivi wako futi saba chini ya ardhi. Pia kuna mkemia Mashimba naye alipotezwa sikumbulki kama ndiye huyo Fupi..

Nakosoa, Aliyepoteza maisha yake ni Dr. Fupi.kwani ndo alikuwa shahidi muhimu wa Serikali kwenye hiyo kesi ya MO, na mashahidi karibia wote nasikia walikufa!!

Sasa hivi Mkemia Mkuu wa Serikali ni Ernest Mashimba huyo bado yuko hai ingawa alikuwa amepata ajali mbaya lakini sasa hivi yuko fit.

Shida Serikali yetu tumebinafsisha kila kitu, Chunguza sana viwanda vya wahindi ni ngumu sana kuingikilika, sijui kuna nini huko! chunguza kifo kilichotokea Shivji& Sons sijui kesi imefikia wapi hadi leo! na haya ya MO sishangai!!
 
Sisi Wa-islamu huambiwa ukitoa Mkono wa Kulia wa Kushoto usijue, sasa Dewji kutoa ni wajibu wake lakini kupiga kelele nimetoa hivi na vile naona kuna walakin. Ima anajipigia Zumari kurudi tena kilaini kwenye nafasi yake au anajionyesha kwa Kiswahili cha kwetu visiwani ni KUJIPA.

Hizo fedha alizonazo angekaa na kufanya Strategic Plan basi Singida isingemsahau maisha. Unahitaji ukae uangalie vipi kusaidia na Programu ya muda kadha na sio hicho tu kuwe na mfuko endelevu, hayo utayaona aliyoyafanya sio endelevu, akiondoka na kila kitu kimeanguka Puuu!

Namuomba Dewji asome Dark Days in Ghana cha Nkurumah kisha ataelewa Siasa za Africa, vilevile Dewji ajitahidi kumsoma Franz Fanon afahamu akili na uetndaji vitu hivi vinatakiwa vyende vipi?

Panganyile
 
Ningekuwa ni miongoni mwa hao wanaosikiliza hiyo hotuba ningeondoka mapema! Huyu Jamaa nadhani atakuwa Mbunge wa maisha hapo ukizingatia wapiga kura wake ni omba omba na wavivu kila mwaka wana njaa! wanajua MO yupo


Tafadhali bwana! Wape heshima yao wananchi wale...bongo yote omba omba, sio plae tu..eebo!
 
Kimsingi huyu Mbunge utoto bado umemjaa....kuchaguliwa kwake angechaguliwa hata angegombea Biharamulo, Rombo au Nachingwea, upofu wa wabongo upo popote, hasa kwa ulghai wa jinamizi CCM, watu wanafanya ndivyo sivyo. Bora mimi mbunge wangu Missanga ambaye yupoyupo tu, kazi kuchubuka uso kwa ibada.
 
what he says, mkono mtupu haulambwi, sasa iliuwe mbunge kwenye jimbo lake maana uwe tajiri wa kutoa misaada kama iyo! the figures look impressive but ofcourse room for validation is needed, also are those money that clean? can he honestly swear that the money are clean?
 
Kama ametoa hicho kiasi cha pesa tena mfukoni mwake
I wonder anafanya nini katika ubunge zaidi ya kuwa mfadhili... au
Amepata kiasi gani katika huo ubunge manake 1.5bn!!!! in Just 5 years
 
wajinga ndio waliwao

hilo nalo ni neno.

