Hotuba nzuri sana......
I like it.
"HOTUBA YA ALBERT ONDO ASSA ILIBADILI FIKRA ZA MAJESHI YA ALLY BONGO?!
------------------------------------------
Siku ya kufunga kampeni za uchaguzi mkuu wa Gabon uliofanyika siku kadhaa nyuma. Mgombea u Rais wa upinzani mwenye ushawishi na idadi kubwa ya wafuasi nchini humo. Bwana Albert Ondo Assa.
Alifunga kampeni zake kwa kutoa hotuba nzito juu ya majeshi ya Gabon. Mimi nimeitafsiri kwa kiswahili hotuba ile hapo chini isome.
"Majeshi yote ya nchi hii. Amkeni kutoka katika lindi la usingizi mzito ambao kimfanano haupishani sana na kifo. Tazameni idadi ya maskini vijijini. Hurumieni vijana wanaovuja jasho bila ajira mijini. Jiji la Libreville limejaza omba omba.
Kuwa na idadi kubwa ya makabwela. Juu ya ardhi ambayo imebarikiwa utajiri wa mafuta. Hii ni laana.
Wakati huo huo familia ya Ally Bongo na watu wake. Wakiishi maisha ya kitajiri kufuru na anasa.
Majeshi, polisi na vikosi tihifu vya Ally Bongo. Safari hii ziambieni bunduki zenu. Tumechoka kuilinda dhambi ya wizi wa kura kwa mtutu wa bunduki."
Majeshi! angalieni kipindi cha uchaguzi mnavyopiga, kutesa, na hata kuua wafuasi wa upinzani. Chaguzi za Gabon ni zaidi ya kuitazama filamu ya kutisha iliyoshutiwa kuzimu. Chaguzi za Gabon zinanuka jasho la mauti.
Polisi waheshimiwa msikubali kutumiwa. Angalieni makazi yenu yalivyochoka kama mabanda ya njiwa.
Nani anayewatuma?! muende mafunzoni na kisha mrudi kuilinda dhuluma?! Kama ni familia ya Ally Bongo na vibaraka wake iambieni, "sasa yatosha."
Ardhi ya Gabon inalia, inasononeka, inaomboleza, inaugua. Kwa kuwa nyie mmekuwa sehemu ya watu mnaolinda wasaliti na wezi wa maliasili za taifa hili.
Msisimamie haki, bali simameni kuhakikisha haki inatangazwa pale inaposhinda.
Kama Gabon itaendeshwa kwa haki usawa na hofu ya Mungu. Kila mtu wa taifa hili atajihisi yupo paradiso."