TWisheshagi
Member
- May 2, 2020
- 14
- 209
NIMERUDIA kuisikiliza Hotuba ya Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mara kadhaa. Hii ni hotuba inaweza kudumu kwa muda mrefu sana kama rejea sahihi ya maamuzi sahihi yaliyowahi kufanywa na CHADEMA, tangu mfumo huu wa vyama vingi uanze.
Hotuba ya Mbowe, ni dawa ya kutibu misuli ya moyo katika siasa maamuzi mazuri yanayochelewa, ni mabaya zaidi kuliko maamuzi mabaya yanayokuja kwa wakati.
Katika siasa muda na nyakati ni muhimu zaidi kuliko tukio lenyewe. Maamuzi ya haraka ni ishara ya kudhibiti mipango miovu iliyotegwa kwa muda mrefu na wajanja wachache. Naipongeza CHADEMA kwa kuruka kihunzi hicho kilichokuwa kimetegwa.
Ieleweke kuwa katika siasa hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya matukio yote hupangwa. Na nyakati nyingine, huandaliwa mazingira fulani ili kuharakisha tukio jingine kutokea HONGERENI CHADEMA kwa kuvunja mpangilio wa matukio mengine yaliyokuwa yamepangwa kutokea ndani ya wiki hii inayoanza!
Chadema wamefanya maamuzi ambayo hata sisi ndani ya CCM hatuwezi kuyafanya tumekwisha kupoteza uhalali wa kufanya maamuzi kama yaliyofanywa na Chadema siku nyingi sana.
Chama chetu kiliwahi kuwa na uwezo na jeuri hiyo zama za Mwalimu Nyerere. Baada ya Mwalimu Nyerere, kutangulia mbele za haki, Chama chetu kilipoteza kila kitu:
Mosi, tulipoteza Baba wa Taifa. Nimeambiwa kwa sasa tumebakiza "Mashangazi" wa Taifa.
Pili, tulipoteza Mzee mwenye busara na hekima, mwenye uwezo wa kukemea hadharani bila kificho na mwenye uwezo wa ushawishi na maono
Kwa sasa hatuna mwanasiasa mshawishi ndani ya umma anayetokana na CCM.
Nje ya CCM wapo. Ukitaka mwanasiasa jasiri, mwenye ushawishi na NGUVU ya hoja mtafute Tundu Antipas Lissu.
Ukitaka mwanasiasa mwenye uwezo wa kuvumilia na usikivu uliovuka mipaka ya kawaida na aliyevuka mipaka ya kuwa mwasiasa na sasa ni mwanasiasa taasisi, mtafute MAALIM SEIF Sharrif Hamad.
Ukitaka mwanasiasa mwenye nguvu ya uchambuzi, mtafute Zitto Kabwe.
Ukitaka mwanasiasa mwenye nguvu ya maono, mtulivu wa hoja na mwenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha hoja zake kwa umma mtafute FreemanMbowe
Mbowe, ni mwanasiasa mwenye nguvu ya maono. Ukimsikiliza utanielewa kile nichozungumza hapa hawa ni wanasiasa wachache sana Taifa limewahi kuwa na Kuna kipindi ni natamani angelikuwa CCM ili aweze kuziba ombwe linalotukabili kwa sasa
Huku kwetu CCM, MUNGU wetu ni mkarimu. Ameumba watu wa aina mbalimbali. Wakiishaumbwa, hatuwezi kuwaumba tena Tunachoweza ni kuishi nao katika hali tusiyoweza kuibadili
WANA-CCM wenzangu, tuendelee kuisikiliza Hotuba ya Freeman Mbowe, ni dawa ya misuli ya moyo.
Ndimi Mkukima wa Bamia, Bonde la mto Simiyu-Magu,Mwanza.