hivi waTanzania kweli tunaakili au mapumba, huyu jamaa hawezi kuwa na utu wa kiasi hicho cha kutumia faida yake kulisha wengine, fedha anayoitolea jasho ndio ije kufanya kazi za serikali kweli? kwa nini jamaa anainunua serikali mchana kweupe na anakeep records kwa faida yake na vizazi vyake (vitawala) na vizazi vyetu (Vitawaliwa),
hapo ndipo kwenye matatizo makubwa kabisa kwenye serikali yetu ya Tanzania, haiwezekani mtu binafsi ajenge shule ya serikali au hospitali, ilipaswa kama mbunge aende bungeni kulipigania jimbo lake na suio kutumia mali zake binafsi.
kama ni kutumia chake basi ajenge shule yake private na hospital zake private na awasomeshe watoto na kutibia watu bure na hapo sisi tungejua ni charity org, lakini sio kutumia mali za serikali na kukeep record za kuja kuwasomea watu hadharani

kwa hili MO sijakuunga mkono bado
 
kwa hayo mapesa yake, huyu si mbunge, bali ni mchuuzi wa wapiga kura!!!!!!!!

worse enough, anayapata ya bwerere kwa vile yuko ccm!

shame shame shame...............g.a.b.a.c.h.o.l.i orijino
 
nimemalizia madarasa manne pamoja na kujenga vyoo vya kisasa kwa thamani zaidi ya shilingi Millioni Arobaini na Tano (45 Milioni)

Natamani ningeona hayo madarasa 4 na vyoo vyenye thamani ya TZS 45m
 
Ututajie pia na kodi anazolipa ndiyo tutajua kama kweli hizo pesa ni halali na ana nia njema kwa nchi hii!!!
 
Aliyesema wajinga ndio waliwao hakukosea! Haka kajamaa utajiri wote huo wa kumwaga kameupata migongoni mwa wananchi wa Tanzania na Serikali yao halafu sie tunachekelea na kumsifu badala ya kumhoji atueleze iweje awe tajiri kiasi hicho miongoni mwa Wanyaturu maskini?

Anachokifanya Mo ni kutaka sifa tu hakuna jingine lolote la maana hapa. Hizo fedha anazotoa twashukuru kwamba ameamua kuzirejesha zilikotoka - kwa Watanzania aliowanyonya kwa kuwauzia bidhaa wananchi na Serikali yao na kupata faida kubwa mara hata 100 ya bei stahili. Hivyo ndivyo wafanyabiashara hasa wa asili yake wamekuwa wakifanya - kuwanyonya wananchi. Aliyesema ubepari ni unyama hakukosema hata chembe!
 
Inaonekana mradi wa trekta haukupangwa vizuri ndo maana linakaa bure!!!
 
Mimi nikienda gombea Singida watatupia 'Mbojo' lol. Babu yake Mo ni mchawi wakufa mtu. But Kinyambiss nimeamua kutumikia Taifa langu. Naombeni suggestions za jinsi yakumtoa huyu mwizi, anatuletea michele iliyo expire anatuua taratibu.


Kinyambiss for President 2020. I will fix all this.
 
Huyu kijana anafanyabiashara na baba yake na kuusaka ubunge ilikuwa ni njia moja wapo ya kuwekeza!! Unapowekeza ,unatarajia kupata zaidi ya kile ulichowekeza na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa huyu kijana; matumizi yake akiwa mbunge kwa yote aliyoainisha na asioainisha ni kidogo ukilinganisha na mapato aliyopata kwa kutumia influence ya ubunge pamoja na marupurupu ya ofisi hiyo! Mfanyabiashara yeyote hasa muhindi hawezi kutumia pesa yake mahala ambapo hanufaiki. Huyu kijana anawazuga hao wanyaturu kwa kuwahongahonga unga na khanga/fulana wakati wa uchaguzi halafu ukimalizika uchaguzi huyo anarudi maskani yake Oysterbay Dsm; sidhani kama hata ana makazi ya kudumu huko Singida zaidi ya maduka aliyopamga National Housing!!
 
Taifaaaaaa; (Itikia; Taifa letuuuuu) limenunuliwaaaaaaaa

Taifaaaaaa; taifa letu limenunuliwa
nasema kwheri kwaheri taifa la tanzania!

Inasikitisha ; tusubiri bei ya majimbo mengine!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom