Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia

-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola

-Kama ilivyo kwa madikteta wote,hata huyu anayetisha watu nae anahofu.Anataka kututia hofu kwa vyombo vya dola lakini sisi hatumuogopi kwani sisi tuna Mungu

-Natambua kuna wito wa viongozi wa Dini kutukutanisha.Hatukatai wito kwa kuwa tunawaheshimu.Tutawasikiliza na tutawaeleza msimamo wetu .

Magufuli ndiye anayevunja amani ya nchi hivyo viongozi wa Dini wamkanye kabla hali haijawa mbaya

-Tumeviandaa vyombo vya habari na vya kimataifa ili Septemba Mosi Dunia ishuhudie uovu wa Serikali ya Magufuli

-Tunajua hata baadhi ya Wana-CCM ni waathirika wa Uonevu Huu ,Wasio na vyama na wengine wote tunawakaribisha

Asanteni Wanahabari.Sasa tutaanza kikao chetu cha Ndani kwa mikakati kabambe

Tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi yenu
Eti Mbowe anamwonya Rais huu ni utovu wa nidhamu
 
Ngoja siku hiyo mtatambua km hapa duniani kumbe viumbe hai
 
mkuu september mosi mtakuta wao ndio wako nyuma yenu,kwa kuwa nyie ndo mtatangulizwa mbele nao watakuwa nyuma wakisoma upepo unavyokwenda,na punde mkigeuka nyuma mtajikuta mmebaki peke yenu wao hawapo tena.
Watanzania wote tungekuwa kama wewe nchi ingeshauzwa hii

Hujitambui wewe
 
Mbowe mbona anakimbia siku hiyo hatakuwepo tafadhali msimruhusu asafiri nje ya nchi hiyo tarehe 28th ndo asafiri siyo awaachie msara nyie wenyewe. Nayeye alipaswa ashike UKUTA maana Mh. RAIS ALISEMA NA WENYEWE WAWEPO SIKU HIYO SI KUWANUNULIA VIROBA WATOTO WA WATU NA KUWATANGILIZA
 
Hakuna mpango wa CHADEMA hata mmoja uliwahifanikiwa kila mission imefeli. Waulize hao CHAGADEMA Operation sangara iliishia wapi? Waulize M4C iko wapi? Safari ya matumaini iliishia wapi? mpango wa BAVICHA kuzuia mkutano mkuu wa CCM uliishia wapi? na hata huo UKUTA hawatakwambia umeangukia wapi. Yaani tunawasubiri kwa hamu hawa CHAGADEMA kuwaonyesha kazi tuliyotumwa na Amri jeshi wetu Mh. RAIS
 
hotuba imejaa uoga na undumila kuwili aisee!!! kama mwenye chama cha chadema anaongea kiuogauoga namna hiyo... je akina ben saanane wataandamana kweli😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛 chair wenu kajawa na hofu kiasi hicho??? huu ukuta ni wa mwendo kasi aisee!!😡
huyo ben saanane ndo wa kumuogopa kabisa,ni muhamasishaji wa bar tu kwenye nyama choma,siku hiyo hatakuwepo na hata hapa tutamkosa
 
Nategemea kutakuwa na watu zaidi watakaojiunga na UKAWA kwenye UKUTA kwani hili ni kitu kinahusu taifa zima siyo swala la upinzani. Mkuu wa nchi asiruhusiwe kutumia jeshi kuumiza watu wake kwa sababu yoyote ile.
 
Mbowe Mungu ampe maisha marefu ni kiongozi mwenye busara na hekima anayeheshimika ndani ya nchi na nje ya nchi kwenye hotuba zake ameongea ukweli operesheni #UKUTA maandalizi yanaendelea kama ilivyopangwa hakuna kurudi nyuma.
Fears has no power.....Go mbowe
 
Acheni uongo UKUTA ni wakwenu nyie CHAGADEMA hata CUF wamesema hawausiki. Mkumbuke Magufuli alichaguliwa na wananchi kwa kiasi kikubwa na ndio maana CCM ilipata majimbo 190, UKAWA majimbo 39 na democrasia ya kweli chama kilichoshinda ndo kinaongoza na kufanya maamuzi. Kwanini mnafanya fujo? wakati wananchi waliwakataa ndo maana mkapata majimbo machache?
 
Mwambie mwenyekiti ajumuike na sisi kwenye maandamano siyo tupigwe sisi yeye akituangalia kwenye TV tu na familia yake
Pigwe kwa kosa gani?Umepitia Katiba ukaona kuandamana ni kosa.Hao Polisi ndio wanavunja katiba dada angu
 
Kipondo kinazidi kujaa kwenye sidemirror, days are numbered tusubiri tuone maake siku hiyo ina matukio makuu matatu:-
1 . maadhimisho ya JWTZ tangu kuundwa kwake.
2. Inasemekana kutakuwa na tukio la kupatwa kwa jua.
3. Pia itakuwa ni siku ya kipondo kwa wana ukuta. Let's wait and see.
 
Msipotoshe Umma watakaoandamana siku hiyo ni CHADEMA peke yao na si wana CUF, wala wanaCCM, TLP, UDP , ACT nk. Mrikurupuka kufanya maamuzi ndo maana vyama karibu vyote vimewagomea kuwaunga mkono ' Actually our president is doing well'' God bless Magufuli we play for you
 
Magufuli ameshawaambia watangulie viongozi wa chadema kwenye maandamano wakione cha mtema kuni
Na magufuli naye atangulize familia yake kuzuia ukuta bila kumsahau Jesc.a sio kutanguliza hao askar wenye maisha duni.
 
Back
Top Bottom