Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Chenge,Bulembo,uvccm,mnunua MV DSM na majambazi wengine wote ccm.
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia

-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola

-Kama ilivyo kwa madikteta wote,hata huyu anayetisha watu nae anahofu.Anataka kututia hofu kwa vyombo vya dola lakini sisi hatumuogopi kwani sisi tuna Mungu

-Natambua kuna wito wa viongozi wa Dini kutukutanisha.Hatukatai wito kwa kuwa tunawaheshimu.Tutawasikiliza na tutawaeleza msimamo wetu .

Magufuli ndiye anayevunja amani ya nchi hivyo viongozi wa Dini wamkanye kabla hali haijawa mbaya

-Tumeviandaa vyombo vya habari na vya kimataifa ili Septemba Mosi Dunia ishuhudie uovu wa Serikali ya Magufuli

-Tunajua hata baadhi ya Wana-CCM ni waathirika wa Uonevu Huu ,Wasio na vyama na wengine wote tunawakaribisha

Asanteni Wanahabari.Sasa tutaanza kikao chetu cha Ndani kwa mikakati kabambe

Tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi yenu

Si ndio huyu aliahidi bungeni kuwa angerudisha shangingi lake? Hivi alirudisha?
 
Dah aseeee. Na wahurumia wafata mikumbo yaani watu wa kipato cha chini ., wale wenye thamani ya dola moja......ndiyo. sana aseeee..................ushauri wangu ni huu,,,,achaneni na siasa ,azina faida,,,,,,,...,cha msingi. Tafuteni fulsa za kuwaongezea kipato ......fulsa zipo nyingi tyuuu aseeee sana sana kilimo na ufugaji......""huu ni ushauri Wangu...ka ukipuuza fuata hizo siasa mchana na usiku Fanya majumuhisho ya ulichokipata...zaidi ya maumivu tu mwilini.......""""no matusi ,,

Siku na hata huto tumifugo watakapokuja na kujitwalia ndipo utakapokumbuka umuhimu wa kudai demokrasia!
 
W
Kweli ni stupidity, Ibilisi amewajaza roho chafu hata hawaijui thamani ya Watanzania wenzao. Ila wamuulize Mzee Mkapa, alivyowaua Watanzania kwa kuwaita Wapemba, Wazee wote wenye akili na busara walimbadilikia mno. Nakumbuka Mzee Waryoba kama sijakosea alifika mahali akatamka wazi kuwa Jeshi la Polisi lililoanzishwa na kulipwa kwa kodi za Watanzania haliwezi kuwageuzia bunduki na risasi zilizonunuliwa kwa kodi zao. Hata Majaji wa wakati huo walikuja juu. Magufuli asidhani wenye akili na busara watamchekea.
ewe unamtisha magufuli au unataka kusemaje?
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia

-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola

-Kama ilivyo kwa madikteta wote,hata huyu anayetisha watu nae anahofu.Anataka kututia hofu kwa vyombo vya dola lakini sisi hatumuogopi kwani sisi tuna Mungu

-Natambua kuna wito wa viongozi wa Dini kutukutanisha.Hatukatai wito kwa kuwa tunawaheshimu.Tutawasikiliza na tutawaeleza msimamo wetu .

Magufuli ndiye anayevunja amani ya nchi hivyo viongozi wa Dini wamkanye kabla hali haijawa mbaya

-Tumeviandaa vyombo vya habari na vya kimataifa ili Septemba Mosi Dunia ishuhudie uovu wa Serikali ya Magufuli

-Tunajua hata baadhi ya Wana-CCM ni waathirika wa Uonevu Huu ,Wasio na vyama na wengine wote tunawakaribisha

Asanteni Wanahabari.Sasa tutaanza kikao chetu cha Ndani kwa mikakati kabambe

Tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi yenu
Hii gia haina tija tena, lyk serious' ,mtoke bungeni then uaminishe jamii iingie barabarani...
Dola itawajibika na nyie tu sabab ndo kazi yao...
Wanatoa onyo X3 then action...
Ht km mtaalika wana habari wa mars au jupiter,nothing will change as long huu ujinga wa kujtakia ulemavu hauvumiliki...
 
hotuba imejaa uoga na undumila kuwili aisee!!! kama mwenye chama cha chadema anaongea kiuogauoga namna hiyo... je akina ben saanane wataandamana kweli😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛 chair wenu kajawa na hofu kiasi hicho??? huu ukuta ni wa mwendo kasi aisee!!😡
 
Cha ajabu nilikuwa naangalia location zenu wachangiaji mojowapo ya watu wanaotukana na watu wa Arusha na Moshi kwa nini inamaana nyie bado mna akili ya kuendeleza ukabila?Kuna mtu mmoja anajifanya mkali sana lakini hata kiganja cha tumbili hajai..looh pole sana
 
Mwenye mtizamo wa ukabila kwa swala la kitaifa kama hili anaonyesha ufinyu wa akili zake.
 
Jose tajiri,

Tutaweka video baada ya hizi Updates .
Wanafiki wakubwa.

Tokea waruhusiwe kuandamana ,Mbowe hajaitisha mkutano hata mmoja huku Hai , wananchi wa Hai tunataka maandamano .

Mbowe anakomalia kwenda kuandamana jimbo la Kahama kutafuta nini??
 
Kwahiyo kwa akili zako za CBE mwenyekiti wako akisema anaongoza ng'ombe na wewe unachukulia literally kabisa hao wananchi ni ng'ombe?...

Sasa wewe "mwanaCBE" una mandate gani kumwambia mwingine apige kimya?Hivi CBE ni univeristy?Nimesahau kidogo....if u can see my super sarcasm[emoji111]️[emoji111][emoji111][emoji23][emoji23][emoji23]

Nakufaninisha na yule jamaa aliyezaliwa na kulelewa kule usukumani leo kapata kanafasi anakataza watu wasiende jijini Dar.
Kama shida yako ni kujadili majina ya vyuo anzisha uzi wa aina hiyo utafuatwaa na watu wa aina yako huko.
Acha kung'ang'aniza ung'ombe wako hapa.
 
Wanafiki wakubwa.

Tokea waruhusiwe kuandamana ,Mbowe hajaitisha mkutano hata mmoja huku Hai , wananchi wa Hai tunataka maandamano .

Mbowe anakomalia kwenda kuandamana jimbo la Kahama kutafuta nini??

Una mizuka hatari we dada. Sijui umejifunzia wapi hii kitu
 
Siku CHADEMA ikiacha udini , Ukabila , kukumbatia UFISADI, Kumfukuza Lowasa na ukanda wa kaskazini watakubalika kwa Wananchi
 
Eti amuonya vikali, ajaribu kuandamana iyo tar moja ndio tutajua nani alionya vikali kati yake na presdent
 
Back
Top Bottom