Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Habari Mkuu,Ben saanane!!

Nasubiri updates za kina pamoja na Kauli rasmi ya Maandamano ya Tar 01.Asiishilie kuwataka wananchi katika maandamano tu,bali nitafarijika kama atasema tutakuwa Mstari wa mbele na wake zetu,Nategemea siku hiyo kumuona Mama Lowassa,Mama Mbowe,Mama Lissu na wake za viongozi woote wa UKUTA.
Mwambieni na mkemia wenu na mke wake na nyumba yake ndogo ya Bamaga ajitokeze kutukabili barabarani asiishie kusema ye hajaribiwi wakati anajua hali ikiwa ngumu watawala wa aina yake hukimbiwa na polisi na majeshi wanayodhani yanawatii!
 
Amsha amsha hizi tulishazizoea. Jpm natamani afanye kama ninavyofikiria
 
dah.. hii mikwala sasa n too much.... bora hyo cku ifke tuone
 
Mbowe hana uwezo wa kumuonya Magufuli yeye uwezo wake ni kuwapangia majukumu hao mawaziri wakuu wastaafu Sumaye na Lowasa uwezo wa kumuonya Magufuli hana.
Tar.1 aongoze maandamano yeye na Joyce Mukya nyumbu wengine ndio wafuate tena aanzie kwao Kilimanjaro.
Hata mimi namuonya aache ubabe usio na maana mara moja na pia aache matamko yanayoingilia haki za wengine zilizoainishwa kwenye Katiba na sheria mara moja. Kama hajui kitu juu ya Katiba na sheria amtafute Prof. Shivji ampe tuition, maana najua wapambe wake akina Mwakyembe na Masaju watakuwa wanaogopa kutumbuliwa naye. Nikiwa raia ninayo haki ya kumuonya kiongozi yeyote anayevunja sheria za nchi.
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia


-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola
Tafadhari na wao viongozi wawepo tena mstali wa mbele
 
Freeman mbowe icon ya mabadiliko na demokrasia Tanzania

Tupo nyuma yenu viongozi wetu wakuu
mkuu september mosi mtakuta wao ndio wako nyuma yenu,kwa kuwa nyie ndo mtatangulizwa mbele nao watakuwa nyuma wakisoma upepo unavyokwenda,na punde mkigeuka nyuma mtajikuta mmebaki peke yenu wao hawapo tena.
 
PhD holder wa chemistry mwambieni awaelezee alichosomea kwa kiingereza NDIO MTAMUONA ALIVYO MKALI KAMA PILIPILI
 
Wanamuonya rais vikali na hapo hapo wanasema huu ni utawala wa kidikteta. Makubwa. Wanafahamu ni nini wanachoongea? Huu uasi wa wazi wazi ni lazima ukomeshwe. Hauvumiliki.
Waliochochea mauaji Rwanda ni kitengo cha Umoja wa Vijana wa EMRD waliokuja kujulikana kama Interahamwe. Hawa hawakujali ikiwa dola iliwatesa au hata kuwaua watu, maadam waliouawa ni Watusi kwao ilikuwa sawa tu. Leo historia ile inajirudia Tanzania kwamba Vijana wa CCM wanashangilia haki za kiraia kuvunjwa ilimradi anayefanya hivyo ni rais anayetokana na Chama chao. Lakini historia ni mwamuzi wa haki kwamba huwezi kuishi kwa upanga, ukadumu kwa upanga. Wako wapi Wahutu wale? Wamepotea katika pazia la historia.Huwezi kuwavunja miguu Watanzania wasio na hatia kwa sababu tu unajivunia nguvu za dola ambao ni watoto wa Watanzania hao hao. Huwezi!!
 
Waliochochea mauaji Rwanda ni kitengo cha Umoja wa Vijana wa EMRD waliokuja kujulikana kama Interahamwe. Hawa hawakujali ikiwa dola iliwatesa au hata kuwaua watu, maadam waliouawa ni Watusi kwao ilikuwa sawa tu. Leo historia ile inajirudia Tanzania kwamba Vijana wa CCM wanashangilia haki za kiraia kuvunjwa ilimradi anayefanya hivyo ni rais anayetokana na Chama chao. Lakini historia ni mwamuzi wa haki kwamba huwezi kuishi kwa upanga, ukadumu kwa upanga. Wako wapi Wahutu wale? Wamepotea katika pazia la historia.Huwezi kuwavunja miguu Watanzania wasio na hatia kwa sababu tu unajivunia nguvu za dola ambao ni watoto wa Watanzania hao hao. Huwezi!!
Umebaki kulia lia kama mtoto mchanga. Unafananisha Rwanda na huu upuuzi wa Ukuta? Subiri tarehe moja haki ya nani.
 
Back
Top Bottom