Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

We acha wee wee! Huna anachomiliki Mbowe! Acha kutukana usiowafahamu. Kuna viongozi kibao walifeli fm6 wakaresit Leo wana PhD.
 
Nilikuwa siamini, kumbe Mbowe ni ziro!
Eti maadamano ni uamuzi wa kamati kuu! Kwani kamati yenu kuu sisi inatuhusu nini au ni msaafu kwamba lazima tufuate?
Mmeunda makundi matano, je mmepata mrejesho wa kazi ya haya makundi? Mfano, Sumaye afanye mahusiano ya kibunge na serikali, je hiyo timu imefanikiwa kiasi gani!
Kundi la Lisu limeandaa mashtaka 21, hayo makosa mmeyapata wapi kabla ya tarehe maadamano? Yani kabla hamjatandikwa na dola!
Kama hamjaua UKAWA kwa nini msisubiri wenzenu CUF wamalize uchaguzi ili muwe pamoja Kama timu?
Na tangu lini NCCR wakatii maagizo ya kamati kuu yenu, wasitii maagizo ya chama chao?
Mbowe unataka fujo zenu zitulizwe na vijana wa ccm? Tangu lini vijana wa chama wakafanya kazi ya polisi?
Mbowe nakuuliza tena lengo lako nini kwa nchi hii?
Labda nikueleze, tuliwapigia kura kwa sababu tulitaka mabadiliko baada ya kuchoshwa na ccm, siyo kwamba tulikipenda chama chenu!
Bila Dr Slaa siyo muda mrefu chama chako kitakuwa marehemu
Unaongea kama vile umeshikiwa Kisu, halafu unalazimishwa kushika UKUTA!
 
akili sio shule uliza kina baresa.moo.mengi diamond kama wana hizo pHD NA JE WANA NJAA ? KUONGOZA sio elimu kwani ingelikuwa elimu mimi nimesoma chemia , chemia yangu inaweza kuwaongoza?

Mwambie leaders are born not made
 
Mbona msemaji mkuu wa chama chetu alizungusha fomu six lakini unauchuna? Btw, mbona hata mawaziri wetu wengi tu walifeli baadaye wakarudia madarasa. Lakini ili mjadala unoge hebu weka kwanza matokeo yako hapa badala ya kuponda wenzako ukiwa mafichoni!

Sio huyo tu mwenyekiti Phd holder hawezi kujitambulisha kwa kiingereza alichotumia kujifunzia chemistry
 
Kilimanjaro walishajikomboa kutoka kwenye makucha ya mkoloni mweusi ccm
Ccm ni chama cha watanzania wote, nyie Wachaga acheni kuita watanzania wakoloni weusi.. Mpaka nchi iongozwe na mchaga ndio mnaona mmepata ukombozi.
 
Kama hili swala lina umuhumu wa kuwahusisha wenyeviti kama mwenyekiti wenu anavyotaka? kama vile Dikiteta hali Nduli Idi Amini alivyo wahi kuomba wazichape kavu na Mwl. Nyerere, mwambieni Dikitete U.ch.wa,ra aombe kuzicha kavu na Kamanda Mbowe.
nakuhakikishia hilo likitokea kile kijamaa hakitampiga huyo mumeo makengeza,,, KITAMTAFUNA KABISA
 
Chadema ishapoteza uthabiti wake, ilivuma zamani wakati kauli lengo lao kuu likiwa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Mali za Umma za watawala wa awamu ya 4 Ila sasa ndio wamekaribisha Ufisadi kwenye chama. Kwa hilo wameshapoteza lengo Na kupunguza washabiki pia, watakaobaki ni hao Tu walio Na maslahi Na Chadema Ila Kwa Number ya washabiki imeshapotea Na Siasa is a Game of Numbers.
 
Mbowe kawa mwenyekiti wa Chadema tangu 2004 ,wala hawazi kuachia madaraka kwa wengine, ela zote za ruzuku anazimaliza yeye ofisi za mikoani na wilayani hata ela ya pango wanashindwa kulipa ofisi za wilaya na mikoa za Chadema zipo kwenye hali mbaya sana.
Waambie Takukuru waende wawakamate kama walivyo wakamata uvccm kwa kuiba millioni 200 na kukwapua mali za chama
 
Mwambie mwenyekiti ajumuike na sisi kwenye maandamano siyo tupigwe sisi yeye akituangalia kwenye TV tu na familia yake
Mbowe and Co ni watu wa maji moto, kwenye moto wenyewe huwa wanasepa.
Ili tumuamini ilikuwa asememe wazi yeye na failia yake wataandamana wapi tupeleke kamera zetu
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia


-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola
Mbowe anaji.harishia kuona vikosi, asiondoke nchini hiyo sept 1, awe mbele sio kutetea mafisadi kwa kigezo cha demokrasia!
 
Unaandaje mashtaka kabla hujatendewa kosa! Kuandamana lazima OCD atoe go ahead vinginevyo na UKUTA nao wakiandamana bila ridhaa ya OCD nao pia watakua wamevunja katiba.
 
Back
Top Bottom